Mara zote huwa tunashauriwa kutizamana machoni wakati wa usaili wa kazi. Kwangu mambo sio mazuri kama nafanyiwa usaili na mwanamke, huwa siwezi kumwangalia machoni kwa muda mrefu.
Je, kuna mtu anachangamoto kama yangu? Njia za kutatua hilo ni zipi⁉️🤗
Kutizama mtu machoni haina maana umuangalia muda wote mpaka inakuwa kero au kutafsiri vingine
Ina maana kuwa uwe concentrated na interview yako
Akili isiende kwingine
Kuna wengine kwa mfano anakuwa mbele kuna dirisha na mda mwingi anaangalia nje tu
Au kuna picha unabaki kuiangalia tu au saa nk
Kwa hiyo sio lazima ukodoe macho tu kwenye uso wake kama unamchora