Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Leo, Tanganyika aka danganyika, na hata Zenj zinasherehekea siku ya uhuru. Kwa uchakachuajin uchaguzi, utekaji, mauaji, ufisadi, uchaawa, ubabaishaji, maisha magumu kwa walio wengi na mazabe mengine mengi, kweli tunasherehekea uhuru au udhuru? Je watanzania kwa ujumla wao ni huru? Je haya ndiyo mategemeo, ahadi, na matunda ya uhuru ambapo wachache wananeemeka huku wengi wakiteketea na kutopea kwenye umaskini wa kutengenzwa? Je huu uhuru tunauona majumbani, mezani na kwenye maisha yetu kama watu jamii na nchi? Hebu tuudurusu na kuutathmini huu uhuru.