MUWHWELA
Senior Member
- Oct 26, 2013
- 167
- 238
Habari njema ni kwamba unao UHAI basi jipe shukrani na shukuru viumbe wengine.
Nitajikita kwenye jambo moja tu ambalo binafsi naliona kama ni tatizo la msingi kabisa (Mashindano Katika mambo yanayohitaji ushirikiano).
Elimu ni nyenzo muhimu sana katika ustawi wa MTU mmoja mmoja, familia na taifa kwa ujumla wake. "ELIMU" vyovyote utakavyoielezea utakuwa sawa maana yenyewe ni concept siyo fact.
Elimu ilipaswa igawanyike Katika sehemu kuu mbili
1-ELIMU AWALI - Hii ni Elimu ambayo Kila Binadamu aliyezaliwa na mwanamke anakuja nayo,hata wale wanaozaliwa na mashine kwakuwa amepewa pumzi ya UHAI na Mwili basi Elimu hiyo anakuja nayo.
Kila MTU anayo hiyo Elimu, maana hiyo ndiyo center ya vyote vinavyoonwa na macho ya nyama, ubunifu wote unao uona hapa duniani ni kutoka kwenye taarifa anazopewa MTU wakati anapewa kibali Cha uhai na (Mungu) Mwenyewe kama unaamini Katika MUNGU.
Hii Elimu ilipaswa itabuliwe na mamlaka Ili Kila MTU afanywe huru Ili aonyeshe kile alichopewa na Mungu wakati anakuja duniani, kulikuwa hakuna ulazima wa kumfundisha MTU (aeiou),au (123456689) as foundation, ilipaswa serikali ijue nani alikuja na nini kwajili ya ulimwengu huu.
Swala la age is not a big deal ,hakuna sababu ya mtoto wa miaka 2,3,4,5 aanze shule Tena siyo shule tu, shule ya ushindani, hapana hapana...acha mtoto aanze kusema na kuonyesha alichokuja nacho kabla ya kuambiwa anachotakiwa kuwaza. Tumekosea na tunaendelea kukosea.
Mwisho wa siku Kila MTU ataondoka hapa duniani akiwa anatafuta ulinganifu na MTU Mwingine badala ya kufikiri kuhusu suluhu ya matatizo ya ulimwengu, ambapo Hilo ndilo jukumu la msingi la MTU kupewa Mwili na UHAI (Kuna viumbe wengi hawana Mwili na wanaishi,Bali wewe na Mimi tumepewa miili Ili tuwe jawabu mahala)
2-ELIMU YA PILI (UPILI) MAPOKEO - Siyo vibaya kujua wengine wanafanya nini na wanafanya kwa kutumia kanuni zipi, ni jambo muhimu pia kwa minajiri ya ushirikiano.
Tukifahamu primary need kwamba ni kutambua vipaji basi next inakuwa Kufahamu mifumo Mingine, haviwezi kuwa vitu vya ushindani Bali mashirikiano yanayoleta matokeo Chanya ya kufikia malengo Yale Kila MTU ambayo amepewa kuyatimiza kwa wakati maalumu wa UHAI wake.
Hii ya kupanga MTU wa kwanza mpka wa mwisho ni mfumo wa kikoloni ambao mantiki yake haielezeki kwa MTU MTU mwenye utimamu wa kufikiri, oky wewe wa kwanza then? Does that change your emotional intelligence? HAPANA
Kwenye maisha ya kawaida hatushindani maana safari zetu hazina ufanano kwa umbali tunaendao na wajibu tulioubeba. Why ushindane?
Hao walioleta mifumo Yao ya Elimu miaka hii hawaiishi Tena hayo,tech inawakusanya watu wengi kwa umoja wao na vipawa vyao kuleta suluhu ya matatizo duniani. Haya ndiyo yanayotakiwa kwetu pia.
Natamani niendelee lakini kwa uchokozi tu wa maada basi tunaendelea kwa kadri majadiliano yatakavyokuwa.