Tunashukuru Rais Samia unatujali Wafanyabiashara

Tunashukuru Rais Samia unatujali Wafanyabiashara

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Umekuwa nasi bega kwa bega. Hakuna kipindi kama cha awamu ya tano ambacho sisi wafanyabiashara wakubwa tuliishi kwa wasiwasi na mashaka

Hili la kuwajulisha watanzania kuwa vitu vitapanda bei limenipa faraja sana. Maana sasa waelewe kuwa vita vya Russia na Ukraine vinaiathiri dunia sana. Mafuta ya Vyombo vya Usafiri, ya Kula, ya kupaka. Sabuni, Sukari Mchele, Unga, Nyama, Maharagwe n.k lazima vitaathirika.

Awamu ya tano ingetaka kutumia ubabe kuzuia sisi wengine kupandisha bei. Tulinyanyasika sana sisi wafanyabiashara wakubwa. Lakini sasa tunajisikia amani na tunarudisha kilichoibwa na kupotezwa.

Mwaka 2025 hauna Upinzani. Ni wewe tu. Endelea kutukumbuka pia katika kodi....tupunguzie kodi mama. Tunaingiza mizigo mikubwa kodi ipunguzwe. Kodi inaweza ingizwa kwenye tozo na makato mengine. Tuliteseka sana.

Tunashukuru sasa Watanzania watakuwa tayari kukabiliana na bei zetu hizi pasipo manung'uniko au lawama. Maana wanapenda sana lawama.
 
Umekuwa nasi bega kwa bega. Hakuna kipindi kama cha awamu ya tano ambacho sisi wafanyabiashara wakubwa tuliishi kwa wasiwasi na mashaka

Hili la kuwajulisha watanzania kuwa vitu vitapanda bei limenipa faraja sana. Maana sasa waelewe kuwa vita vya Russia na Ukraine vinaiathiri dunia sana. Mafuta ya Vyombo vya Usafiri, ya Kula, ya kupaka...
Yaani unasema kodi ziingizwe kwenye tozo, ili watumiaji wa mwisho waongezewe mzigo...?!
 
Mama apunguze utitiri wa Kodi ili Wafanyabiashara nao wapunguze huu mfumuko wa bei.

Mafuta yamejazwa kodi kuliko bidhaa yoyote ile

Toba Maulana!
 
Nchi zinazojitambua👇
AARD4K.jpeg
Tanzania mpaka kauli zitapanda bei👇
 
Back
Top Bottom