Tunashukuru sana kamati ya usajili Yanga nusura tupigwe yule Inonga badala ya Bangala

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Wakuu,

Kama mnakumbuka wakati wa usajiri kipindi kile yanga kulikuwa na majina mawili mezani,wote wakiwa ni wacongo man
Yaani yanick bangala na henock inonga injinia alianza kumfuata kwanza inonga ambaye akaanza kuleta mashauzi kama mwanamke ndipo injinia akasafiri mpaka Morocco kumfuata kiraka bangala litombo ambaye alisajiriwa kama beki wa kati..hivyo inonga mpango ukafeli na akaenda simba.

Lakini kufikia sasa tunaona usajiri upi ulikuwa wa faida zaidi
Kwanza bangala anacheza namba nyingi na amekuwa mchezaji muhimu zaidi kikosini.

Huku kazi yake ikionekana kwa kiwango kikubwa na kukubalika...mara nyingi amekuwa akicheza kama kiungo wa chini kitu ambacho inonga hawezi kwani hana ubavu..

Mpaka sasa bangala amechangia mafanikio kwa team yake ikiwemo kutengeneza ulinzi imara na kupelekea yanga kuwa unbeaten mpaka sasa na ikiruhusu magoli machache zaidi..

Huku inonga huko simba akigeuzwa kichaka cha walevi kumalizia haja zao wazi wazi, amekuwa ni mchezaji mwenye sifa na maneno mengi kama muimba taarabu na pia ametengeneza ukuta mbovu na mwenzie onyango hali iliyopelekea kukosa kombe msimu huu na kutobolewa mechi mbili tena na vibonde kagera na angalau team nzuri mbeya city,

Kwa mantiki hii unaona namna yanga walivyonusurika kupigwa za uso kwa inonga kama ambavyo walinusurika kuuziwa mbuzi kwenye gunia kwa Ibrahim ame ,ambaye muda sio mrefu atarudi kwao Zanzibar kucheza ndondo.

Huyo simba waliingizwa chaka wakidai ni zaidi ya mwamnyeto leo hii inadhihirisha wazi huku bakari akiwa ndiye beki ghali zaidi wa kitanzania kwa sasa..

Simba wanapaswa kusajiri kitaalamu kama yanga
 
Kutokana na kutambulika kwangu humu jukwaani kuwa ni mshabiki wa mwananchi, lakini ukweli kabisa Inonga ni bonge moja la beki. Ni beki haswa bila ya Inonga, Simba walikuwa wameruhusu magoli mengi kuliko ilivyo sasa. Huyu ni beki anaye sahihisha hadi makosa ya wenzie. Yanga tungempata huyu jamaa aisee Bangala asingekuwa na majukumu mengi angeenda zake kwenye kiungo na fundi mwenzie Aucho.
 
... bakari akiwa ndiye beki ghali zaidi wa kitanzania kwa sasa..
Simba wanapaswa kusajiri kitaalamu kama yanga
kuwa ghali unaweza pia ukawa ni uamuzi wa mnunuzi. Inawezekana akaenda dukani kuulizia kiatu cha sh. laki mbili kama kipo, na wauzaji wakakwambia ni hiki hapa, kumbe walikuwa wanakiuza sh. elfu thelathini
 
kuwa ghali unaweza pia ukawa ni uamuzi wa mnunuzi. Inawezekana akaenda dukani kuulizia kiatu cha sh. laki mbili kama kipo, na wauzaji wakakwambia ni hiki hapa, kumbe walikuwa wanakiuza sh. elfu thelathini
Muache mkuu itakuwa hajui Man U tulimnunua bei gani Maguire
 
kuwa ghali unaweza pia ukawa ni uamuzi wa mnunuzi. Inawezekana akaenda dukani kuulizia kiatu cha sh. laki mbili kama kipo, na wauzaji wakakwambia ni hiki hapa, kumbe walikuwa wanakiuza sh. elfu thelathini
Amekuwa ghali sababu pia ni mchezaji muhimu na mzuri tena tegemeo.na ndio maana tumetambua thamani yake.

Huoni van djik pale Liverpool? Analipwa mshahara mzuri sababu ya kazi yake..!
 
Inonga anakuwa staa pale anacheza na MAYELE
 
Inonga arudishe haraka jezi ya mayele kabla hayajamkuta, na mayele aache undezi wa kubadilishana badilishana jezi na wachezaji washirikina wanso pretend kuwa marafiki zake…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…