Tunasubiri kauli ya Waziri wa Wizara ya Nishati juu ya bei elekezi ya kuunganishwa umeme

Tunasubiri kauli ya Waziri wa Wizara ya Nishati juu ya bei elekezi ya kuunganishwa umeme

Chendembe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
444
Reaction score
488
Wanabodi, bila shaka tunafahamu kauli za mtangulizi wa Wizara ya Nishati kuhusu malipo ya gharama za kuunganishiwa umeme ya TZS 27,000.

Nafikiri tuliowengi tuliunga mkono tamko hilo kwa mantiki kwamba miundombinu si mali ya anaeunganishiwa. Hata hivyo, kwa maoni yangu ni Kama vile kumekuwa na mkwamo wa utekelezaji wake.

Labda taratibu za kupanga bei zilikiukwa, au mazowea tuliyojizowesha kulipia gharama ambazo hazitugusi moja kwa moja, au shirika halikiridhia kwa mazoe ya kupokea pesa isiyozingatia uhalisia wa majukumu yao na umiliki wa miundombinu.

Ni busara kabla ya yote, kutatuwa mkwamo huu ili wananchi tujuwe mbivu na mbichi.
Kazi iendeleeeeee
 
Hilo neno TAMKO ndio tatizo kubwa kwenye siasa za Tanzania kwasababu mtu anaweza kuamka nyumbani kwake akatamka chochote tu kwasababu ana mamlaka.

Ilitakiwa kwanza iundwe mikakati ya utekelezaji wa hayo mambo ndipo ipitishwe sheria ili utekelezaji uwe smooth bila kelele yoyote. Sasa kwa haya matamko bila strategies ni maigizo tu hakuna cha maana.
 
Kwakuwa lilishatamkwa, ni vema Sasa kutamkwa Kama liendelee au laa, kwa kuzingatia tamko litakalotolewa Lina athali kubwa kwa Serikali, wananchi na shirika
 
Kwani hilo lilikua tamko la Medard Kalemani kama yeye au lilikua tamko la waziri/wizara/serikali?
 
Tamko ni kuunganishiwa umeme ni TSh 27000 iwe mwendo wa haraka au wa pole! Maana hata wakisema kuunganishiwa lazima ulipe milioni tano, pace ya TANESCO itakuwa ni ile ile. Ila ukitaka pace ya TANESCO iongezeke tamko liseme hivi: 'HELA YA KUUNGANISHA UMEME WALIPWE WAFANYAKAZI WA TANESCO WANAOUNGANISHA UMEME NA WASITOE RISITI - HIZO HELA ZIWE ZAO'!
Baada ya mwezi nchi yote itakuwa na umeme!
 
Kwani hilo lilikua tamko la Medard Kalemani kama yeye au lilikua tamko la waziri/wizara/serikali?
Ni wakati Sasa kubainisha Kama ilikuwa yaSerikali au sio, na tuone utekelezaji wake
 
Kitu kilipishwa na Bunge na wala so Tamko la Kalemani,,lakini pia hata tannesco kunavipeperushi vipo vinasema kuunganishiwa umeme iwe Rea au Tanesco ni 27elf.

Pia kumbuka Tanesco wanapewa pesa byibgi na serikali kama Ruzuku ambazo ndo kodi hizi zetu ,,so ni haki watanzania kulipia elf 27 kwani wanakuwa wameilipa tanesco kupitia kodi zingine zinaOenda kama ruzuku Tanesco.

Angekuwa Magufuri angeweza shida ni hawa wapya wanamazoea ya kiazmani
 
27000 siyo gharama halisi, imekaa kisiasa zaidi. Vinginevyo Tanesco itakufa soon
 
Wanabodi, bila shaka tunafahamu kauli za mtangulizi wa Wizara ya Nishati kuhusu malipo ya gharama za kuunganishiwa umeme ya TZS 27,000.

Nafikiri tuliowengi tuliunga mkono tamko hilo kwa mantiki kwamba miundombinu si mali ya anaeunganishiwa. Hata hivyo, kwa maoni yangu ni Kama vile kumekuwa na mkwamo wa utekelezaji wake.

Labda taratibu za kupanga bei zilikiukwa, au mazowea tuliyojizowesha kulipia gharama ambazo hazitugusi moja kwa moja, au shirika halikiridhia kwa mazoe ya kupokea pesa isiyozingatia uhalisia wa majukumu yao na umiliki wa miundombinu.

Ni busara kabla ya yote, kutatuwa mkwamo huu ili wananchi tujuwe mbivu na mbichi.
Kazi iendeleeeeee
Hapa wauza nguzo wapo,na watumia rea kujenga mazingira ya rushwa wapo,huenda maelekezo yakaondo uchafu huo.
 
Umekuja kwa gia kama una hoja ila kumbe una hila, so unataka ziongezwe ili muendelee kula siyo? Mbona hyo hyo imeunganisha za 70% enzi za jpm na leo inakuwaje mnaleta uhuni? Game ishawakata mnataka kuhamisha magoli
 
27000 siyo gharama halisi, imekaa kisiasa zaidi. Vinginevyo Tanesco itakufa soon
Elewa kuwa wanafanya biashara, na biashara ni mtaji. Wanatakiwa kuwekeza katika usambazaji ndipo wavune pesa kutokana na matumizi ya umeme.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Uamuzi wa Serikali kutoza nguzo na vifaa vingine kwa bei elekezi ya shs27,000 unatekelezwa na hakuna mkwamo.
Ninadhani mradi huu ulifadhiliwa na Bank ya dunia na sisi wenyewe watumiaji wa umeme tunalipa asilimia 3 kwa ajili ya mradi wa REA.
Hili ongezeko la asilimia 3,ambalo linachangiwa na watumiaji wa umeme (Wengi wao wa mijini),kwa kipindi hiki Cha zaidi ya miaka 5, kimeongeza uwezo wa serikali, kufikisha huduma ya umeme vijijini na maeneo ya pembezoni mwa miji.
Miongoni mwa maamuzi bora ya Serikali, ilikuwa kuongeza ushuru wa asilimia 3 kwa watumiaji wa umeme,ili kupeleka huduma hii vijijini.

Ushauri
(1). Baada ya kufikisha huduma huduma ya umeme wa REA, kwenye vijiji vyote, maduhuli yatakayo patikana yaboreshe miundo mbinu ya umeme, ili kuepuka ukatikaji wa umeme.
(2). Maduhuli yatakayo kusanywa,yaelekezwe kwenye uanzishwaji wa vyanzo vingine vya Nishati ya umeme (kama vile Nishati ya makaa ya mawe na uranium).
(3).Baada ya kukamilika Ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JN Dam ) Rufiji,basi Serikali ifanye mapitio ya gharama /bei za umeme, Tariffs, ili kuwapunguzia watumiaji wa umeme majumbani na viwandani gharama (Tariffs za sasa siyo rafiki).
 
Back
Top Bottom