Tunatafuta msaidizi wa masoko na miradi

CATERING

Member
Joined
Sep 29, 2015
Posts
9
Reaction score
4
Habari ndugu,

Tuna kampuni inayojishughulisha na mambo ya catering services. Imesajiliwa na vibali vyote vipo current. Kama heading hapo juu nahitaji mtu wa kunisaidia masoko na usimamizi wa miradi.

- Asaidie kampuni ipate ukumbi wa kuwa tunatoa huduma ya chakula kwa shughuli zote zitakazofanyika ukumbini humo,kwa mkataba maalumu. au

- Asaidie kupata ofisi au shirika litakalohitaji huduma ya chakula kwa mkataba maalumu. au

- Asaidie kutuletea kazi ya kutoa huduma ya chakula kwa siku moja au kwa muda maalumu katika dhifa na matamasha,pia na shughuli mbalimbali sehemu yoyote, kama magraduation, vipaimara, harusi, send off, kitchen party na shughuli zozote zile ziwe ndogo au kubwa.

* Malipo mazuri yatakuwepo kwa kila kazi itakayoletwa,na mkataba utakuwepo kusimamia na kuratibu kazi uliyoileta(kama utapenda kuisimamia).

*Kampuni inafanya kazi zake Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Mbeya na Tabora.

Karibuni sana, kwa maelezo na maelekezo zaidi nipm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…