Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk .Wilbroad Slaa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk .Wilbroad Slaa, amesema kuna haja kwa Rais Jakaya Kikwete, kuwaomba radhi Watanzania, kufutia kitendo cha serikali yake, kushindwa kutimiza ahadi ya kuibua ajira 1,000,000, kama alivyokuwa ameahidi katika kampeni zake za mwaka 2005...
http://www.globalpublisherstz.com/habari_mbalimbali/
Sawa, ajira zinakuwapo lakini wapambe wake wanazinywa kwa kuwapa ndugu zao. Mpaka waishe hao ndio walala hoi wataziona. Tena ukionyesha harufu ya upinzani ndio ufe kwanza ndipo upate, maana kwa Tanzania ya leo mpinzani ni kama shetani na CCM ni mungu (sio Mungu)
Leka
Hayo hayo ya kutotekelezeka kwa ilani za CCM aliyasemaga Mkapa. Sijui kwa nini mpaka leo Watanzania wanaendelea kuwaamini wana CCM na kuwapa kura wakati wanajua ilani zao za uchaguzi ni uongo mtupu.
Wako wengi mitaani mkuu SISIMIZI.Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.
Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.
Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.
tatizo ni elimu......wananchi vijijini hawaelewi kitu wakisha pewa khanga. Mijini cCM wanaiba kura
Tatizo wale wenye upeo wa kuelewa hawapigi kura wanasingizia haitasaidia kitu wanaachia wale wenaodanganyika na khanga na pilau
Mkuu Sisimizi hapo umenena.Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.
Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.
Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.
Mkuu Sisimizi hapo umenena.
To be frank Dr.Slaa is the only guy humo Bungeni ambaye anatoa vitu ambavyo
vinaweza kukufanya utambue ile hadhi na kazi ya Bunge kuwa ni ya kukosoa na kuirekebisha "SIRI-KALI".
Kweli tunahitaji vijana au wazee wa aina hiyo humo Bungeni hao wanaolala wote watoke jamani.
Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.