Emanuel Gabriel
Member
- Feb 7, 2013
- 16
- 5
TUNATAKA, HATUTAKI
Tunataka uwekezaji, hatutaki uporwaji,
Wao wachukue mji, tubaki watazamaji,
Tunakemea ulaji, tunakataa upigaji,
Hofu yetu urithi wetu
Tunataka washiriki, hatutaki wadhibiti,
Bandari waimiliki, tubaki kwenye makuti,
Apange Ahmediki, shuruti ya Mburahati
Hofu yetu nguvu yetu
Hatutaki nia njema, yaboreshwe mashariti,
Tumechoshwa na hujuma, wengi wenu wasaliti,
Leo tuseme salama, kesho tushikwe mashati,
Hofu yetu umoja wetu
Tunataka ufanisi, umateka hatutaki,
Mwuonao adanasi, punde hawaambiliki,
Sasa twaamua sisi, kisha hatutashiriki,
Hofu yetu uhuru wetu
Tuikubali lawama, hasara hatuitaki,
Bora tukose kheshma, ila tuipate haki,
Heri mwisho mwema, kuliko uharakiki,
Hofu yetu nchi yetu
Emanuel Gabriel Someke
emanuelsomeke@gmail.com
29/06/2023
Tunataka uwekezaji, hatutaki uporwaji,
Wao wachukue mji, tubaki watazamaji,
Tunakemea ulaji, tunakataa upigaji,
Hofu yetu urithi wetu
Tunataka washiriki, hatutaki wadhibiti,
Bandari waimiliki, tubaki kwenye makuti,
Apange Ahmediki, shuruti ya Mburahati
Hofu yetu nguvu yetu
Hatutaki nia njema, yaboreshwe mashariti,
Tumechoshwa na hujuma, wengi wenu wasaliti,
Leo tuseme salama, kesho tushikwe mashati,
Hofu yetu umoja wetu
Tunataka ufanisi, umateka hatutaki,
Mwuonao adanasi, punde hawaambiliki,
Sasa twaamua sisi, kisha hatutashiriki,
Hofu yetu uhuru wetu
Tuikubali lawama, hasara hatuitaki,
Bora tukose kheshma, ila tuipate haki,
Heri mwisho mwema, kuliko uharakiki,
Hofu yetu nchi yetu
Emanuel Gabriel Someke
emanuelsomeke@gmail.com
29/06/2023