Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
Wadau salaam,
Kwa kawaida uamuzi wa kujenga taifa lenye watu wa aina fulani u mikononi mwa wananchi wenyewe na wananchi ni mimi na wewe. Kwa hiyo mchango wako wewe na mwingine na mwingine (uwe hasi au chanya) unachangia kujenga jamii ya aina fulani na hatimae taifa la aina fulani.
Kwa kawaida jambo lolote liwe jema au baya, huanza kama fikra, hutolewa kama hoja, huchambuliwa na kisha hutekelezwa ili kuleta matokeo ya aina fulani.Kitendo cha mtu kuamua kutojilazimisha kufikiri vya kutosha, humfanya asiwe na mawazo yenye mtiririko mzuri ndani ya kichwa chake , kitu kinachomfanya anapoongea ashindwe kutoa hoja na ajikute akipiga kelele tu ambazo kimsingi hazina athari yeyote ya maana katika jamii.
Kasi ya wengi wetu kupiga kelele badala ya kujibu hoja pale tunapoulizwa ni kwanini vyama vyetu havijafanya jambo fulani ambalo vilitakiwa vilifanye, au kwa nini vimefanya jambo fulani kinyume na ilivyotakiwa kufanya au kwani nini vimefanya jambo ambalo halikutakiwa kufanywa kabisa, imeongezeka sana!.
Inavyoonekana tatizo hili kwa kiwango kikubwa huchangiwa na wengi wetu kuamua kutochambua mambo tunayoyaona, kuyasikia au kuyasoma amma kwa makusudi, kwa kusikiliza ya kuambiwa tu badala ya kuchanganya na zetu, au kwa kukosa uwezo (ni jambo la mjadala), au kwa uzembe.Ni kitu cha kawaida sana siku hizi chama, mwanachama au kiongozi anapoulizwa swali, badala ya kujibu swali huibuka na kuanza kupiga kelele.Mara utasikia mnafiki wewe! msaliti wewe,! mburura, kachukue hela yako! wewe mwanamke au mwanaume n.k.
Kwa kuwa taifa hujengwa na wewe na mimi, na kwa kuwa mazoea hujenga tabia; basi ni hiari yetu kuchagua kujenga Taifa la wapiga kelele! kwa kujizoeza kupiga kelele mbele ya hoja au taifa la wajenga hoja kwa kujizoeza kukabiliana na hoja zinapojitokeza.
Wanasema dunia ni yetu chaguo ni letu na akili kumkichwa.

"Let Us Urgue not Shouting, for Our love to The Nation, today and Tomorrow!"