Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Singida Black Stars SC dhamira yetu ni kushiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup 2024 endapo kila kitu kitaenda kama tulivyopanga.
Tumeshawasiliana na waandaaji tunasubiri watupe uthibitisho rasmi na mpaka sasa hatuoni kikwazo chochote kutoka kwao.
Tayari tumeshatoa taarifa kwa wachezaji wote wanatakiwa kuripoti jijini Dar es Salaam Julai Mosi 2024 kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo.
Tumeamua kuyatumia mashindano ya CECAFA Kagame Cup 2024 kama sehemu ya programu ya Benchi la Ufundi kwa ajili ya maandalizi kuelekea msimu wa mashindano 2024/2025.