Profesa
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 905
- 624
Kama ni ya Kisiasa je siasa gani tunataka? Na je siasa hiyo ndiyo itakayoweza kubadili hali duni ya wengi na kuleta hayo yanayodaiwa kuwa ni maisha bora? Na hayo masha bora ni yapi? Ni ya kisasa au ya asili? Ya kisaa ni yapi na ya asisli ni yapi? Je ya kisasa yna faida gani ukilinganisha na ya asili? Na ya asili yanafaida gani kulinganisha na ya kisasa?
Kama ni uchumi, je nchi hii ina utajiri wowote wa rasilimali asili au za kutengenezwa zinazoweza kutumika kukuza uchumi? Kamahatuna tufanyeje? kama tunazo Je Uchumi tulionao sasa unatuletea matumaini yeyote? Hali ya matabaka ya kuchumi yakoje? Kuna usawa katika kupata huduma za afya? Elimu? Maji? Chakula? Kama ni ndiyo au hapana, kwa nini?
Kama ni utamaduni, tatizo ni nini? Je kuna utamaduni tunaoutaka ambao tunaamini unaweza kutunufaisha kwa hali yoyote ile? Kwanini tunahitaji huo na tusiukuze utamaduni tulionao sasa? Mfano Nyumba za Tembe ni utamaduni au ni umasikini? Ufugaji huria ni utamaduni au ni umasikini/uharibifu wa mazingira (ssina uhakika kama mbogo na swala na punda milia wanalaumiwa kwa hili pia maana tunataka waongezeke kwa wingi na kupunguza hawa wakwetu wa asili, tuongeze wa kigeni na kufuga kwa "kisiasa")? Je Kuvaa Rubega (Uhuru wa kuvaa na kuvua na kumudu hali zote za hewa) ni utamaduni au ni kupitwa na wakati? Ngoma zetu za asili zina kasoro gani? Ngoma za wenzetu zenye technolojia ya komputa zina kasoro gani? Ni kipi kinadumishwa kwa sasa? Kwanini?
Je kwa sasasa nhi yetu iko huru? Uhuru wa kisasa? Kiuchumi? Kiutamaduni? Au tuko utumwani kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni? Nani ndivyo nani ni mkoloni? Kama sivyo, nini tunachojivunia kujitawala?