Pre GE2025 Tunataka uchunguzi haraka kutekwa kwa raia wawili Kigoma na Dar es salaam na uzembe wa jeshi la polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko makubwa na kulaani vikali kutekwa kwa wananchi wawili Dar es Salaam na Kigoma katika mazingira yanayotia shaka, huku Jeshi la Polisi likionyesha uzembe wa hali ya juu katika kushughulikia matukio haya. Matukio haya yanatoa picha ya wazi kwamba ama Jeshi la Polisi linahusika moja kwa moja au linashindwa kabisa kutimiza wajibu wake wa kulinda raia na mali zao.

Tumepokea taarifa kuwa tarehe 28 Februari 2025, Method Damian Kumdyamka (45) alitekwa nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam na watu wanane waliokuwa na silaha na gari aina ya Prado. Licha ya familia yake kutoa taarifa na kutembelea vituo vyote vya Polisi jijini Dar es Salaam, hajapatikana kwa siku 3 sasa na hakuna hatua yoyote madhubuti iliyochukuliwa na Jeshi la Polisi kumtafuta au kuchunguza.
WhatsApp Image 2025-03-02 at 15.14.30_3eed1f24.jpg

Dahlia Majid Hassan
Tukio jingine, Februari 10, 2025, Manase Daniel (40), maarufu kama 'White', alitekwa mchana kweupe akiwa kwenye duka lake la vipuri maeneo ya Senga, Kigoma Ujiji, alifungwa pingu na watu waliokuwa na silaha na kuondoka naye. Ndugu zake waliripoti kituo cha Polisi, kwa Mkuu wa Wilaya na baadaye RTO, lakini hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusu alipo. Manase ni tumaini la pekee kwa familia yake, anasubiriwa na watoto wake sita, mke na baba yake ambaye alikuwa akisubiria kupelekwa Hospitali kufanyiwa upasuaji.

Soma Pia: Method Damian Kumdyanko adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha

Ukimya wa Jeshi la Polisi kuhusu matukio ya utekaji yanatia shaka sana na kujaza hofu kuhusu usalama. Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa watekaji walitumia silaha, pingu na mbinu za kiusalama, mambo yanayoashiria uwezekano wa kuwa watekaji ni maafisa wa usalama (Polisi). Vinginevyo, ni dhahiri kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kutekeleza majukumu yake ya msingi, likiruhusu matukio ya utekaji kuendelea kushamiri bila hofu ya kuwajibishwa.
ACT Wazalendo inaitaka serikali kuchukua hatua zifuatazo haraka sana, kunusuru maisha ya wananchi hawa wasio na hatia:

i. Kulitaka Jedhi la Polisi kutoka hadharani kueleza walipo wananchi hawa na hatua zozote za kiuchunguzi zilizochukuliwa.

ii. Tunaendelea kuitaka Serikali kufanya uchunguzi huru na wa haraka wa matukio haya na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

iii. Ni wakati sasa, Serikali kuhakikisha raia wote wanakuwa salama na kusitisha mara moja mwenendo huu wa kutekwa kwa watu bila hatua za kisheria kuchukuliwa.

ACT Wazalendo itaendelea kushinikiza uwajibikaji na kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa wote. Jeshi la Polisi linapaswa kutambua kuwa Watanzania hawatakubali kuishi kwa hofu huku dola ikiendelea kushindwa kulinda maisha yao.

Imetolewa na:
Ndg. Dahlia Majid Hassan
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani – ACT Wazalendo
Machi 2, 2025

Mmh
 
Ase.

Ndio kuelekea Uchaguzi mkuu 2025.

Hao waliotekwa nao pia ni Wanasiasa kama wetu wa CHADEMA?
 
Ndg. @hassandahlia7
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani – ACT Wazalendo
Machi 2, 2025
 
Attachments

  • FB_IMG_17409226145458414.jpg
    FB_IMG_17409226145458414.jpg
    329.9 KB · Views: 2
Haya mambo sio sawa na Kwa kweli hayafai kabisa na sijui mamlaka zinajiskiaje Kwa kukaa kimya Kwa mambo kama haya yanayoumiza wahusika na familia zao.

Mamlaka husika nishughulikie jambo hili
 
Mmmmmhhh,No reform No election,tuungane wote bila kujali bila kuja nani,wapi,chama Wala Nini,tupinge uhai wetu kupote za hivi,???? Uhai ni zawadi ya mungu hakuna mwenye kuchezea . Ukiangalia unaogopa no kila siku kila mahali utekaji sijui .viongozi wa dini watoke na kukemea Hali hii mbaya kwa nchi yetu kweli kisiwa Cha amani kweli???? .Askofu kemea Pepo la utekaji.,nabii kemea Pepo ,Wacheni kuziba masikio dini zote acheni unafiki wa kemeeni uaji,huu
 
Back
Top Bottom