Tunataka Ujasusi wa kiuchumi uimarishwe Tanzania

Tunataka Ujasusi wa kiuchumi uimarishwe Tanzania

Burkinabe

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
2,354
Reaction score
4,024
Asalam Aleykum,
Niliwahi kusema hapa Jukwaani kwamba nchi yetu ni " A sleeping giant".

Hii ni kutokana na kwamba licha ya kuwa na raslimali za kila aina lakini bado Watanzania wengi tunaishi chini ya dola moja!

Hii kwa kweli inavunja sana moyo.

Binafsi nilishasema na leo narudia tena kwamba kama nchi tunayo kila sababu ya kujivunia intelijensia yetu katika masuala ya Ulinzi na Usalama. Nathubutu kusema kwa Afrika tunaongoza katika masula ya Kiulinzi na usalama kutokana na ubora wa vyombo vyetu hivyo.

Lakini kwa bahati mbaya sana, linapokuja suala la intelijensia ya kiuchumi, tuko vibaya sana na nadhani kwa Afrika tunaweza kuwa wa mwisho kabisa kulingana na uwiano wa raslimali tulizo nazo na kile tulicho nacho kama Taifa.

Hivyo, kwa sababu idara yetu ya TISS ambayo imepata Mkurugenzi Mpya na anayeonekana kuwa na CV nzuri sana ikiwamo katika masuala ya usimamizi wa mashirika ya umma (Mfano NSSSF), binafsi ninafarijika kwamba sasa Intelijensia na ujasusi wetu katika masuala ya kiuchumi, unakwenda kuimarika.

Kwa wale tuliofuatilia, Balozi Siwa, kwa usimamizi mzuri ameweza kufanikisha shirika kujiwekea ukwasi wa zaidi ya trilioni 7 ambazo zinaweza kuwalipa wastaafu wote kwa zaidi ya miaka 40!

Tunataka ujasusi na intelijensia ambayo iliweza kuinua uchumi wa shirika moja tu la NSSSF hadi kufikia kiasi hicho ambacho ni karibia 25% ya bajeti yetu ya mwaka mzima, ikatumike kuimarisha uchumi wetu kwa ujumla.

Hakuna Taifa linaloweza kuendelea pasipo kuyanyonya mataifa mengine! Huu ndio ukweli mchungu. Sisi kama Taifa tumezungukwa na mataifa tajiri sana ambayo kama tungelikuwa na Intelijensia inayojielewa, basi Tanzania ingekuwa mbali sana!

Lakini badala yake, tumekuwa tunatumia raslimali zetu wenyewe kuyasaidia mataifa hayo kwa gharama ya umaskini wetu.

Na kwa bahati mbaya sana, hata yale mataifa tuliyosaidia kufika hapo yalipofika, mengi yao hayana shukrani kwa nchi yetu. Mfano, kuna kipindi raia wetu wanaojitafuta huko Msumbiji na Afrika Kusini walipata misuko-suko ambayo wengine ilipelekea kupoteza maisha yao na wengine kurejezwa nchini wakiwa hawana chochote!

Sasa kwa sababu tumeshajifunza kutokana na makosa, kwa nini intelijensia yetu sasa na wao wasifanye kama ambavyo matafa yaliyoendelea yalifanya na yanazidi kufanya kwa maana ya kuchukua kwa akili mali katika mataifa tunayoyasaidia katika kulinda amani n.k.

Naomba nihitimishe kwa kumwomba Mkurugenzi wetu mpya wa idara kwamba, tuhamishia nguvu kubwa sana katika masuala ya intelijensia na ujasusi wa kiuchumi.

Hili lianzie katika kuhakikisha masuala ya kuingia mikataba kati ya viongozi wetu na mataifa mengine linaangaliwa kwa umakini wa hali ya juu, maana hata hivyo tunajua idara yetu imesheheni wataalam ambao ni cream.

Tunataka kuwa Taifa kubwa kiuchumi barani Afrika na duniani kwa ujumla kabla au ifikapo 2050. Naomba hili ndo likawe lengo kubwa la idara na nchi kwa ujumla. Tumechoka kuishi maisha ya kimaskini kwenye nchi TAJIRI.
 
kwa mfumo huu wa utawala na kwa Katiba yetu hii hili linakuwa ni ndoto, ujasusi wa kiuchumi ni kitengo nyeti ndani ya TISS, kwa TISS hii yetu ndugu unategemea nini hapo? wacha tuendelee kulala kwanza.
 
kwa mfumo huu wa utawala na kwa Katiba yetu hii hili linakuwa ni ndoto, ujasuzi wa kiuchumi ni kitengo nyeti ndani ya TISS, kwa TISS hii yetu ndugu unategemea nini hapo? wacha tuendelee kulala kwanza.
Nadhani tumeanza kuamka.
Balozi atakuja ku-apply kile alichojifunza huko alikokuwa Balozi. Maana licha ya kuwa nchi isiyo na raslimali, lakini uchumi wake unakua kwa kasi sana. Hadi tunavyoongea, wenzetu wanaishi maisha ya First World Country!
Tunautaka ujasusi wa hivyo, utumike na hapa kwetu pia.
 
Back
Top Bottom