BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
Sisi watanzania, tunalitaka lile kundi la akina mama wa CCM (UWT) lione haja ya kukemea majizi na wachepushaji wa fedha za wananchi.
Kila mahala ukipita lazima ukutane na hadithi ya majambazi kukwapua fedha za miradi na za ofisi za umma. Majizi yametamalaki yanakomba na kufakamia.
Tunamtaka Mary Chatanda ainuke akemee vikali ujambazi wa fedha za umma, akemee wazembe na wavivu, na akemee ujanja ujanja kwenye rasilimali za nchi.
Akina mama wanateseka hawana maji wala hospitali kwa sababu ya majizi na wavivu. Huduma hazipatikani kwa sababu ya fedha kutapanywa na kukwapuliwa na magoigoi wasioweza kazi.
Tunamtaka Mary Chatanda ainuke kwa madoido na mbwembwe awafokee hawa majambazi na majizi sugu ili taifa lipone.