Tunatazanma soka au mashindano ya ulimbwende? The game is not the same anymore

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
.
Miaka ya 1959-74 Jijini Liverpool, kulikuwa na Kocha Billy Shankly YES alikuwa 'Mwendawazimu' aliyelipenda soka na kulihusudu, huyo alikuwa mwanaume sana.
.
Bill aliwahi kuwaambia wachezaji wa Liverpool, tatizo mnahisi mchezo wa soka ni UHAI na KIFO ila soka ni zaidi ya hivyo[emoji2] ukivunja mguu jikaze sio mali yako ni mali ya Liverpool[emoji119][emoji119] huyo ndie Shankly bwana.
.
Wakati dunia ya leo tunawajadili Instagram players wakina Jesse Lingard na Paul Pogba, kuna wanangu kutoka Ghetto wanawakumbuka wakina Roberto Carlos na vipara vyao, Marc Vivien Foe (Marehemu) na Kipilipili chake, Ghetto linawakumbuka Jose Rene Higueita kutokea Bogota Colombia, alipewa jina la 'The Madman".
.
Wakati huo tunawajadili mabishoo wakina Theo Walcott, bado masela wanakumbuka fainali ya World Cup 2006, Zinadine Zidane na maamuzi yake, hana muda na refa akasogea kwa Materrazi akaweka ndoo ya maana akala red yake akasepa nje[emoji119] watu walikuwa wanaume haswa.
.
Wakati huo Academy ya Manchester United watoto wanachipukia wale wa Class of 92 akina Ryan Giggs, walikuwa wanakula makonzi na Paul Ince, aliwaambia nifateni mimi, mimi ndie kiranja hapa United.
.
Wakati dunia mnajadili issue za unene wa Eden Hazard, ila wahafidhina wenyewe wale Mancunians wanakumbuka Eric Cantona aliwageukia viungo wa United, aliwaambia kazi yenu ni kukaba kisha nipeni mpira niuchezee mimi fundi[emoji2]
.
Wakati huko Italia kwenye kumalizia soka la wanaume Antonio Conte aliwahi kuvua nguo mbele ya wachezaji akawaambia tizameni mimi ni mwanaume, msiniletee ulaini wenu [emoji2]
.
Anyway tuendelee kutafakari hawa mabeki wenu wa buti moja tu chini, ila wakumbusheni mwanaume mmoja wa Serbia Nemanja Vidic, wapeni story za Jap Staam kisha waambie kuliwahi kuwa na Tony Adams pale Highbury ile Gunners ya kiungo Patric Viera.
.
Professa wa Ghetto

 
Kila zama na mambo yake. Soka sio mieleka, kama kizazi cha zamani kilifurahia ubabe wa wachezaji wacha na sisi tufurahie burudani za wachezaji wa kizazi chetu kuanzia instagram mpaka uwanjani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…