Tunaumia sana mashabiki wa Simba,mnayoyafanya viongozi wa Simba sio mazuri

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Kwa Mara nyingine club pendwa ya Simba inaangukia pua baada ya kukosa kutwaa kombe la Cecafa

Tunaumia sana hasa mambo ambayo viongozi wa Simba mnayafanya,kama hampo tayari kushiriki haya mashindano bora mkae kimya msishiriki kama Yanga

Mnasajili kwa mbwembwe halafu mnaangukia pua,

Mnarudia yale yale makosa ya kutowapeleka kikosi fully kilichosajiliwa kucheza Sport Pesa,mkapeleka kikosi cha ajabu ,tukaangukia pua

Tena Cecafa mnarudia yale yale,mashabiki tunaumia na upumbavu mnaoufanya lakini hamjui tu tunavyoumia,bora msiwe mnashiriki hayo mashindano
 
Pole sana Mkuu! Ndio hivyo tena Azam wamefanya yao!!!
 
Hawa simba nao hovyo sana, manara alituambia mmeunda vikosi vitatu vya nguvu, mkishinda mnajitapa, mkifungwa mnadanganya mlichezesha kikosi B, yaan kwa akili ya kawaida tu, wawa, salamba, kagere ni wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya kikosi B
 
Washabiki wa Simba ni wajinga sana timu ya Simba imezidiwa uwezo uwanjani...imefungwa na Azam , sasa viongozi wafanyeje,?....Okwi.Boko wlikuwepo siku Simba inafungwa na Kagera Sugar na hawakufanya chochote...Hata kwenye Kagame wangekuwepo bado Simba wangefungwa tu hata kwenye fainali wasinhefika...hakuna timu isiyofungwa
 
Bora wachezaji wote wawepo,kuliko kuweka kikosi B
 
Vibabu vimeshndwa kuisaidia timu, Wawa ni zaidi ya uchochoro
 
Viongozi wafanyeje hata wangeweka kikosi A sijui C matokeo yangekuwa hayo huo ndo uwezo wa simba kwa vikosi vyake anavyojitambia kuwa viko makini, waache viongozi wafanye majukumu yao
 
Napendekeza kipindi kama hiki ndio wachezaji wapewe likizo.
Wakati mashindano yote yamemalizika.
Yaani
VPL
FA
Sportpesa
Kagame
Chonde chonde Viongozi wa Simba SC, muda huu ndio unafaa kuwapa wachezaji wetu Likizo.
Maana hakuna tena mashindano yoyote.
Mfano tungeshinda Sportpesa tungepata nafasi ya kuwa onesha wacheji wetu soko la Wingereza. Kwenye mechi na Evartoni.
Chonde chonde viongozi msiwapumzishe wachezaji mashuhuri wakati wa mashindano yanaendelea.
Mda mzuri ni sasa ambapo mashindano yote yameisha
Chonde Chonde
 
Raisi alishasema kwa mchezo huo mnaoonyesha hamuwezi kuleta kombe

Ni lazima mtobolewe tundu
 
Kilichonikera ni kusajili kwa mihemko bila kuangalia nafasi,

Leo hii tumesajili Salamba, kaheza,mohamed Rashid, kagere wote hawa ni strikers.

Wakati timu haina mawinga kabisa zaidi ya kichuya na dogo Rashid juma tuliempandisha. Nilitegemea tununue Strikers wawili na mawinga wawili.

Huku tukiangaza angaza nafasi zingine zinapwaya vipi matokeo yake tumetupa pesa yote kwa strikers. Hiii nilazima itafanya wachezaji kuchezeshewa namba ambazo hawana mazoea nazo.
 
Daaaaaah we jamaa vp.
Sidhani kama unaelewa habri za future plan. Toka mwanzo walisema kua hatutatumia kikosi kizima tutatumia hiki kingine kwa ajili ya plan ya badae.
Mi naona wamefanya vyema mana wanajua nani wamwache nani abaki na kocha atakua anawaelewa wachezaji wake waliosajiliwa.
Hivi wasingewatumia hao nani angejua uwezo wa Rashid Juma, nani angemwamini Pascal Wawa.
Au mnataka kama mtu mmoja anataka kujenga viwanda kwa miaka mitano wakti hata msingi haukuandaliwa. Sasa sijui hivyo viwanda vitakuaje.
Tuache kulalamika mi naona Lengo la viongozi wa simba limetimia.
Ila pia simba mnaupugufu wa kiungo mchezeshaji demla na Mzamiru hawawezi kabsa kuunganisha na washambuliaji. Kama hawataliona hilo patakua na shida sana kupata matokeo. Timu inakosa kabsa muunganiko na washambuliaje.
Afu kingine sijui kocha anamwangaliaje Gyn mana ni mzr kupeleka mashambulizi lakini si mzr kwenye ukabaji, angekua anamchezesha tu ka winga mshambuliaji badala ya anavyomtumia ka beki, labda kwa mfumo wa 3:5:2
 
Everton wanavifunga vitimu ushenzi 22..mngeweza kubeba hii aibu ya karne
 
Mezaa majiihayooo yauhaiii dogooo tuliza mzukaa
 
Taabu sana watapata mikia FC.
 
jiwe aliwaambia kwa mpira ule mliocheza na kagera sukari pale taifa kuchukua kombe msahau na mtapata tabu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…