Plot4Sale Tunauza viwanja katika maeneo mbalimbali

Naomba kuuliza mfano nimeinunua hii nyumba na kiwanja chake hapo hapo nikaenda bank kukopa kwa dhamana ya hiyo myumba unaweza niambia nitavuta mkwanja bei gani alafu rudi hapo juu usome hiyo figur ulioandika. Kweli kigamboni mbutu 35m sasa kibugumo mji mwema kibada shangwe utauza kwa bei gani mkuu. Au mimi ndio sijui thamani ya viwanja na jengo kama hilo.
 
Hata mm nimeshangaa kwakweli. Akikujibu naomba unitagi please
 
Jibu maswali haya kwanza
Gharama za kiwanja ukubwa huo ? _
Gharama za ujenzi wa nyumba hadi ilipofikia ?_
Gharama za upimaji wa kiwanja ?_
Tufanye kiwanja ni 10 m kujenga hilo pagara tufanye 10m haya kupima tufanye 5m haya hebu na ww sema gharama halisi za hilo eneo na kujenga kwa huko mbutu mchanga wa bure kabisa tofali umezichukua mbali sana ni pale dege haya tupe mchanganuo wako dalali. Na ukumbukr hapo nimesema tufanye ila bado nikiamua kumuweka fundi nikamlipa kwa tofali bado hiyo nyumba haifiki 10m kwa ujenzi wa mbutu na maeneo kuanzia kibugumo kwenda mbele. Na kuna kitu kinaitwa value for money je hapo kipo kweli au unataja 35 as if hakuna opption nyingine
 
Nyumba ya vyumba3 isivuke 10M?
 
Omba Moderator wabadilishe heading isomeke "Pagale linauzwa Mbutu- Kigamboni"
 
Bora umwambie wewe, hapo ilipofikia zaidi 15+M imekata..
Kwa mahesabu yapi bhana yaani kupanga tofali 15m alooo unachekesha ww na kama umetoa hiyo labda ulikua unajengea mchanga wa mwezini
 
Jibu maswali haya kwanza
Gharama za kiwanja ukubwa huo ? _
Gharama za ujenzi wa nyumba hadi ilipofikia ?_
Gharama za upimaji wa kiwanja ?_
Hicho kiwanja kwa huko hakizidi 8M
Hiyo nyumba mpaka hapo kwenye kozi ya renta haizidi 15M na kama imezidi jua umepigwa.
Jumla ni 23,hiyo nyumba ulitakiwa uizwe 25-27M na sio zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…