Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Mahusiano ya miaka na nyakati hizi yamegubikwa na changamoto nyingi sana kutokana na kusokenana na mfumo rasmi wa kuratibu na kusimamia ustawi wake katika hatua za awali na kadiri muda unavyozidi kwenda.
Hapa nitaangazia dhana potofu dhidi ya uhalisia wa Maisha katika jamii eneo la mahusiano kama ifuatavyo;
1. Vijana na mabinti wa sasa wanadhania kuishi pamoja katika mahusiano halali na rasmi ya ndoa katika umri mdogo ni ubatili dhidi ya Maisha wanayoyatarajia siku za mbeleni. Ukweli ni kwamba hakuna ubatili wowotw kuanza maisha rasmi kwapamoja katika umri sahihi baada ya kupevuka na kuvunja ungo na kupata mafunzo sahihi ya namna ya kuishi kama mume na mke.
2. Vijana na mabinti wa kisasa wanaamini kuwa mwanaume na mwanamke wahusika nakuwajibika na majukumu sawa sawa ndani ya mahusiano rasmi. Ukweli ni hakuna majukumu sawa sawa ndani ya mahusiano bali majukumu huzingatia uwiano sawa unaotazama muda,afya,kipato,uwezo,maarifa,jitihada,bidi, na uelewa wa muhusika.
3. Vijana wanaamini wanaume huingia katika ndoa kwa lengo kuu la kufanya mapenzi kisha vinginevyo vinafuata. Ni kweli kufanya mapenzi ni sehemu ya shughuli za ndoani ila sio shughuli ya mara kwa mara au pekee.
Kiwango cha kufanya mapenzi hupungua kadiri umri ukienda na majukumu kuongezeka lakini pia akili hutumika zaidi katika kumridhisha mwenza kuliko nguvu za mwili. **** shughuli na majukumu mengine ya tofauti yatayohitaji muda,akili,pesa, na jitihada za watu wawili Zaidi kuliko unavyodhania.
4. Vijana na mabinti hutazamia upendo kama tendo la kufanyiwa vitu na mtu mwingine zaidi ndipo wahisi ni upendo halisi. Ukweli ni kuwa,utakapofikia umri wa ukomaavu utakuja kugundua kuwa upendo ni kujitoa zaidi kwa mwingine bila hofu ya kuhisi unatumika. Yule umejitoa sana kwake na akakudharau au kukupuuza akifika umri wa ukomaavu kuna asilimia kubwa sana atatamani siku zirudi nyuma ili akutunze asikupoteze maana atakuwa ameanza kuelewa maana ya neno upendo.
5. Vijana na mabinti huamini unaweza kwenda kuwa mume au mke wa mtu direct kutokea hatua ya uvulana na usichana bila kupitia mafunzo kamili ya kuwa mwanaume au mwanamke.
Ukweli ni huwezi kuja kuwa mume au mke wa mt una baba au mama wa familia bila kupitia mafunzo sahihi na kamili ya uanaume na uanaumke.
6.Vijana na mabinti hudhani kuwa pesa ndio msingi wa mahusiano ya ndoa na ili yawepo lazima pesa ziwepo. Ukweli ni kuwa pesa ni muhimu ila sio msingi wa kuanzisha mahusiano rasmi ya ndoa.
Upendo ndio msingi wa kuanzisha mahusiano sababu mnaweza kukosa pesa ila upendo ukawafanya kupanga maisha ya mbele zaidi mkizitafuta pesa ila huwezi kuutafuta upendo ukiwa na pesa na ndio maana kuna wanajamii wenye kipato cha kawaida na wanafamilia zenye ustawi mzuri ila kuna matajiri wenye pesa nyingi ila baba,mama, na watoto hawapo pamoja na wana mifarakano isiyo na mwisho.
7. Mabinti hudhania usalama wao na kuwa na guarantee ya future nzuri ni kujiwekeza na kuwa na mali binafsi zenye majina yao ili kujilinda na manyanyaso ya wanaume siku za baadae ikiwamo kufukuzwa na kutupwa mtaani bila pakwenda.
Ni kweli mali huumpa mwanamke sauti juu ya mali ila si juu ya mahusiano. Kuna uwezekano mkubwa wa kuwa mhanga wa ndoa za manyanyaso kutokana na kuvutia wanaume wasioweza kujitegemea na wategemezi kwa mwanamke na wenye uwezo mkubwa sana wa kurubuni akili ya mwanamke na kukuharibia maisha. Mali sio ulinzi dhidi ya manyanyaso kwenye ndoa bali elimu juu ya mahusiano sahihi na majukumu yako kama mwanamke au mke.
8. Vijana hudhania kulala na wanawake wengi haina madhara siku za baadae ndani ya mahusiano yao na inawapa ufundi. Ukweli ni kwamba utaweza kupata mwanamke wa kutulia nae ila ni vigumu sana kukubali kuachia mwanamke ambaye anafanya vizuri kitandani ila hafai kuwa mke,kuna yule anaekiss na kujua kuflirt vizuri,kuna yule anaye jua kukujali sana ila, kuna yule ambaye yupo vema sana kiuchumi,haw ana wengine wenye sifa zinazokufanya usitake kuachia mwanaume mwingine awachukue ndio watakao kunyima amani na utulivu pale utakapotaka kusettle na mke. Ni ngumu sana kwa kijana mla mademu wengikusettle kama ilivyongumu kwa teja kuacha madawa.
9. Mabinti hudhani katika haya maisha accomplishment kubwa na kuwa na fedha na mali na ndio maana huhangaika karibia robo tatu ya usichana wao kutafuta pesa kwa jasho na dam una ikibidi hata kurisk maisha yao. Ukweli ni kuwa fedha na mali hutumika kukuvusha kutoka usichana hadi utu uzima kwa utulivu ili kukufikisha kwenye mazingira salama ya kutengeneza familia yako. Hakuna accomplishment kubwa kwa mwanamke kuishinda familia yake ya baba,mama na watoto.
Ndio maana hata wadangaji kama wakina Hamisa Mobeto pamoja na kupata maokoto kupitia udangaji bado watafosi waolewe ili kuwaambia wanajamii wameweza kuaccomplish mission ya kuwa na familia kama mwanamke anavyotakiwa kuwa. Asikudanganye mtu mwanamke bila familia ni nyani wa zoo,hawezi kuwa na furaha kama nyani wa porini.
10. Vijana na mabinti hudhania wana time frame na timeline sawa. Ukweli ni kwamba mabinti muda wao wa kujenga future yao ni mfupi na muda wa kuifurahia au kuteseka nayo ni mrefu wakati vijana muda wa kuijenga future yao ni mrefu ila muda wa kuienjoy ni mdogo sana. Binti ana allowance ya muda kuanzia miaka 16 hadi 26 (10 years grace period) ya kujenga future akibugi huko mbele kuna vitu hawezi kuvibadili hata kwa miujiza. Kijana ana kuanzia miaka 14 hadi 75 (61 years grace period) kujenga maisha factor muhimu ikiwa uwezo wake wa kujifunza na kujiboresha.