Gharama ya mafuta ya magari ni ghali sana kwa hivi sasa na nimesikia kuwa DIT wana utaalamu wa kukarabati magari na kuyawekea gesi asilimia ili itumike badala ya mafuta ya diezeli na petroli. Nimesikia utaratibu huu tayari umeanza kule Dar es Salaam na hivyo na sisi wananchi wa Mwanza tunaomba muje mfungue tawi lenu huku na sisi tupate kubadilisha magari yetu kutoka matumizi ya mafuta ya diezeli/petroli na kutumia gesi. Karibuni sana mtapata wateja wengi sana.