Jana Mhe. Mpina alifukuzwa Bungeni na kutakiwa kutohudhuria mikutano 15 ya Bunge. Tulisoma HOJA zake lakini uamuzi ukafikiwa kuwa afukuzwe. Kwa kuwa nchi hii inaongozwa kwa kufuata UTAWALA BORA, pia inafuata sheria, kanuni na taratibu hivyo ninaomba Wanasheria nguli watufafanulie hoja za Mpina kifungu kwa kifungu kufuatana na sheria ya sukari ili tujue ukweli nani ana kosa kati ya Mhe. Mpina na Bashe.