Tunawapenda na kuwakubali kwasababu hutuwajuwi!

Tunawapenda na kuwakubali kwasababu hutuwajuwi!

Ben-adam

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2023
Posts
1,043
Reaction score
2,309
Tunawapenda na kuwakubali kwasababu hutuwajuwi!

Kuna vitu vingi vinavyoweza kukufanya umpende mtu au vitu vya mtu fulani ambaye wala humjuwi na haujawahi kuonana naye, uandishi wake kama wengine wanavyosema, jokes, uchangiaji wa hoja na mengine mengi tu


Wakati unaendelea kusoma alichoandika Blandina, unahisi furaha sana wakati huo unamCreat blandina kwenye ubongo wako (tofauti na uhalisia) unaweza kumwona mrembo sana, mrefu, maji ya kunde nk (unamtengeneza vile unavyotaka/unavyodhani) kulingana na vile utakavyomuona unajikuta uko katika hali ya Kummiss😅


Siku ukibahatika kukutana naye utastaajabu! sio kwamba ni mbaya, isipokuwa Blandina unaemjua wewe hayuko hivyo 👩‍🦲itakuchukua muda tena kufanya modifications


Ukitaka kusafiri kwenda Bukoba, japo hupajuwi; unaweza kuwa na furaha kutokana na sifa kadhaa ambazo umewahi kusikia kuhusu Bukoba; hivyo utajitengenezea bukoba yako akilini mwako siku ukifika bukoba yenyewe ...


Unaweza kuwa na wafuasi wengi sana kwenye majukwaa kama haya lakini ukienda kutoa hotuba usisikilizwe (ukapuuzwa) hata kama unapoint za maana, lakini kitu hichohicho ukikiweka kwenye maandishi (vitabu nk) utapata watu wengi sana


Watu wengi walimpuuza Yesu kwasababu walikuwa wakimuona hata wewe huenda huenda ungekuwa miongoni mwao!
Hawa mitume na manabii tunawakubali kwasababu tunawasoma kwenye vitabu tu (hatuwajui)
Ukimsoma mtume Paulo unamuona kama Giant fulani hivi enh💪🤣

Kila mtu anasema hakuna Nabii kwa sasa!
Je unaaminije Zamani kama walikuwepo? kwani kizazi hiki hakuna wanaotabiri??
 
Hapo umenigusa mkuu Mimi ndo huwa tabia yangu,kama naenda mkoa mpya ambao sijawahi kufika
huwa nautengeneza ndani ya kichwa changu kwanza
Ukienda ukakuta pako chini ya viwango ulivyokuwa unafikiria unaanza kuponda🤣
 
Back
Top Bottom