Hata mi huwa najiuliza hivi ni kwa nn dunia inahangaika sana miaka hii kuwaweka wanawake ktk nafasi zisizo zao!?
Kila kilichoumbwa ktk dunia kina nafasi yake, mgawanyo wa majukumu kati ya mke na mume ni outomatic!
Hakuna kiumbe jike kikataka kiendelee kuwa jike lakini kiwe nafasi sawa na dume! Au kinyume chake, hii ni ajabu sana!"
Kwa movement, hizi kila kizazi kinachofuata kitakuwa na matatizo zaidi ya kijinsia.
Naungana na mleta mada kwamba, hili litawasumbua saana!
Sent using Redmi Y2
Hongerenj wanawake na wasichana kwa siku ya wanawake Duniani , sisi wanaume tunawapenda sana na tunawapa pole kwa kutuzaana kutulea ingawa nanyi mnatakiwa muwe na shukrani kwa wanaume na ambao ndio walio shipa mpini wa maendeleo ya mwanamke .
Hata mlipokutana mjjni Addis Ababa, Ethiopia mwezi Juni 1995 mlitoa mapendekezo kwa kutumia ibara ya 66 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu za Haki za Watu kuelewa umuhimu wa wanawake katika dhima njema katika misingk ya usawa , amani , uhuru , utu , haki , umoja na demokrasia , nafasi ya mwanamke katika maendeleo , kuondoa ubaguzi kwa wanawake na haki ya ustawi wa Mtoto na mlizingatia Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Na. 1325/2000 kwa msaada wa ubia mpya wa Maendeleo Afrika NEPAD .
Humo mna mapendezo kadhaa mnashauri Nchi wanachama ziangalie katika
Ndoa - mnapendekeza namna ya kutengana , kuachana na kubatilisha ndoa
Upatikanaji wa haki na usawa mbele ya sheria
Haki ya kushiriki katika siasa na kutoa maamuzi
Haki ya kuwa na amani
Ulinzi wa wanawake katika migogoro ya kivita
Haki za elimu na mafunzo
Haki za kiuchumi na kijamii
Haki ya afya ya uzazi
Haki ya kupata maendeleo endelevu nk
Vyote hivyo vitahitaji ridhaa za wakuu wa nchi na bahati mbaya au nzuri wengi ni wanaume .
Ambapo nchi za Afrika zimeshaanza kuchukua hatua mbalimbali za kuwawezesha wanawake hasa kati uongozi , elimu , afya na kijamii .
Mikataba kama hii wanawake mnatakiwa muipokee bila ya kusahau mila na desturi duniani hazilingani kutokana na
SLEPT FACTOR
S- social
L- legal
E- Economy
T- Technology
Kwa nchi zetu za afrika ambapo maisha kwa ujumla bado ni duni kwa wanaume na wanawake ambapo Afrika wanaume ndio wameshika mpini wa utawala ma maendeleo ,
Wanawake muwe na imani wanaume hasa wa afrika wana nia nzuri nanyi ila wasiwasi na hofu ya mwanaume wa afrika ni jinsi wanawake mnavyopokea huku kuwezeshwa , nendeni taratibu msiende kwa pupa kwa mambo mengi yapo tangu kuumbwa kwa mwanadamu Adamu na Hawa .
Kuna mapokeo ya baadhi wanawake ma wasichana hasa walionda vyuo huko wakikutana na mitaala ya haki za binadamu mitaala ambayo mingi inakinzana na mila na desturi za Afrika , hapo ndipo tunawaona baadhi mmejawa na mihemko mkitaka mabadiliko over night .
Katika kosa ambalo wanawake wa Afrika mnatakiwa msilitende kama wanawake wengine walivyofanya hasa wanawake wa Ulaya na America , pamoja na yote angalieni maendelo ya mwanamke jinsi yatakavyosaidia zaidi Nchi na jinsi maendeleo ya mwanamke yatakavyoimarisha ndoa yake na familia yake msiingalie sana kutaka maendeleo ya mwanamke yatakayomwezesha kuwa huru sababu ya haki ya utu wa mwanamke hapo MTAWATIBUA WANAUME WA AFRIKA.
Kifupi sisi wanaume tunawapenda ndio maana tunakesha tukitafakari kuwawezesha ,
HAKUNA KAMA MAMA
MAENDELEO YA BABA MAMA YUKO NYUMA
HATA MAENDELEO YA MAMA WANAUME TUPO NYUMA YENU.
Sent from my iPhone using JamiiForums