Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Huyu mama ni tukio lililotokea Dec 27, mkoani Arusha ambapo mama huhu akiwa mjamzito alichezea kichapo cha mbwa koko kutoka kwa mume wake, na baada ya haya yote aliomba polisi wamkanye mume wake apunguze kumpiga kwakuwa bado anampenda. Uzi wa tukio hili uko hapa.
Nimekutana na video hii ikanikumbusha jambo kutana kwa dada ambaye namjua, unaweza kusema ni mtu wa karibu kiasi na mimi, ambaye hali yake haipishani sana na dada huyo hapo.
Hapa ndio nimepata swali la kumuuliza Waziri Dkt. Gwajima D, mtu kama huyu unamsaidiaje ambayo anapitia ukatili lakini haoni kama anaatahili kutendewa vyema na huyo aliyemfanyia hivyo achukuliwe hatua?
Huyu dada ambaye namjua naye utasema karogwa. Mpenzi wake amekuwa akimpiga mara kwa mara, wanasuluhishwa wanaendelea na maisha maana ameshashauriwa mara nyingi amuache mwanaume huyo lakini ni kama unatwanga maji kwenye kinu!
Sasa siku hiyo (kama miezi mitatu hivi iliyopita) alipigwa vibaya sana kiasi kwamba sasa hivi amepata tatizo la kuanguka kama degedege si degedege, kuzimia si kuzimia, alimpigiza kichwa wakati anamtembezea kichapo, lakini yule mpuuzi anakwambia anaogopa kwenda kumripoti polisi sababu anamuonea huruma atakamtwa.... mara aaah atabadilika tu akinioa 😩😩😩.
Baada ya kuchezea kichapo hivyo hakuweza kwenda hospitali sababu pia alikuwa kayumba kiuchumi. Kwahiyo tatizo hilo limeenda bila kuchekewa akiwa hajui nini kinamfanya mpaka anakuwa anaanguka hivyo without warning. Nahofia inaweza kuwa something deadly, ama siku likatokea la kutokea akapigwa na kufanywa kilema au akamuua kabisa.
Sasa kwenye mazingira kama haya unamsaidiaje mtu kama huyu apate msaada stahiki na anayefanya ukatili huo kuchukuliwa hatua stahiki? Dkt. Gwajima D?