WATCH: What to know about Kwanzaa
Kwanzaa, sikukuu ambayo jina lake linatokana na lugha ya Kiswahili, huadhimishwa na mamilioni ya watu kila mwaka, kuanzia Desemba 26.Maadhimisho ya mtu mweusi iliyoanzishwa na msomi na mwanaharakati Maulana Ron Karenga katika miaka ya 1960, sherehe hii ya wiki nzima huwaleta pamoja Waamerika wa asili ya Kiafrika wa dini zote kusherehekea urithi wao wa kitamaduni na kujitambua kuwa tuna asili pia imani na historia yetu.
Sherehe hii huadhimisha historia na jumuiya kwa vitu vya kitamaduni kama vile kinara, au kishikilia mishumaa, ambacho huonyesha mishumaa ya jadi nyeusi, nyekundu na kijani inayowakilisha kanuni saba:
- umoja,
- kujitawala na kujitegemea,
- Ujamaa kwa kazi ya pamoja,
- uchumi wa ushirika,
- madhumuni,
- ubunifu
- na imani.