SoC02 Tunaweza itumia JamiiForums kuleta mapinduzi makubwa ya Kibiashara miongoni mwetu, tuanze sasa

SoC02 Tunaweza itumia JamiiForums kuleta mapinduzi makubwa ya Kibiashara miongoni mwetu, tuanze sasa

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
Moja ya vitu ambavyo vinatuchelewesha sana watanzania basi ni ubinafisi, tuna ubinafisi wa kutisha sana na ambao hauna afya kabisa mbele ya safari zetu, nakumbuka kipindi cha nyuma ilianzishwa hadi Jamiiforum saccos, ila hii ilikufa si kwa sababu ya wizi hapana ni kwa sababu ya ubinafisi mkubwa sana tulio nao na sijji tuna rithi wapi.

Ni waambie ukweli kwamba bila kuunganisha nguvu, bila kukusanya idea pamoja hakuna sehemu tutafika, hatuwezi shindana na wachina au Wahindi au Wazungu, Zambia leo hii wanalia kwa sababu ya Wachina kuingia na kuanza kufuga hadi kuku, sasa wachina wakipelekea kuku wao sokoni ni hadi mzigo wao usishe na nyie ndio muuze.Kuna baadhi ya Wakenya walio wekeza hata hapa Tanzania wameunganisha nguvu zao wenyewe na kuja kuwekeza Tanzania, mimi nina rafiki zangu wa Kikenya wamewekeza Arusha na walijichanga kama wan ne na kuja kuwekeza na uwa nawaambia kwamba sisi hatuwezi kabisa kwa sababu ya ubinafisi mkubwa sana tulio nao na kuwaza hasi.

Jamii forum hasa jukwaa la ujasiriamali lina weza kuwa sehemu ya kuuzalishia makampuni, sehemu ya watu kukutana kubadilisahan mawazo, kushare experience, Ifike wakati tuache uoga wa kwamba hatuwezi kutana pysicaly kwa sababu tunaogopa kukamwata, haya mambo yalisha pitwa na wakati ni lazima tuitumie jamiiforum kupiga hatua zaidi ya hizi. Lazima twende physically sasa.

Moja ya maeneo ambayo tunaweza fanya kazi ni pamoja na ushirika katika biashara, kuwa na taasisi za kukopesha kama Saccos, ushirika wa masoko na kadhalika.

USHIRIKA WA BIASHARA; kupitia jamiiforum, watu tunaweza unganisha mitaji, narudia tena haya mambo ya kwamba ohoo hatuaminiani, ohoo, watanzania wezi, ohoo, sitaki shida, haya maneno ni ya kijinga sana na hayana tija na one day tutakuja kujuta sana kwa hizi furusa, ni lazima tuunganishe mitaji ili kushindana na wageni, hakuna namna wewe unafuga kuku 400 utaweza shindana na wawekezaji wenye kuchinja kuku 400,000 kwa wiki, au wanao fuga zaidi ya kuku million 4 hakuna namna, hakuna namna wewe utaweza furukuta mbele ya wawekezaji wenye mitaji na wenye maduka makubwa, hivyo ni lazima ni lazima tuache ubinafisi, tuache mawazo hasi kwamba Watanzania hatuaminiani, Watanzania ni wezi, mara sijui nini, tutafute njia sahihi za kuunganisha mitaji yetu inawezekana, kila mtu akitaka awe na kijikampuni chake hakuna sehemu tutafika niwahakikishie hili. Wachina wanakuja kwa kasi ya kutisha na wataturudisha nyumbani, hatuwezi shindananna wale jamii.

SACCOS; Wakenya wanapata mitaji yao sana kwenye saccos kuliko hata kwenye mabenki, na Kenya ni moja ya nchi zenye saccos nyingi sana Duniani, kama usha wahi fika kule na kukutana na gari zimeandikwa SACCO, hizo zote ni SACCOS, na zimewatao sana, sisi hili ni gumu sana kama kawaida tuna mawazo hasi, tunawaza hasi kuhusu saccos, mitaji hatuna, Mabenki mashariti yao ni magumu sana na Benki zinakopesha matajiri wenye mitaji mikubwa sana sio sisi wa lala hoi au wanyonge, hivyo kupitia jamiiforum tunaweza fanya jambo kuhusu kuwa na sehemu ya mitaji, make tunapata changamoto sana ya mitaji, hakuna sehemu ya kupata mitaji, tuangalie tunaweza fanya vipi. Ilikuwepo Saccos na ilikufa kwa watu kuto kujali si kwa sababu nyingine ile hapana, tunashindwa nini uwa na chombo cha kupata mitaji? Tuna kwama wapi? Tunatarajia weli tushindane na wageni kwa hizi mawazo yetu?

MASOKO;Hapa ni sehemu nyingine ya sisi humu kuunganisha nguvu zetu, ndo maana narudia kusema tunashindwa ku utilize JF, vilivyo, kuna wajasirimali wengi sana humu wana fanya biashara mbali mbali, yaani hata kusaidiana kwenye masoko pia ni shida? Nini shida? Wivu? Kwamba nikimsaidia Fulani kwenye soko atanizidi? Atafaidika sana? Tutengeneze mifumo ya kusaidiana kwenye masoko, narudia tena tumelala sana na jamii forum tunaitumia sana kwenye mambo mengine ila hatujaitumia kutengeneza pesa na utajiri.Mimi labda nazalisha bidhaa fulani na niko Arusha na kuna mdau mwingine wa jamiiforum anazalisha pia na yuko Arusha na anasoko na hana mzigo, tunashindwa kweli kuunganishana? Tuache mambo ya ajabu ubinafisi sijawahi ona faida zake, tufunguke tusaidiane kuuza.

MIKUTANO YA BISHARA; Hii pia ilikuwepo kipindi cha nyuma na ikafa, kwa nini ilikufa ni ubinafisi ule ule ninao usemea, tunashindwa kutengeneza hata mtandao wa biashara? Kufanya meeting? Hatuwezi kweli na hili? Hili pia ni ngumu sana? Hapana sio ngumu ila tuna ubinafisi mkubwa sana, ila tunaweza kuwa na mikutano ya biashara, tukabadilishana uzoefu, changamoto na kujega network za biashara zetu, hii sijui tunashindwa nini na yenyewe , sijajua kwa kweli ila tunaweza sana.

Ushindani wa biashara ni mkubwa sana hasa ukitlia maanani ushindanikutoka nje, chukukia mfano, hii nchi ina kampuni za ujenzi ngampi? Ni zaidi ya 5000 ila angali ni wa kina nani wanajenga barabara zetu, sasa hawa Watanzania Makandarasi hakuna hata mmoja mwenye wazo la waunganishe nguvu, yuko lazi kampuni yake ife au akose kazi miaka hata mitano kuliko kuunganisha nguvu, hizi ndo akili zetu, tunaona tukiunganisha nguvu watakao faidika ni wengine.

Ni waombe sasa kupitia jamii forum hebu twende mbele zaidi, haya mambo ya kuwa tunawaza negative hayana tija na wala sioni yanasaidia nini, twende mbele tuone tunaweza fanya nini, tuone tunaweza shirikiana katika engo gani na ni ipi hatuwezi shirkiana au inahitaji muda kidogo, inasikitisha sana wageni tena jirani zetu wana jiunga wanakuja kulima vitunguu Tanzania sisi tupo tumelala, huu ni uinga mkubwa sana, kuna jirani zetu wako Tanzania wanalima vitunguu kwa mitaji ya kuunganisha nguvu, na wamefanikiwa, why not us?

Tuitumie Jamiiforum kufaya mambo makubwa zaidi na mapinduzi mkaubwa sana kwenye Nyanja za uchumi, hii pia inaweza leta taswira nzuri sana kwa watawala na wakaona hii forum sio ya mchezo mchezo ina nguvu sana na pia hii ni njia pekee ya sisi kushindana na hawa wageni, Serikali haiwezi kusaidia mtu mmoj mmoja kushindana na wageni hilo halipo, kwamba ije ikusaidie wewe una kampuni yako moja ya ujenzi ikusaidie kushindana na wachiana? Hilo halipo. Tuanze sasa tuone na tushindwe kuliko kila msiku ni ohooo, watanzania hivi ohooo Watanzania vile.Hebu tuanze na tushindwe kuliko kuto kujaribu na kukalia kuwaza negative pekee.

‘’Nzi akiacha mambo ya jabu anaweza tengeneza asali, so na sisi tukiacha mambo ya ajabu tunaweza kuja fanya vitu vikubwa sana’’
 
Upvote 3
Back
Top Bottom