Tunaweza kuboresha Podium zetu Ikulu ili kuongeza taswira na muonekano wa unadhifu?

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
5,555
Reaction score
6,972
Huenda kuna maarifa mengine tusiyoyajua ila muonekano wa Podium au jukwaa za kuhutumia viongozi hauko katika muonekano nadhifu zaidi kutokana kuwa kuweka material ya bati, ambazo zimeonekana kuwa na michubuko na mabonde mabonde.

Kwa utajiri wetu wa misitu na aina mbalimbali za miti tungeweza kutengeza au hata kuweka Podium za mbao na kuleta unadhifu zaidi.

Moja ya vivutio vya vyetu ni sanaa ya uchongaji vinyago ( maarufu vya kimakonde) na uchongaji wa milango ya Zanzibar iliyotumika katika majumba ya kifahari. Kwa nini tusitumie vipaji hivi vya sanaa kutengeneza Podium nzuri na zenye kuvutia kama milango ilivyo?
Au kuna kazi yake material ya aina hiyo?
 
Wazo zuri kuliko haya mabati yenye taswira mbaya.
 
Mkuu umewaza vyema natumai wahusika watapita hapa na kufanya jambo.
 
Mkuu umewaza vyema natumai wahusika watapita hapa na kufanya jambo.
Wazo lako ni zuri kwani pia tutakuwa tunatangaza nchi na kuvutia watalii kama ROYAL TOUR VILE!
 
Ukweli mtupu.
alafu muonekano mbaya unaweza hisi majeneza ya watoto wanauzwa.
wawe wabunifu wazuri na usanifu wa rangi,kuna rangi zikiwa pamoja hata kama kitu kizuri kinaoneka kibaya.

wazingatie na kimo cha Rais wetu. Rais akisimama zinamziba sehemu kubwa ya mwili anaoneka kichwa tu kama muhudumu wa kibanda cha tigopesa!
 
Naam naamini wachonga milango wanaweza kuchonga pia podium zetu zikawa za unadhifu zaidi
 
Dizain mshika kibubu anatafuta uhalali wa kusain bili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…