Tunaweza kufufua shirika la Posta, kodi zilizopo sio rafiki pia sio rahisi kwa mteja kuzielewa

Tunaweza kufufua shirika la Posta, kodi zilizopo sio rafiki pia sio rahisi kwa mteja kuzielewa

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Pamoja na kazi nzuri ya Serikali ya kuboresha uchumi na miundombinu,
Nafikiri ipo haja sasa ya kuja na mpango mkakati wa kufufua shirika letu la posta kwani lina uwekezaji mkubwa wa miundo mbinu karibu Nchi nzima wa Mabilioni iliyojengwa kwa kodi za wananchi

Kwanini tusije na mpango mkakati na unaoeleweka wa kodi kwa bidhaa zinazopita posta, hasa kwa hizi bidhaa moja moja hadi tano hivi ambazo ndizo huingizia wenzetu pesa nyingi za kuendesha Shirika.

Hizi formula za kodi zilizopo kwa sasa sio rafiki lakini pia, sio rahisi kwa mteja kuzielewa zinafanya hata mtu asitake kuwatumia kwani hata ukiagiza Bidhaa nje ya Nchi huwezi hata kukadiria kodi itakuwa kiasi gani na ndio hukaribisha mazungumzo pale mzigo unapofika.

Mf; unatumiwa tu zawadi ya viatu/raba unaambiwa kodi 115,000, unatumiwa zawadi ya kasimu ka laki tano, unaambiwa kodi laki 4 nk nk nk hata Wazungu wanakata tamaa kutumia shirika letu kwani wanapotumia watu wa kawaida vizawadi vya kuwasaidia hushindwa kulipia kodi ya kuvitoa hadi aliyetuma tena ajulishwe achangie...

Naona kama tunang’ang’ania kodi kubwa ambayo hata hatuipati tunaacha shirika la Mabilioni linafilisika na kupoteza ajira kwa maelfu za wafanyakazi ambao nao wanalipa kodi kubwa
 
tuwape DP world tu, tumeshakubaliana kila palipokosa ufanisi tubinafsishe maana wenyewe hatuwezi kuleta ufanisi.
 
Kulifufua ni simple sana
1.serikali ipige marufuku mabus kusafirisha parcel
2.kuwe na Monopoly,ukitaka kuagiza bidhaa nje ni lazima ipotie posta hadi kukufikia.
3.walipe wafanyakazi vizuri
4.shirika litoe huduma ya delivery ya vyakula kwenye migahawa,yani shirika liingie mkataba na mahoteli

TTCL (japo hujaizungumzia lakini nalo ni shirika letu)
1. TTCL pekee ndio ipewe mamlaka ya kutoa huduma ya Internet Tanzania, na watoe huduma ya bei ya chini zaidi
 
Back
Top Bottom