Tunaweza kupunguza gharama za mwenge

Tunaweza kupunguza gharama za mwenge

Joined
Oct 13, 2018
Posts
35
Reaction score
260
Na Thadei Ole Mushi.

Tukiweza tuangalie upya utaratibu wa Mbio za Mwenge. Sio kila kitu kilichoanzishwa na wazee wetu kinakuwa na tija wakati wote.

Katika kipindi hiki Corona ikiwa inatikisa Dunia ni vyema tukapunguza Mikusanyiko. Fikiria Mwenge huu utapita kila Mkoa na kila Wilaya na kutakuwa na mikesha karibia kila Mkoa.

Cha pili gharama za kuukimbiza tungeweza kusema tumalizane na issue ya madawati mashuleni kabisa ingeleta tija kuliko kupoteza Fedha hizi kwa ajili ya mafuta ya magari, posho nk.

Kama issue ni mwenge kukagua Miradi ya Maendeleo nafikiri Tamisemi inatosha kwa waziri na manaibu waziri... Nafikiri wakuu wa mikoa, Wilaya na wakurugenzi wapo site kila siku. Hii Kazi ya kuzindua Miradi kwa Mwenge haina tija Sana.

Tunaweza kupunguza Gharama kwa kuwa na maadhimisho ya siku Moja unawashwa Tena Kilimanjaro ambako ndilo ulikotakiwa uwekwe kwenye Mlima tusome kauli Mbiu yake na watu watawanyike.

Katika nchi ambayo hatuwezi kuongeza Mishahara ya watumishi, tuna Miradi kibao inayohitaji Fedha sioni umuhimu wa kupoteza Fedha hizi kwenye kuukimbiza Mwenge.

Ole Mushi
0712702602

FB_IMG_1620805419458.jpg
 
Mwenge ndiyo Hirizi Kuu ya Amani, Umoja na Mshikamano mkubwa wa Watanzania tuliyoachiwa na Wazee wetu ( hasa kutokea Bagamoyo ) hivyo msiuhoji sana au kupoteza muda wenu juu yake.
 
point ya kuuweka kwenye mlima kilimanjaro ni nzuri ila kwa tabia zetu sisi watanzania itabidi ile sehemu unapowekwa uwekwe na ulinzi kama kambi hata ya mgambo la sivyo watauiba.
 
Mwenge ndiyo Hirizi Kuu ya Amani, Umoja na Mshikamano mkubwa wa Watanzania tuliyoachiwa na Wazee wetu ( hasa kutokea Bagamoyo ) hivyo msiuhoji sana au kupoteza muda wenu juu yake.
Hii ndumba haifai kizazi cha sasa
 
Bajeti ya mwenge ni kiasi gani na inaidhinishwa na mamlaka ya Bunge au wakina nani wapo nyuma ya hili? Tuhabarishane
 
Back
Top Bottom