Hivi chanzo hasa cha uchafu ni nini? Maana bila kujua ugonjwa ulipo utahangaika sana kumeza dawa lakini wapi...
Kuna sababu nyingi lakini kubwa hasa ninayoiona kwa nchi yetu ni kutolipa kipaumbele swala la usafi wa mazingira. Hapa najumuisha wananchi (yaani mtu mmoja mmoja, vyombo vya habari, makampuni na sekta zingine binafsi) na hata serikali (yaani serikali kuu, serikali ndogo, mamlaka na mashirika yote ya kiserikali) swala usafi halina uzito kwetu. Kwa maneno mafupi tunachukulia poa poa tu. Lakini, hivi unajua hili tatizo linaweza kuleta athari gani na je hizo athari zitampata nani? Acha basi nitaje walau athari moja tu;
Hili tatizo linaweza kuleta matatizo ya kiafya yatakayotutesa/yasiyotibika kwetu na hata kwa tunaowapenda sana ikiwemo watoto tutakaowazaa au tuliowazaa tayari!
Kadri tunavozidi kutochukua hatua, athari zitakuwa ngumu au kutowezekana kabisa kuziondoa. Muda wa kuanza kutoa kipaumbele kwa swala la usafi ni sasa!!! Je tunaanzia wapi? Nimejaribu kuelezea vichache
Nikianza na sisi mtu mmoja mmoja. Tunahitaji kubadilika mara moja! Hebu tuelimike na tustaarabike. Kuna sehemu ambazo serikali na wakati mwingine hata sekta binafsi imeweka miundo mbinu mizuri tu ya kuhifadhi uchafu lakini cha ajabu hatuifanyii matumizi sahihi. Utakuta mtu choo kipo lakini anakojoa kwenye chupa anatupa kwenye mtaro. We mwenzetu kwani una shida gani? Na wawanaomuona hawamkemei utasikia kabisa wanasema "mwamba huyo kashafanya yake", yani na sifa wanampa. Mtaro wa kupitisha maji machafu, we mwamakwetu mule unatupa taka ngumu! Ndoo ya kuwekea uchafu ipo lakini unatupa uchafu chini. La haula!
Hivi mnaelewa kweli kwamba athari za tabia za watu wa aina hii zitatuumiza sote sio tu walochafua peke yao! Sasa inakuwaje mtu anachafua nasi tunamuangalia tu kama vile kafanya kitu kizuri. Sote tunapaswa tukemee kama ambavo tunavokemea tabia zingine zisizofaa.
Kwa vyombo vya habari, mnayo nguvu sana kwenye jamii. Kama mkiamua kulivalia njuga hili mkatoa ushirikiano wenu basi swala la uchafuzi wa mazingira linaweza kuisha kabisaaa. Mfano, kwenye chombo cha habari unachomiliki ukaweka dakika 10 tu za kutoa elimu juu ya kuondokana na uchafuzi wa mazingira, ikanaoneshwa athari zake, ikatolewa mifano nchi safi na chafu, kwa ufupi mkatumia ubunifu wenu na watangazaji wenu kuhakikisha ujumbe unafika.
Pia mkaweka vipindi kwa ajili ya kuonesha ubunifu mbalimbali unaosaidia kuepukana na uchafuzi wa mazingira hiyo itaamsha pia wataalam kuja na mbinu za kuhifadhi uchafu, kuchakata tena uchafu (recycling) au za kuzalisha taka ambazo ni rafiki katika mazingira.
Kama mlivoinua sanaa, mpira wa miguu, masumbwi n.k., hili la uchafuzi wa mazingira pia mnaliweza kwani nguvu zenu tushaziona zinavoweza kuleta matokeo makubwa kwa jamii.
Kwenu sekta binafsi, zipo ambazo zinaisaidia sana jamii kwenye swala la mazingira, zipo pia ambazo hazijigusi kabisa na mbaya zaidi zipo ambazo ndo wazalishaji wakubwa wa uchafu au bidhaa zao zinachangia kuleta uchafuzi mkubwa wa mazingira.
Jamani! Si sawa makampuni kuwa yanapata faida kubwa ilihali wanaingiza jamii kwenye gharama kubwa kutokana na shughuli za uzalishaji zinazofanywa na sekta binafsi. Hebu hakikisheni shughuli zenu zinakuwa ni rafiki kwa mazingira.
Zidisheni ubunifu katika mnavyozalisha kuhakikisha haviongezi uchafu pia wekeni sera na mikakati ya kwamba moja kati ya harakati zenu za kurudisha kwa jamii "CSR" ihusishe kutatua tatizo la uchafuzi wa mazingira. Mfano, kampuni ikaweka mkakati wa kuhakikisha maeneo yote ya umma mnayawekea ndoo za kuhifadhia taka tena sio moja, ziwe za kuweka taka za aina tofauti tofauti kwa ajili ya urahisi wa kwenda kuzichakata tena.
Katika pita pita zangu kwenye mitandao ya kijamii nimeshaona nchi za wenzetu wamewekewa sehemu maalumu ya kuweka chupa za plastik, na unapoweka kila chupa moja ina thamani hivo unaodoka na pesa yako kila unapoweka taka za plastik japo ni pesa ndogo lakini ni motisha!
Kundi la mwisho na nimeliweka la mwisho kwasababu ya nguvu yake. Hawa wakiamua kitu kitekelezwe basi kinafanyika bila pingamizi hasa kikiwa kina nia nzuri. Kundi hili ni serikali yaani seriakli za mtaa, mamlaka za kiserikali, taasisi za serikali, vyomba vya serikali, serikali kuu na wote ambao wako ndani ya kundi la serikali.
Kwanza kabisa, hayo yote nilioyataja juu kwa mamlaka yenu mnaweza kuyasimamia yatekelezwe.
Tukianza na kuwasimamia mtu mmoja mmoja, serikali ya mtaa inaweza kufanya kazi katika maeneo tunayoishi. Taka zisitupwe ovyo na zikusanywe kwa mpangilio maalumu (yani taka zitenganishwe za chakula kivyake, karatasi kivyake na plastics kivyake n.k.).
Pia maeneo ya umma, serikali inaweza kushirikisha vyombo vya usalama kusimamia na kuhakikisha wanaokiuka wanafikishwa vyombo vya sheria kwa hatua stahiki. Kama ambavyo imewezekana kuondoa vibanda sehemu zisizoruhsiwa, tumeona mgambo wakifanya kazi yao. Hivo tunaweza kuwatumia pia katika usafi au tukatumia shirikishi.
Serikali pia inaweza kuweka mkono wao kwenye vyombo vya habari kwa kuwahamasisha waweke matangazo yanayohusu usafi wa mazingira kwa muda flani katika wiki kwa kurudishiwa kiasi cha gharama za tangazo hilo hivo vyombo vya habari vinaweza kuwahusisha watu mbalimbali wenye utaalamu na maswala ya mazingira kutengeneza matangazo hayo ili yawe yenye tija.
Na pia, serikali ichukue hatua kali dhidi ya kampuni zinazochangia uchafuzi wa mazingira kama ambavyo tayari tumeona wanaoleta kelele wameshungulikiwa na NEMC, kasi hiyo ifike na kwa kampuni zinazozalisha taka.
Pia wanaweza kuwawekea kodi ya uchafuzi wa mazingira yaani asilimia 10 ya mauzo kama kodi ya kuzalisha taka.
Mbali na hilo, serikali inaweza kuhamasisha makampuni katika utunzaji wa mazingira, mfano kwa kuwapunguzia kodi wanaotengeneza njia za kutunza mazingira au wanaozalisha bidhaa zinazochangia utunzaji wa mazingira au kuwapa mkopo wa mtaji wale ambao wanaanza kampuni zinazotengeneza bidhaa ambazo zinatumika kutunza mazingira. Angalizo, mitaji hii ifuatiliwe kwa umakini mkubwa ili pesa zisiishie kwa mafisadi.
Sheria za mazingira nazo zitazamwe tena kama bado zinatusaidia katika hali tuliyo nayo sasa, na kama ni ndio basi zisimamiwe kama zinavosimamiwa sheria zingine zisikae kama geresha, au la sheria ziongezwe na zikazwe zaidi.
Bajeti yetu pia iseme kwa uwazi na ukubwa namna imegusa usafishaji wa mazingira.
Na kwenye elimu, somo la usafi wa mazingira liwepo na liwe la lazima kuanzia msingi hadi sekondari ili watu wapate ufahamu wa kitaalamu. Na kadhalika na kadhalika siwezi kumaliza yote kwasasa.
Kuna namna nyingi za kufanya hayo niliyotaja ni machache tu kulingana na nafasi niliyopewa na jamii forum. Itoshe tu kusema, njia zote nilizotaja zitawezekana kama tu tutalipa kipaumbele swala la usafi wa mazingira yetu.

Upvote
0