SoC04 Tunaweza kuzuia majanga mbalimbali na kama sio kuyamaliza kabisa haswa kwa kutumia teknolojia

SoC04 Tunaweza kuzuia majanga mbalimbali na kama sio kuyamaliza kabisa haswa kwa kutumia teknolojia

Tanzania Tuitakayo competition threads

MIKAEL MTANZANIA

New Member
Joined
May 28, 2024
Posts
3
Reaction score
2
kwa mkono wa: Mikael Mtanzania.

Yeyote asiyekubali kubadilika basi mabadiliko yatamuacha nyuma.
Tumekuwa tukisikia malalamiko mengi hasa yanapotokea majanga au unapotokea moto umewaka sehemu mfano majumbani mwawatu au kwenye majengo kumbi na sherehe malalamiko yanayo tokea ni kuwa zima moto wamechelewa kufika sehemu husika lilipotokea janga la moto au wamefika huku hawana maji ya kutosha, naamini pengine hata wewe ni mmoja ya watu walio wahi kutoa hukumu kuhusu zima moto hawafiki sehemu kwa wakati.

kama ambavyo teknolojia imekuwa basi tunaweza kuitumia kisawa sawa kutusaidai kwenye maswala haya ya majanga makubwa, linapotokea tukio la moto kuwaka mahala fulani au kwenye jengo flani inalazimika kupiga simu kwa zima moto ukweli ni kitendo kizuri lakini jiulize itagharimu muda gani mpka kikosi cha zima moto kiweze kufika palipotokea tukio ukilinganisha na foreni za barabarani

Niwazi kuwa kikosi cha zima moto kikiwa kinawahi sehemu kuokoa kinayo haki ya kupita popote pale ili kufikisha msaada eneo husika lakini kiuhalisia ni mzunguko mrefu sana ambao unaweza kugharimu mpaka lisaa, Kwaiyo kama utatumika muda mwingi hivyo ni ngumu kuokoa chochote na zaidi ya hapo kila mmoja atabaki anachagua wa kumutupia lawama.

Ninalijua mbinu zipo nyingi sana za kupambana na maafa mbalimbali lakini nyingi zimekuwa zikifeli na maafa yakitokea lazima yaharibu kwa asilimia mia moja.

(Ninaliomba nikazie kwenye zimamoto kwanza na mbinu gani zitumike kwa kuzuia majanga kama hayo kwa kutumia teknolojia)

Lazima kuwe na system kutoka kwenye jengo au nyumba mpaka makao makuu ya zima moto ambayo ipo connected na hata kujenga jengo lazima Ufatwe utaratibu maalumu wa nchi utaratibu huo uwe ndani ya system ili inapotokea shida iwe rahisi msaada kupatikana, system hiyo iweze kutambua dalili na viashiria kuwa nyumba flani maeneo flani au kwenye jengo flani kuna viashiria vya moto muda wowote panaweza kuungua, hii itawasaidai upande wa zima moto kufika kwa wakati eneo la tukio na bila kupigiwa simu.

Mfano mdogo nchi kama Ufaransa tukio lolote la kuungua au kuwaka kwa moto lazima kikosi maalumu cha zima moto kijue hata kabla ya mwenye nyumba kujua au mmliki wa jengo, kwani wamaefunga system maalumu ambazo hata kama ukiunguza maharage ule moshi ukifuka watajua kuna shida ya moto mahala flani.


Sitaki kuamini kuwa nchi yangu inashindwa kuwajibika kutafuta solution simple kama hii itakayo saidia kupunguza matatizo ya moto, lazima tukubali kuitumia teknolojia na tusikubali ituache nyuma kabisa.
Kuna wakati majanga ya moto yanatokea wewe haupo nyumbani kwako lakini kukiwa na system nzuri ambayo iko connected na makao makuu ya zima moto itakusaidia wao kuweza kujua kuwa nyumbani kwako kuna dalili za hatari na wao kufika mapema.

Tusikubali tatizo mpka litokee ndio tuanze kupigiana simu wakati kuna njia zinazoweza kujua tatizo hata kabla alijatokea, lazima jeshi la zima moto litambue wakati linaendelea kubolesha namna ya kujaza maji kwa haraka kwenye magari yao lazima pia watambue tunaweza kutambua shida ya moto hata kabla ya moto kuwaka.

Hii kwenye video hapo chini ilitokea uko kwenye nchi za watu katika chuo kimoja, Kuna mtu alikuwa anapasha chakula akasahau Kwa microwave, moshi ukafuka na ukagusa zile smoke detectors ndio alarm ikalia hivyo wanafunzi wakamulia wote chuo kizima watoke nje, hata kabla ya wanafunzi kusimama vizuri magari manne ya zima moto yakatua ndani ya sekunde chache, walipofika zima moto wakaenda ndani wakangalia shida nini, ndio wakakuta Kuna mtu alikuwa anapasha chakula akasahau kwenye microwave ndio maama moshi ulipofuka walijua na waliona kwenye system yao, wakazima alarm wakaondoka zao, lakini harakati zote hizo zilitumia ndani ya dakika 15.




Kwa hiyo lazima tuwe na system zilizo connected na makao makuu ya Zima moto kuzuia majanga kama haya, (mbona inawezekana kabisa)

sikushangaa kwa nini zimamoto wametumia muda mfupi sana kufika kwenye tukio, ila nilishanga jinsi ambavyo system zao zipo active sana inapotokea dalili ya hatari kama hiyo.


Mfano mwingine ni pale linapotokea bomba la maji limepasuka pengine nyumbani kwa mtu au barabarani, itagharimu siku moja au mbili mbele ndio bomba lije kuzibwa na hapa utakuta lita nyingi za maji zimepotea na kuitia taasisi hasara kwa sababu ya kusubilia taarifa kutoka kwa msamalia mwema, na wakati Dawasco wanweza kutafuta conection itakayo wasaidia wao kujua sehemu flani kuna bomba

limeleta shida hivyo inapaswa timu ya mafundi kufika mapema.

Vivilevile upande wa TANESCO Binafsi sidhani kama kulikuwa na haja ya kupigiana simu au kupelekeana taarifa inapotokea shoti ya umeme au changamoto ya umeme, nilitamani kusikia wao Tanesco ndio wakipiga simu na kuuliza hata nyumba ya mtaa ulioleta shida ya umeme, kama wangeunganisha na system inayowapatia taarifa wao moja kwa moja kupitia mifumo yao.

Ni sadiki kusema inawezekana kama gridi ya taifa ikipata shida wanajua na pengine iko mbali watashindwaje kuweka mfumo kwa mteja wao unaowaptia taarifa moja kwa moja, endapo ikitokea changamoto.
inawezekana kuzuia kabisa majanga kama haya ikiwa tutaitumia vyema teknolojia.

Ni yule mtibeli wa kisukuma.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom