SoC01 Tunaweza tukapunguza mimba za utotoni kwa kutumia nyenzo moja tu, Yaani utoaji wa elimu kwa jamii

SoC01 Tunaweza tukapunguza mimba za utotoni kwa kutumia nyenzo moja tu, Yaani utoaji wa elimu kwa jamii

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Habari ya kwako ewe mfuatiliaji wa makala hii natumaini langu sote tuwazima wa afya.

Leo nimekuja kwenu tuliweke bayana swala linalohusu kwamba ni kwa namna gani tunaweza kuwanusuru mabinti kupata mimba zisizotarajiwa pia kwa namna gani elimu ya ujinsia itaweza kukomboa vijana wote kwa ujumla kujiingiza katika vitendo vya ngono zembe na badala yake kusimama katika njia waliyoichagua kwenda nayo baada ya kupata elimu hiyo.

Kwanza kabisa elimu ya ujinsia ni elimu ambayo inatolewa kwa vijana wenye miaka angalau (16) na kuendelea lengo kubwa likiwa ni kumuandaa kijana dhidi ya changamoto za ujinsia zinazoweza kumzonga kwa wakati wa maisha yake ya ujana kipindi ambapo yupo shuleni au mtaani tu. Sasa jambo kubwa mahususi ni kwamba wazazi wanalo jukumu la kuwapa elimu ya ujinsia vijana wao ili waweze kutambua nyendo zao na kujua palipo pema na pabaya na kama wengi tujuavyo kwamba ujana ni maji ya moto.

Lakini Hasa Tatizo limekuwa kwa wazazi wengi kwamba wanaogopa kuwaambia vijana wao mambo yanayohusu ujinsia huku wazazi wakidhani kwamba vijana wao hawapaswi wasikie mambo kama hayo kwa kujali labda vijana wataharibikiwa kwa kuambiwa hivyo.

Mda mwingine mzazi anashikwa na aibu ya Kumwambia mwanae vitu kama hivyo bila ya kujua kwamba kama kijana huyo asipoambiwa leo hii usishtuke leo hii au kesho tu ukakuta kafanya ngono zembe huko mara gafla kapata magonjwa au la! Yaweza kuwa kampa binti wa watu mimba je? Ikiwa we ni mzazi hapo utakua umemlinda mwanao au umemwangamiza wewe mwenyewe kwa kudhani hapaswi kusikia maswala yanayohusu jinsi na ujinsia pia wewe ni mzazi sasa fikiria nani atakaye mwambia kiundani kama unavyotakiwa umwambie huyo kijano wako. Hivyo kuna mengi ndani ya elimu ya ujinsia ikiwemo jinsi ya kuepuka maambukizi na hata kujua kuhusu elimu ya uzazi wa mpango Hata pia kuielewa elimu ya ujinsia kwa ujumla.

Hivyo ni ombi langu kwa wazazi na mtu mmoja mmoja atakaeguswa na hili ni kwamba yawezekana unaye binti yako au kijana wako mpe elimu ya jinsi na ujinsia usikae usubiri mpaka akafundishwe na mwalimu je?

Utajuaje kama anaweza kuharibika kabla hata ya yeye kupata hiyo elimu kutoka kwa mwalimu wake huko shuleni.wazazi jitahidini kutoa elimu lakini pia serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoguswa kwa ukaribu na hili waendelee kutoa elimu na kufanya uhamasishaji kwa vijiji na jamii nzima kiujumla Kwa hakika tukifanya hivyo tutapunguza watoto wa mitaani kwakuwa vijana watakua tayari wamepata kuijua vizuri elimu hii kuwafanya Vijana kuwa na afya bora. Ili waweze kusoma na kuendelea mbele kwa ujenzi wa taifa.

Asante
#mabadiliko yanaanza na sisi wenyewe.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom