Lah Fredoh
New Member
- Oct 31, 2020
- 1
- 0
Dunia imejaa watu wenye vipaji, ujuzi, elimu na maarifa ya kila aina na tofauti tofauti kwenye nyanja mbalimbali, ambazo licha ya uwezo walionao,hawana ajira na wamekosa fursa au kutopewa nafasi ya kuonyesha taaluma, ujuzi, vipaji au maarifa waliyo nayo.Wote tunaelewa changamoto za soko la ajira, Hii ni changamoto ambayo wengi wetu imetukuta au tumeshawahi kukabiliana nayo Kwa namna Moja ama nyingine,hasa pale unapenda kwenye udahili ukiamini unanafasi ya Kupata ajira lakini unashangaa kachukuliwa mwengine ambae hana sifa!
Lakini vipi kama kungekuwa na mbadala wa hili,tungeweza kuunda platform Moja matata sana ambayo inaweza kukutanisha Hawa watu wote Kwa pamoja wakakaa chini na kuanza kuumiza vichwa namna ya kuzitambua, kuzikabili na kuzibadilisha changamoto za kila siku za kimaisha kuwa fursa ambazo zingewaingizia kipato.
Je, unaonaje badala ya kusubiri milango ifunguliwe, kwanini tusiifunguwe wenyewe? Badala ya kusubiri fursa zitufuate Kwa Nini tusizitafute wenyewe?
Nimekaa nikatafakari kitu gani kifanyike basi kuweza kufanikisha hili:
---
Maono(Vision): Lazima kuwe na Kundi linaloamini katika Mabadiliko na lenye kuona mbali.
Fikiria kundi la wataalamu wenye nia moja wakikusanya ujuzi wao kushughulikia changamoto Fulani, wakatafakari Kwa pamoja na kutoa suluhisho Bora Kwa haraka pia gharama ziwe nafuu maradufu.
Hebu fikiria eidha tuunde jukwaa, taasisi,au shirika au chochote kile ambacho kitaweza ku-draw attention ya watu Kwa namna itakavyokua na uwezo wa kutatua changamoto ngumu na kutoa suluhisho za kiubunifu kwamba Nini kifanyike hatua Kwa hatua ambapo mtu yeyote anaweza kusaidika popote,Kwa jambo lolote na Kwa haraka! Hili si ndoto tu—inawezekana.
-Tunaanzaje?
1. Hatua ya kwanza ni namna ya Kupata Hawa wataalamu wa nyanja mbalimbali na wawe wenye uelewa au kuelewa changamoto kubwa za kimaisha ya kila siku zinazotuzunguka na zenye fursa.
Ni masuala gani tunayoyaona katika jamii zetu yanayohitaji kushughulikiwa Kwa haraka?
Tunawezaje kutumia ujuzi wetu wa kipekee kuyakabili na kuyatatua?
Ni njia gani za ubunifu tunaweza kuchukua ili kutoa suluhisho la kudumu?
Tuanze kwa kufikiria na kufanya utafiti. Pamoja, tunaweza kuchora ramani ya mapungufu katika sekta mbalimbali kama vile elimu, afya, teknolojia, au miundombinu na kuunda mikakati madhubuti ya nini kifanyike Kwa kutoa ushauri wa kitaalam kupitia watu tutakaokuwa nao katika jukwaa hili.
2. Kutumia ujuzi tulionao
Kila mmoja wetu ana kitu cha kuleta mezani—iwe ni utaalamu wa kiteknolojia, ubunifu, uongozi,kipaji au ujuzi Fulani kwenye nyanja fulani. Kwa kuunganisha nguvu zetu, tunaweza kuwa na nguvu ya pamoja yenye sauti kubwa
Hii inahusisha:
Kutambua nguvu na shauku za kila mtu.
Kuunda timu zinazolenga majukumu au miradi maalum.
Kuhamasisha uvumbuzi na mawazo mapya.
---
Kwa Nini Hili Ni Muhimu
Mpango huu si kuhusu kupata kazi tu au pesa; ni kuhusu kuunda kusudi la pamoja, kuleta mabadiliko, na kuachana na Ile dhana ya kusubiri kuajiriwa. Ni kuhusu kuthibitisha kwamba, kwa mawazo sahihi na ushirikiano, tunaweza kubadilisha changamoto kuwa fursa na kubadilisha jamii.
---
Mtandao mkubwa wa Hawa wataalamu unahitajika,namna ya kuujenga nayo nichangamoto nyingine,Nimeona nililete humu hili wazo,kama Kuna wadau wataliunga mkono na wanamapendekezo basi mnakaribishwa Ili tuanze huu michakato mzima!
Jiunge Nami na Uwe Sehemu ya Mabadiliko na kama wazo hili linakugusa na unataka kuwa sehemu ya safari hii, basi tuwasiliane! Nitaandaa group dogo la watu wenye shauku na ujuzi ili kuanzisha mpango huu pale nitakapopata idadi ya kuridhisha.
Karibuni!