GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Wengine wanaweza wakaishia kusema kuwa ukimchungumza sana bata hutamla, lakini acha tu ukweli usemwe! Watanzania wengi bado ni wachafu!
Siwakejeli! Nitaanzaje kufanya hivyo na huku na mimi ni Mtanzania? Nitawezaje na huku hao ni ndugu zangu, mama zangu, dada zangu, kaka zangu na watu wa "nyumbani" kwetu? Shauku yangu ni kutamani kuona tunapiga hatua kwenye hilo eneo.
Najua ukienda kwenye mikoa ya Kigoma na Kagera, hasa maeneo yanayopakana na Burundi, watakuambia kuwa Warundi ni wachafu. Lakini kwa kuwa na mimi nimezunguka karibia mikoa yote ya Tanzania, nimejiridhisha kuwa japo wengi hawajioni hivyo, lakini idadi ya Watanzania bado ni "wachafu", hasa linapokuja kwenye suala la vyakula.
Kwa sababu ya niliyojionea maeneo mbalimbali, nimekuwa nikihofia wakati mwingine kula chapati kwenye magenge ya vyakula. Bora ninywe supu bila vitafunwa kwa kuwa yeyewe ni ya moto kuliko chapati zinazoshikwa kwa mikono mitupu, mikono iyo hiyo inayopokea hela inayotoka kwenye mikono tofauti kwa watu tofauti!
Hilo la chapati ni moja tu, lakini mifano ni mingi!
Nipo safarini kwenye mkoa mmoja Kanda ya Ziwa. Ni maeneo ya vijijini. Jana Mchana ulipofika muda wa kwenda kula, nililazimika kwenda kaumbali kidogo, umbali wa sh 1,000/= kwa gari, kutafuta chakula. Kamghahawa nilikoingia ndiyo wa "hadhi" ya juu eneo hilo.
Baada ya kuagiza chakula, nilikodoa macho kuangalia vile kinavyopakuliwa! Kilichofanyika, ndicho nilichokitarajia. Kulionekana changamoto ya kiusafi!
Bakuli la mboga liliwekwa juu ya "figa", ambalo lilikuwa jeusi kwa masinzi. Baada ya wali kupakuliwa, lile bakuli lenye mboga lilichukuliwa na kukalishwa juu ya sahani yenye wali! Sikumbuki kama kitako cha hilo bakuli lenye mboga kilifutwa kwanza kwa mikono au kilikalishwa tu vivyo hivyo, sikumbuki!
Mhudumu alipokileta, nilianza kumhoji sababu ya kufanya hivyo! Alipoomba msamaha, niliamini kuwa somo limeshaeleweka, hivyo kwa kuwa nilikuwa na njaa na sikutaka kuwaitia hasara, niliutoa wali uliokuwa umekaliwa na kitako kichafu cha bakuli na kuendelea kula.
Kwa kadiri ya uelewa wangu, mazingira kama hayo ni ya kawaida sana nchini! Lakini siamini kama inapaswa kuwa hivyo.
Nafikiri mabadiliko yanahitajika!
Kama unakubaliana nami, pendekeza suluhisho!!!