Tunayalaumu mataifa yaliyoendelea kwa kutuangamiza, huku nasi tunajiangamiza

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
418
Reaction score
526
Sisi wenyewe watanzania hasa ninaowalenga wamiliki wa maabara na maduka ya dawa. Hawa watu wanaushirikiano na wanacheza faulo sana yani unakuta mtu wa duka la dawa ye anauza dawa na hata muda kuhoji kama mhitaji wa dawa amepima na kupewa maelezo ya dokta ilimradi kataja jina la dawa anahudumiwa.

Shida zaidi inakuja kwa mtu wa maabara wengi si waaminifu wao wanapima mkojo na kusema ni UTI hata kama ni dalili tu zimefanana wakati unampa maelezo ya awali.

Sasa kwa hali hii tunachangia miili kuwa sugu dhidi ya kusikia dawa na kuwajaza sumu ktk miili yao kwakuwa dawa anazopewa haziendani na tatizo hivi ndiyo tunauwana wenyewe taratibu.Ni vema wahusika ktk sekta hizi wawe makini afya ni mtaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…