Tunda awekwa kitimoto na familia yake kwa kutembea na mume wa mtu 'Kinje'

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

DAR ES SALAAM: Kufuatia sakata la video akiwa anafanya vitendo vya kimahaba na mume wa mtu, Kinjekitile Kingunge ‘Kinje’ kusambaa mitandaoni hivi karibuni, muuza sura katika video mbalimbali za wasanii wa muziki Bongo, Tunda Sebastian amejikuta akiwekwa kitimoto na familia yake.

Uchunguzi wa gazeti hili kupitia kwa rafiki wa karibu na Tunda ulionesha kwamba baada ya video hiyo kusambaa ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani wazazi wake walikasirishwa mno na kitendo hicho, ndipo wakamweka kitimoto japokuwa hadi sasa hajakaa nao sawa.

“Familia ya Tunda ilimweka kitimoto mwanadada huyo na kumsema sana ambapo aliahidi kwamba atabadilika na akawaangukia wazazi wake na kuwaomba msamaha licha ya kuwa haikuwa kazi rahisi kwa kweli,” alisema rafiki huyo.

Ijumaa Wikienda lilimtafuta Tunda ambaye alieleza kuwa, baada ya video hiyo kuvuja kulitokea mtafaruku mkubwa kwa wazazi wake huku mpenzi wake akikasirishwa na kitendo hicho na hadi sasa hazungumzi naye.

“Nimejifunza sana maana ile video imenivuruga sana kwa kweli kwani wazazi wangu walikasirika sana, mpenzi wangu mpaka sasa haongei na mimi ila bado ninaendelea kumwelewesha kwamba ile ilikuwa ni pombe tu.

“Naamini hasira zake zikiisha atanitafuta tu maana najua ananipenda, nimekoma kunywa pombe na nimeshaacha kabisa kwa kweli,” alisema Tunda.

Video hizo zilikuwa gumzo mitandaoni kabla ya Kinje kufiwa na baba yake, Mzee Kingunge hivyo watu kuacha suala hilo kwani ni kumuongezea maumivu juu ya maumivu.


Muungwana
 
daah pombe zaidi ya mara 2 tofauti mnakunywa na kinje
 
Hii ya kuwekwa Kiti Moto kwangu sio habari.., Ila siku akiwekwa kitu chenye Ncha Kali naomba mnitag bandugu!!!
 
Nauliza jamani Mtu aliyesoma ICT VETA anaweza kusoma Diploma in Computer Science ktk vyuo vyetu hapa Tz?!
 
Walimwengu tu ndo wanasubiliwa kumfunza maana wazazi washashindwa
 
Tunda weehh..... a.k.a yahaya!!
 
Chain itamtuliza tu, mtakaposikia anasingizia uchawi, ndipo dunia itakuwa imemfundisha adabu.
 
Tunda akija kuolewa atatulia sana kwa maana kamaliza starehe zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…