Tunda/mboga zinaloliwa kimasihara

Tunda/mboga zinaloliwa kimasihara

Gily Gru

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
8,632
Reaction score
23,673
Fenesi haliliwi bila mafuta, lazima upake mikono mafuta Ili lilile vizuri. Wabishi wanakula bila kupaka mikono mafuta Na wanadai utamu WA fenesi Ni Utomvu. Tunda hili halioshwi Na Utamu wake ni pale unapolamba mikono….
fenesi.jpg


Bungo kiutaalamu lazima ulitie kidole ndio uliweke mdomoni. Likiwa mdomoni raha yake limumunywe taratibu mpaka utamu uishe. Wajuvi huwa hawali bila chumvi, huwa linatiwa chumvi kisha linatiwa kidole wanalikoroga na kidole mwisho wanalimumunya. Utamu wake unakilea pale unapolamba kidole…
photffo-4.jpg



Embe dodo kiutaalamu huliwa kwa kunyonywa, lazima ulishikilie na mkono mmoja kisha ulinyonye mpaka kokwa. Wataalamu wanaolijua vizuri huwa wanaliita embe Ng’ong’o na wanalila likiwa limeiva ila wabishi wananyonya hata likiwa bichi, litaivia tumboni. Raha yake uwe unaliminya wakati unalinyona na kumumunya. Wajuvi wakimaliza kulila lazima wanyonye kokwa…
mango.jpg



Ndizi mbivu ni tunda lenye sukari na haliliwi mpaka limenywe maganda. Kitaalamu ndizi huliwa kwa kumenywa maganda. Watu wanapenda kumenya maganda nusu huku unalimenya kidogo kidogo na kulila mpaka ufike chini. Wabishi wao humenya yote ndio wale na wakimaliza kula wanachukua yale maganda wanasugua meno ili yawe meupe pee; au wanachukua yale maganda wanajisugua kiungo kinachouma kupunguza maumivu…..

Pic+ndizi.jpg


Chungwa ni tunda tamu sana na humenywa kwanza kisha linakatwa kati na ukilishika lazima uliminye na kulikamua mdomoni. Wabishi wanapenda wakila chungwa wanalikamua, wanalinyonya na wanakula mpaka nyama zake za ndani. Raha ya chungwa mbegu lazima uteme kwa kuzirusha….
726381571-H.jpg



Chenza kitaalamu unalimenya na kulila nyama ya ndani. Chenza haliliwi kama chungwa, usije kula chenza ukazani umekula chungwa. Wabishi wanamega chenza utazani chenza, na wanakula kisha wanatema mbegu zake, Raha ya kula chenza lazima ulimege ule kipande kimoja badala ya kingine……
cm.jpg



Muwa ukiwa umekatwa si tunda ila ukiwa umepandwa ni tunda. Kitaalamu huwa hutolewa ganda na kuliwa ndani kwa kutafunwa, kisha unakaushwa utamu na kutemwa. Wabishi huwa wanakula muwa na maganda yake yote kisha wanatema. Wabishi hao huwa wanakula mpaka fundo. Ila utamu wa muwa ukikolea basi hadi macho yatafungwa…
main-qimg-c5bebcdad4f62688b1926a02836ab3c6-c.jpg



Pilipilini tunda linalowasha sana na huliwa zikiwa mbichi au zimepikwa. Pilipili zenye kuleta muwasho mzuri ni pilipili mbuzi au mwendokasi. Utamu wa kula pilipili lazima makamasi yadondoke. Wabishi huwa wanakula pilipili na mbegu zake na makamasi yakidondoka hawayafuti huwa wanayameza kabisa. Raha ya kula pilipili ni pale unapoenda kunya matako lazima yawashe sana na ukila nyingi ushuzi wake unakuwa unawasha pia. Wale wanaovamia pilipili na wako kimayai mayai lazima chozi lidondoke na wapige chafya za kutosha….
image-20160108-3317-1j96zt7.jpg

2954F8B300000578-0-image-m-61_1433357859738.jpg


Kitunguu ni mboga ambayo inaungwa kwenye mapishi mengi kuleta ladha. Wenye magonjwa ya unene wa kupitiliza au presha huwa wanashauriwa wale vitunguu vibichi. Hata wabishi wamekwama kwenye kitunguu, maana kikimenywa lazima chozi litoke. Hata uwe JIWE vipi kitunguu raha yake huliwa huku unalia bila kupenda….
austria-man-in-kitchen-chopping-onions-X39N45.jpg



Wajuvi fungukeni Ni Mboga/Tunda gani uliwaji wake lazime uwe WA kimasikhara masikhara Tu. Je kitu gani unapenda Kukila, Kutafuna, Kumumunya au Kulamba Kimasikhara?????
 

Attachments

  • 1582575592513.jpeg
    1582575592513.jpeg
    95.8 KB · Views: 10
Nazi haieleweki kama ni Tunda au Mboga, ipo kote kote. Nazi huwa inagongwa, unainywa maji kisha unaipeleka nyumbani Ikakunwe na mbuzi...


Majuzi nikiwa napita sokoni nilinunua nazi ili niende nyumbani nikazile kimasikhara ila zilitia huruma mpaka nimeirudisha sokoni wanibadilishie. Kusema ukweli nilishindwa kuila Kimasikhara kabisa yani... (Sitanii kabisa)
IMG_20191212_170111_6.jpg

IMG_20191212_170154_4.jpg
 
Nazi haieleweki kama ni Tunda au Mboga, ipo kote kote. Nazi huwa inagongwa, unainywa maji kisha unaipeleka nyumbani Ikakunwe na mbuzi...


Majuzi nikiwa napita sokoni nilinunua nazi ili niende nyumbani nikazile kimasikhara ila zilitia huruma mpaka nimeirudisha sokoni wanibadilishie. Kusema ukweli nilishindwa kuila Kimasikhara kabisa yani... (Sitanii kabisa)
View attachment 1368492
View attachment 1368493
Aisee ni halali kabsa kuzirudsha sokoni

yess BiShoo haswaaAaa
 
Komamanga nalo huliwa kimasihara likiwa limekomaa hupasuka lenyewe kisha ndani limepangika mithili ya punje za mahindi zikiwekwa kwenye kopo kwa kushindiliwa basi ndio hivyo unazichukua na kuzirushia mdomoni moja moja kama unakula karanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boga ni mboga tamu sana wataalamu wa upishi huwa wanalipika kwa nazi ila kuna wengine wanalila kwa kuchemshwa tu hawataki mambo mengi. Wajuvi huwa wanakula boga wanakula mpaka majani yake haliachwi kitu. Likiwa limepikwa unaweza lila kwa kijiko au mikono, raha ulile taratibu..
maxresdefault.jpg



Ila mtu akikwambia unaliwa KIBOGA lazima urushe ngumi, ulaji wa boga ni wa masikhara na hakuna anayependa kuliwa kimasikhara..
 
Bamia ni mboga inayotengenezwa kwenye mapishi mengi sana, kitaalamu wengi wanapenda kuzipika mfano kama mlenda, kwenye mchuzi nk. Wajuvi wao hula bamia mbichi kabisa wanadai ni dawa ya kisukari, mara vidonda vya tumbo na magonjwa mengi tu. Raha ya bamia anajua mlaji wake huwezi kuielezea
IMG-20170926-WA0002.jpg


Hata uwe mpenzi laji wa bamia vipi, ukiambiwa una KIBAMIA, lazima unune...
 
Back
Top Bottom