Tunda na ganda

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2008
Posts
777
Reaction score
50
Kuna bwana mmoja alikwenda kwa daktari akisumbuliwa na ugonjwa wa ngozi,baada ya maongezi ya muda mrefu kidogo,daktari akashauri

Daktari,"Itabidi uwe na tabia ya kula matunda na maganda yake,itakusaidia sana kuondoa tatizo lako."

Mgonjwa," Mmmmmmmhhh"

Daktari," Mbona unaguna"

Mgonjwa,"Hiyo itakuwa ngumu"

Daktari,"Kwani wewe unapendelea tunda gani"

Mgonjwa,"DAFU"
 
hiyo lazima iwe ngumu, mshikaji ni wa mitaa ya pwani nini?
 
Teh teh kazi kweli kweli. Nanasi je linaweza kuliwa na maganda yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…