Tunda sikupata ila na yeye nilimkomesha

Jacaranda

Member
Joined
Oct 23, 2011
Posts
45
Reaction score
20
Alisisimama mbele yangu huku umbo lake likionekana vizuri kwenye nightdress yake ya pink,akawasha taa ya rangi ya bluu. Akapanda kitandani na kuanza kunipapasa kifuani kisha akaanza kuushusha mkono wake taratibu kuelekea mapajani mwangu.mshawasha wa mapenzi ukanijaa na kunifanya nihisi kama miguu yangu imekufa ngazi.Nikamgeuza na kumuweka chini yangu. Ghafla nikasikia "Jac nilikuwa nataka unikumbatie tu mpaka asubuhi" nikaguna kwa sauti huku nimetoa macho "Inaonekana huna mapenzi kwangu, unachojali ni mimi kukutimizia tu haja zako za kimwili" wakati bado nashangaa akaongezea "hivi kwa nin usinipende jinsi nilivyo na si kwa kile nachokufanyia kitandani?" nilipomtazama usoni nikagundua yuko serious na kwa usiku huo tunda sipati.Nikageukia ukutani na kusinzia

Wiki moja ilipopita nikamtoa out kwenye hotel moja kubwa hapa dar tukapata chakula cha mchana ambacho kilikuwa expensive na kisha tukaaelekea mliman city na kuingia moja kwa moja kwenye duka la nguo za kike.Akajaribu gauni kadhaa ambazo zilimpendeza sana kisha akaelekea kwenye viatu akatafuta viatu ambavyo vitamachi na gauni moja,nikamwambia usiwe na shida tutanunua vyote akajibu lakini swity ni expensive sana hacha nichague gaun moja na viatu vitakavyoendana navyo nikamjibu chukua vyote usiwe na hofu.mmm mara akaelekea kwenye mikufu akachagua mkufu wa dhahabu akauvaa akaniambia "vipi baby hapa nimependeza" nikamjibu yap chukua na huo pia.Waoo alifurahi natamani ungemuona.duu mara akelekea kwenye bikini,akachagua bikini na bra yake vyote vya rangi nyekundu vyenye bei ya laki mbili nikamwambia nahivyo dia weka tu usiwe na hofu.Alikenua meno wewe utafikilia ameshinda bahat nasibu ya sh million 500, aise nataman ungemuona.,nahisi moyoni alikuwa anawaza kweli nimepata buzi.

Alipomaliza akaniambia "Vimetosha baby twende tukalipe" Nimkajibu taratibu kwa sauti ya kistarabu "Baby nilikuwa nataka uvishike tu mikononi kwa muda" akatabasamu huku akiniiambia "ila na wewe baby unavimisemo" nikaendelea "Inaonekana huna mapenzi kwangu,unachojali ni mimi kukutimizia haja zako za shopping tu" akanitazama kwa macho yaliyojaa hasira,nahisi angekuwa na bunduki ningekuwa maiti kwa sasa. Kwa pozi lilelile nikaendelea "hivi kwa nini usinipende jinsi nilivyo na si kwa pesa zangu zinachokufanyia"

Sikijua aliondokaje mle dukani lakini vitu vyote alivyokuwa amevibeba nilishangaa viko sakafuni.Natokea siku hiyo sjamuona tena,Tunda sikupata ila na yeye nilimkomesha.am smart than her aaaaaaah
 
Mlimani city hakuna duka linalouza bra na matching (bikini?) kwa tshs 200,000, ama mlikuwa zimbabwe?
Ukitunga story tumia mandhari uliyozoea ili isiwe too fictious.
Hongera kwa kumkomoa.
Dah! niko usingizini nikaota King'asti anaposti, kumbe anaposti kweli bana. Aleluyah
 
Last edited by a moderator:
Mi naomba tuondoke na mlinzi, kazi za uhaousigelo tumlipe kama overtime and any other assigned duties. Hii one night stand ya wiki moja itakuwa safi sana, staki kukosana na mkeo SL
Nimelipia tatu, tunaondoka na hauzigeli wetu manake naskia madagascar hauzigeli ni bei mbaya sana.
 
Mi naomba tuondoke na mlinzi, kazi za uhaousigelo tumlipe kama overtime and any other assigned duties. Hii one night stand ya wiki moja itakuwa safi sana, staki kukosana na mkeo SL
huyo SL wala asikushtue , hapa nakuchukua wewe ili kulipiza kisasi, alimwaga vegetable mimi namwaga ugali. tena ukuje na kamera ya kuazima ili tumjump roho yake kwa mafoto.
 
Kila foto utakayokuwa na mie utailipia, nitaangalia rates za maselebriti wa bongo. Camera utaninunulia huko huko, na nguo sibebi kabisa. SL namuogopa ni mke mwenzangu asije akaniharibia kijiwe changu cha town aisee!
huyo SL wala asikushtue , hapa nakuchukua wewe ili kulipiza kisasi, alimwaga vegetable mimi namwaga ugali. tena ukuje na kamera ya kuazima ili tumjump roho yake kwa mafoto.
 

Good story....

usiache uandishi.... Ila mshkaji noma kweli, yani kukugusa tu, basi tayari ushamweka chini?? duh:frog:
 
Mlimani city kuna duka la nguo na dhahabu?

Peleka hii kwenye FB.
 
Hata kama ni uongo lakini ina mafunzo fulani ya ukweli ndani yake. Wanawake wengi ndivyo walivyo, ukiuza cheni bandia nami nakupa mihela feki ngoma droo mpaka mechi nyingine.
 
story umeisoma kwenye kitabu cha THINK BIG umeibadilisha kwa kiswahili ndo umekuja kutuwekea hapa, acha fix.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…