Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amepewa adhabu na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ya kutofanya kampeni kwa siku 7 halafu anajirekodi malalamiko yake kwa kiingereza

Watanzania wanajua Lisu hajatumwa na mtu wanajua bila ccm kumpiga risasi asingefika ulaya wanajua unyama wa ccm ndiyo umempa Tundu lisu umaarufu, hawatambui kinachoendelea kwa magufuli zaidi ya kujua kuwa kuna ufisadi mkubwa ndiyo maana wakakosa pesa za nyongeza za mishahara kwa miaka mitano huku pesa zingine zikitumika kumrejesha ikulu kwa nguvu pasipo ridhaa ya wananchi.
 

Ushauri tu.

Kuweni makini, msije mkawatesa hata wale wasio husika.
Hii nchi ni nchi huru kisiasa.
 
ccm wao wapo juu ya Sheria juzi IGP kasema hakuna aliye juu ya Sheria lakini Polisi wake wamevunja Sheria kuwapiga mabomu wananchi pasipo kuchuliwa hatua yeyote, ccm wapo juu ya Sheria hata Tume yao ya uchaguzi haithubutu kuwagusa imeamua kuwaonea chadema pekee alafu eti hawataki wapinzani waongee hata kingereza? maccm mna nini? acheni Roho mbaya zitawafikisha wapi?
 
Ushauri tu.

Kuweni makini, msije mkawatesa hata wale wasio husika.
Hii nchi ni nchi huru kisiasa.
ccm ndiyo inawatesa wananchi hakuna uhuru Tanzania kuna Mkoloni kaburu mweusi, Uhuru utakuja tarehe 28 October pindi Tundu akiapishwa kuwa Rais wa Tanzania
 
CCM wamejaza mabango peke yao nchi nzima ,wanajisifu wamefanya mambo makubwa sana lakini wana mgombea weak vibaya mno hawezi kufanya kampeni mfululizo for 7 days mmebaki kutumia polisi na NEC kumdhibiti Lissu Muda wa kukataliwa duniani na mbinguni umeshafika kwa Meko.
 
Nenda anakoishi Amsterdam akakuongoze wewe na familia yako sisi watz utuachie JPM wetu, msituletee huu ujinga wenu hapa nchini.
Ujinga upi mkuu,kuingia mikataba na mabeberu kisha kuificha,au kushindwa kusafiri kwenda kutimiza majukumu yako because of your incompetence ndo ujinga unaozungumzia hapa? Kukimbia shule kwako isiwe sababu ya kudhani watanzania wote tu washamba na mapoyoyo kama ninyi
 


Maneno chungu nzima yaliyo sheheni horror stories tu kuwafanya Watanzania hawana akili ya ku-analyse mambo wakiwa level headed bila ya mihemuko ya kijinga - mambo mengi anayo zungumza humu ni kutunga tu yenye lengo la kuleta taharuki tu. Eti Lissu anazungumza kiingereza kimakusudi ili kunufahisha wageni - uongo mtupu yaani hata hujui kwamba hata angezungumza kiswahili Google translator inaweza kutafsiri kwa kiingereza bila ya matatizo yoyote - mambo nengine yana shangaza sana, hapa unajaribu kumkandia Lissu by hooks and crooks umesahau kwamba alidhinishwa na NEC kugombea Urais baada ya kukidhi vigezo kama washindani wenzake LEO hii unatuketea adidhi za kutunga tu as if NEC ilifanya makosa kumpitisha Lissu - akili gani hizi, nyie ndio mnataka kutuletea balaa kwenye Taifa letu - FYI mimi ni mwanachama ahi wa CCM lakini siwezi kuhunga mkono propaganda za kutaka kuvuruga Taifa letu, kama hatutaki vyama vya upinzani kwenye Taifa letu,Basi itangazie Dunia tujuwe moja - hacheni mambo ya kujipendekeza.
 
Mleta mada hutaeleweka...kiuhalisia watanzania wameichoka ccm, sio kwamba wanampenda sana Lissu au kumchukia sana Magufuli. Tatizo hapa ni CCM.

Kwenye hali hii ukileta hoja yoyote kinzani unaweza kupigwa mawe!
Huo ndio ukweli.

Ndio maana Lissu akiwa Rais halafu naye akaleta usenge tutamtaka apishe kiti kwa mwingine
 
Kusafiri kwenda kutimiza majukumu?
Wapi huko?

Ndio nyie mlileta ujinga wakati wa corona eti hoo haongei na wenzie, hafuati kanuni za mabeberu za kujikinga na covid

Haya hao walikuwa wanaongea na kufuata kanuni za mabeberu wamefikia wapi?


Sikiliza bwana mdogo, uongozi ni pamoja na kujiamini na kufanya kile unachokiamini kina manufaa kwako na kwa wananchi wako siyo huyo kiraka wenu amaesema hatuwezi kuishi bila wazungu.
Nwambieni awachukue nyie mashabiki wake wote nendeni nae mkaishi huko kwa mabwana zenu.
 
ccm wengi wana machungu mno, mfano wafanyabiashara wakubwa wameporwa pesa mali zao kwa kubambikiwa bill kubwa zisizoelewa na TRA huku Sheria mbovu mbaya ikitumika vibaya kuwakomoa kuwatisha wafanyabiashara ambao wengi ni wanaccm, kenya Uganda wao wanaendelea vizuri akiba ya pesa za kigeni dola ipo vizuri hawana vikwazo kwa yeyote kutuma pesa tokea nje kuja kwao wawekezaji wapo huru, lakini Tanzania hata kutumiwa Dola 5000 tu imekuwa shida wakati hizo pesa zingeweza kuja kutumika Tanzania zikaleta maendeleo, watanzania wanaenda kuwekeza Zambia Malawi msumbiji Rwanda Burundi congo kusiko na ujinga wa kusumbua watu pindi wakitumiwa pesa tokea nje ya Nchi.
 
Wewe nenda kaishi na mabwana zako chato na Rwanda acheni wapenda mageuzi wajiamlie acheni watumie ridhaa yao kuchagua acheni kuwachagulia ccm kwa kumtumia IGP na Tume isiyo huru ya ccm, toeni uhuru, wananchi wanataka uhuru tokea kwenu makaburu weusi
 
Aandike tu lugha yoyote wanayoweza kuelewa huko nje ili hawa wakoloni weusi wakileta ujinga na sisi tuwekewe vikwazo ili akili iturudie.
 
Wewe kafiri wa ccm acha upumbavu wako.
 
Aandike tu lugha yoyote wanayoweza kuelewa huko nje ili hawa wakoloni weusi wakileta ujinga na sisi tuwekewe vikwazo ili akili iturudie.
Mkoloni mweusi hataki hata wenzake ccm watumiwe pesa toka nje ana wivu balaa ukitumiwa pesa nyingi tokea Ulaya anatumia BOT kuzipora kwa vitisho kuwa utabambikiwa kesi ya uhujumu uchumi na kibaya zaidi pesa zote wanazichukua wao binafsi, ukoloni wa ccm umewaumiza wengi wana machungu makubwa dhidi ya utawala huu wa kidikteta
 
Aahhh kumamake...andiko kama Gazeti

Alafu msingi ni Lissu kuandika kingereza.


Kwaiyo Mkutano na waandishi wake habari aliufanya kisukuma???



Weee Mzeee makalio yako.
 
Pole sana. Umemeza dawa za pressure? Naona unaandika tu. Watu wenye maoni kama yako walieleweka sana Kipindi kile marais waumini wa demokrasia wakiwa ikulu.
Sasa hivi hata yule taahira anajua hakuna demokrasia, hakuna haki, ushamba umekithiri vitisho kilakona. Rais anadiriki kusema ukichagua mpinzani sileti huduma za maendeleo. Bado unatetea tu.
Kipindi ambacho marais wanaoheshimu kanuni za Tume kama vile kutokutoa rushwa Kipindi cha kampeni, kauli za Lisu kuomba msaada kwa wazungu zingekuwa si za kizalendo. Lakini kwa Rais anayetoa rushwa kila jina ya nchi hii wazi wazi, Kilia cha Lisu kwa wazungu ni halali na tukiongezee mwangwi kisikikke mbali ili tupate msaada kwa haraka.
Kama huna taarifa rais dhahiri alitoa rushwa kigoma tsh bilioni tano Ujenzi wa Barabara. Sasa hivi vijijini mbolea inatolewa bure kwa wakulima mpaka wanaogopa. Zoezi lilizinduliwa na Bashe akishirikiana na kampuni ya Yara kati ya rukwa au tabora. Hiyo ni mifano michache tu ya rushwa.
Sidhani kama huu uonezi wewe huuoni. Najua unauona uwenda hujajaaliwa moyo wa kuubeba uchungu wa wanaodhulumiwa na kuonewa na kuubeba uchungu wao. Tunakipenda chama chetu lakini si kwa dhuruma hizi. Watu wanaona kila taasisi ya umma inashindana kumgandamiza Lisu mpaka wanagongana. Hii ni aibu.
Tatiza ya maendeleo ya vitu ni vyenyewe kutokusema ni mpaka uvisemee. Sasa wananchi wa kuyasemea hayo mavitu ndio walionyang'anywa hela wakiitwa ni mafisadi. Wafanyakazi hakuna nyongeza ya mshahara miaka mitano,zuia Kulipa baadhi ya watumishi Umeme na maji kwa miaka mitano, wengine kujilipia mafunzo. Nani wa kuyasemea mavitu katika hali hiyo. Basi angekuwa anatutaja ushiriki wa wafanyakazi katika hayo mafanikio. Hujisifu peke yake bila mimi bila mimi.
Tumsaidie anayeonewa kufikisha kilio sehemu mbalimbali ulimwenguni ili apate msaada.
 
Kwani shida nini? Kwani Ukisikia mtu anaongea kiingereza huwa unapandisha mashetani?
Issue ni kwa kuelewa walengwa wa ujumbe wake huo. Kama analenga ujumbe uwafikie watanzania, atatumiaje kiingereza badala ya kiswahili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…