Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
MGOMBEA WA CHADEMA MH TUNDU ANTIPAS LISU, KAMA HAELEWI!
Na Elius Ndabila
0768239284
Leo nikiwa napitia mitandaoni nimekutana na Twitter ya Mh Lissu ambayo imepambwa na Picha ya Mh Rais Dkt Magufuli na Naibu Spika Mh Dkt Tulia Ackson. Kwenye twitter hii Mh Lisu ameandika maneno haya "Hii ni rushwa ya uchaguzi, tendo lililokatazwa chini ya sheria ya uchaguzi. Popote atakapogombea awekewe pingamizi na wagombea wetu ili aenguliwe kwa mjibu wa sheria. Watao rushwa hawa wafuatiliwe kila mahali waliko na kuwekewa mapingamizi ili uteuzi wao utenguliwe" mwisho wa kunukuu.
Ninaamini Mh Lissu kwa kuwa ni member wa JF atasoma andiko hili. Kwanza Mh Lissu aache kuwapotosha wanachama wa CDM kwa kitu ambacho anajua hakina uhalali wa kisheria. Ninaomba nimkumbushe Mh Lissu kuwa hadi sasa CCM haina wagombea wa Udiwani wala Ubunge, CCM hadi sasa inamgombea Urais tu ambaye ni Mh JPM (bulldozer). Kipindi cha uchaguzi hakizuiliwi watu kufanya kazi za maendeleo, sheria inakataza kufanya kazi za maendeleo ambazo zinaweza kutafsiriwa Kama Rushwa endapo tu utakuwa umeshapewa ridhaa ya kugombea.
Mh Tulia hadi sasa siyo mgombea na hajatangazwa na CCM kuwa ni mgombea popote. Hata hivyo dhana ya mtu kuitwa mgombea ni hadi tume ya uchaguzi imtangaze mtu kuwa ni mgombea. Kwa Katibu ya CCM BADO Mh Tulia ni mtia nia na si mgombea. Michakato ya utia nia husimamiwa na chama na situme kama unavyotaka kuwaaminisha watu. Labda Mh Lissu uniambie lini CCM imetangaza Wagombea wake? Ninadhani andiko langu fupi litawaongezea tafakuri juu ya uelewa wa maswala haya.