Pre GE2025 Tundu Lissu endelea kugawa Ulichonacho (Elimu ya Katiba) na uache kulalamika juu ya vinavyotolewa na wengine

Pre GE2025 Tundu Lissu endelea kugawa Ulichonacho (Elimu ya Katiba) na uache kulalamika juu ya vinavyotolewa na wengine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Maandiko yanasema Wana wa ngurumo Petro, Yakobo na Yohana hawakuwa na Fedha bali walichokuwa nacho ni "Kumpa yule Mlemavu wa Miguu Kutembea".

Yule mlemavu alikaa pale akiamini Fedha (Madera na tukutuku) ndio uponyaji wake lakini Wana wa Ngurumo wakampa Kutembea (Elimu) naye akasimama na kwenda zake kuyafurahia maisha

Tumemuona Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu akigawa madera kwa wapigakura wake wanyonge akiamini anawasaidia.

Wewe Tundu Antipas Lissu endelea kuwalisha Wapigakura Elimu ya Katiba lakini bila kulalamika wala kukejeli na kushambulia mtu yoyote.

Mavuno ni mengi Watenda Kazi wachache.

Mungu wa mbinguni aibariki Jumatatu Yako. 😄😄
 
Neno analolitoa ni kubwa na lathamani kuliko sadaka za matajiri hekaluni pa Bwana
 
vijana tunaelewa sana anachoongea Tundulisu ni suala la muda tu mbegu huanza kumea taratibu na baadae kuwa mti wenye kivuli. Sauti yake inaeleweka Sana mtaani
 
Maandiko yanasema Wana wa ngurumo Petro, Yakobo na Yohana hawakuwa na Fedha bali walichokuwa nacho ni " kumpa yule Mlemavu wa Miguu Kutembea"

Yule mlemavu alikaa pale akiamini Fedha (Madera na tukutuku) ndio uponyaji wake lakini Wana wa Ngurumo wakampa Kutembea ( Elimu) naye akasimama na kwenda zake kuyafurahia maisha

Tumemuona mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa mh Joseph Mbilinyi aka Sugu akigawa Madera kwa Wapigakura wake Wanyonge akiamini anawasaidia

Wewe Tundu Antipas Lisu endelea kuwalisha Wapigakura Elimu ya Katiba lakini bila kulalamika wala kukejeli na kushambulia mtu yoyote

Mavuno ni mengi Watenda Kazi wachache

Mungu wa mbinguni aibariki Jumatatu Yako 😄😄
Mama Abdul anagawa tukutuku 18,000 nchi nzima kwa ajili ya kampeni kutoka UAE hizo hela amezipata wapi?
 
Laigwanaan Lissu hatowahi kuwa Raisi wa Tanzania.

Ni kwasababu hivi sasa anaonekana kuwa anapata viwewe, anaweweseka, ana woga na wasiwasi saa zote. Yaani anaoyesha dalili zote za kuwa na PTSD. Usiombee mtu yeyote yule apitie aliyoyapitia Lissu.

Na hiyo inatokana kuwa Lissu ni mhanga wa kupigwa risasi kwa kujitoa mhanga ili mazingira ya Usalama wa wafanyasiasa utiliwe mashaka na hatimaye Nchi ionekane haina Usalama.

Hata atoe elimu gani, ama adanganye vipi, au afoke, atukane, adhalilishe, asambaratishe pamoja na kujikosha kutaka apewe kura za Huruma, hatokuja kuwa Raisi wa Nchi hii.
 
Back
Top Bottom