Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hana sifa za kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama

Hana busara, ila wengi watakupinga kwa mada hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aacha uoga,mpaka Hapo unaonekana unaemsema ni mkuu jiwe a.k.a malaika mkuu,kwa sifa hizo zote anazo ambaye hashauriwi,hakosolewi wala hajaribiwi.JIWE
 

Kwa marais wa sasa walio madarakani mtu yeyote anaweza kuwa rais., Lissu akipata hiyo fursa kwa mara ya kwanza Tz itakuwa imeandika historia kupata rais makini na msomi anayejua wananchi wake wanataka nini
 
Kwa marais wa sasa walio madarakani mtu yeyote anaweza kuwa rais., Lissu akipata hiyo fursa kwa mara ya kwanza Tz itakuwa imeandika historia kupata rais makini na msomi anayejua wananchi wake wanataka nini
sidhani kama anatosha ktk hicho kiti
 
hata kama unajua mambo mambo kitaaluma hutakiwi kuonyesha dharau kwa wenzako.......'wewe mwanasheria wa wapi' hizo ni dharau kwa mwanataaaluma mwenzako
Je aliyesema “unanijibu hivyo mimi” yule mkrugenzi ni Lissu je aliongea kwa misingi gani?
 
Superiority complex inamsumbua. Aliwahi kuwatusi wabunge wa CUF kipindi cha nyuma, sababu ni ule wingi wa wabunge wa CHADEMA, akawaambia wanaume ndio wanaowafuata wanawake na sio wanawake kuwafuata wanaume.

Mdomo huponza kichwa, maneno ya wahenga.
 
Lissu anajisikia sana, mtazame anavyoing'ata midomo yake wakati akiongea, ndio utajua ni mjivuni kiasi gani.
 
Tatizo upinzani wa Tz unatuzingua kwa sababu huwa hawamuandai mgombea wa raisi badala yake huwa wanamuandaa siku hiyo hiyo ya uchaguzi hapo ndo napowaona wanapwaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upinzani wa nchi hii huwa haukomai kisiasa, muda huu wanamjadili Lissu wakati watu makini hivi sasa wanatimiza ahadi za mwaka 2015, wakizinduka mwaka 2020 na wakashindwa uchaguzi watadai wameibiwa kura.
 
Pepo la ccm linakutesa utanyoka
 
Kwa hiyo wenye sifa kwa mtazamo wako wewe ni wale wajinga kama nduguyo wa sasa, au vipi?
 
Naona Lissu kamwaga mafuta kwenye shimo lenye manyoka waliozaliana miaka mingia sasa yanaangaika kutoka shimoni ya nashindwa
Mkuu tatizo lako wewe hujui kutofautisha kati ya kauli za Rais wako to be Tundu Lissu akiwa Tanzania kwenye jukwaa la kitaifa la watanzania na zile anazo zifanya akiwa katika majukwa ya kimataifa. Huyu jamaa amefeli kote kote. Hivi wewe huoni kama yeye anatuumbua sisi kama Balozi wetu nchini Amerika Dr. Masilingi alivyo mwambia? Naomba angalia hii Clip mwishoni mwishoni.
Kwenye majukwaa kama hayo watu wengi wenye busara na upendo kwa nchi zao na uzalendo, wanayatumia kupigia debe nchi zao ili; moja tupate watalii wengi kama nchi ina vivutio vizuri vya kiutalii, mbili kuwavutia wateja kuja kuwekeza nchini ili kijana kama wewe na kizazi chako baadae wapate ajira na kukuwezesha kuwa na maisha bora na ya amani na utulivu.

Naomba utambue pia kuwa Tundu Lissu hana udiplomasia hata mmoja. Lugha yake anayo tumia kwanza ni chafu na yenye chuki na pili ni kama ya mtu ambaye yuko katika mkutano au darasa wakati yale yalikuwa mazungumzo ya kawaida ya kisiasa kuelezea tofauti zao. Lakini yeye anatumia lugha ya defamation. Ulaya kufanya hivyo ni offend. Unapaswa kushtakiwa!

Ebu jaribu kusikiliza Bobi Wine mpinzani wa Uganda kwenye hii Clip anavyo jua kuji-articulate, utafikiri kuwa yeye ni msomi kuliko Lissu, wakati yeye ni msanii tu wa music. Na ukiangalia Uganda chini ya Rais Museven wana matatizo makubwa zaidi kuliko sisi, lakini sijamsikia akitoa kauli za ukali na matusi au kejili aidha kwa Rais wake au kwa nchi yake. Na kiingereza chake ni excellent kuliko hata ambacho Lissu anakivunia na kumpa kuchwa na kiburi cha kumsakama Rais wetu.
Ni haibu kubwa sana kuona msomi wetu Tundu Lissu anapayuka mambo ambayo ni ya uongo na asiyo yajua. Wewe unamwona yeye anafaa kuwa kiongozi wa nchi? Jamaa mwinye tabia hiyo?

Ni haibu kubwa sana kwa Taifa letu na sielewi wewe unaupata wapi ushujaa wa kumshabikia jamaa ambaye anakuchimbia kaburi lako ili uzikwe.

Kama unajua vizuri maana ya "Body Language" naomba mwangalie Lissu kwenye Clip hii ambako yuko kwenye huo mkutano na hao wanfunzi na hizo Clip nyingine mbili Balozi Masingili akiwepo. Halafu angalia pia Boss alanguage ya huyo Mama ambaye anaendesha huo mkutano.
Kwenye hii clip utamwona Lissu anavyo jisikia raha na amani ya kupata jukwaa lake peke yake ili atoe uongo wake usio na miguu wala kichwa bila kubughuziwa na mtu mwingine. Huyo mama ambaye anaongoza huo mjadala unamwona jinsi alivyo kuwa uncomfortable na kauli za bwana Lissu? Anamshangaa mwana siasa maarufu wenyewe wanavyo dai anavyo kuja kutoa uozo kuhusu nchi yake na Rais wake. Nina uhakika 100% anajua kila kitu kuhusu Tanzania na anajua kuwa Rais Magufuli ana enjoy overwhelming popularity. Statistics za dunia zinaonyesha hivyo, lakini yeye mkoma wetu anamaanisha sio. Sijui hasikilizi media nyingine zinavyo sema?

Kwenye hizo Clips nyingine unamwona jinsi gani Lissu amekuwa stressed kwa vile Bolozi yuko na ambaye ata mchallenge.

Swala jingine ambalo ningependa utambue ni kwamba, sisi tuna mgogoro mkubwa sana na jumuia ya Ulaya. Jumuia ya Ulaya ilitaka watulazimishe sisi wana East African Community tukubali mkataba wao wa EPA. Sisi watanzania kwa juhudi za wanasheria wetu hasa
Pro. Paramagamba Kabudi ambaye mimi "I am so proud of" baada ya kuuchambua huo mkataba wakaona dosari zilizopo na kuiomba serikali yetu ikatae huo mkataba mpaka hapo utakapo rekebishwa kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mkataba wa EPA ni mkataba wa kitapeli - JamiiForums
Nakueleza haya kijana wangu ili utambue kuwa ulimwengu sio mzuri kama wewe na Rais wako to be Tundu Lissu mnafikiri ulivyo. Ulimwengu una sura mbaya sana katika maswala ya kiuchumi. Wazungu wanataka East Africa iwe Damp ya products zao ambazo kwao hawazitaki ili watuuzie sisi na ikibidi watupe kwa mikopo ambayo wewe na mimi na vizazi vyetu hatutakuwa na uwezo kamwe kukipa. Mbali na hayo kuharibu sera yetu ya kuitaka Tanzania kuwa nchi ya viwanda au kuwa katika uchumi wa kati.

Jamaa yako inaniwia vigumu kumwelewa anataka nini? Ana wajazia wazungu mambo ya uongo tu, lakini yale mazuri hayaoni na hataki kuyaona mpaka anawekwa chini na Balozi wetu wa Amerika Dr Masilingi kama mtoto mdogo?Aisee huyu ni msomi wa ajabu sana.
Hii inaonyesha kuwa ni kiasi gani Tundu Lissu ni Psychopathic kama alivyo kuwa "Napoleon Bona Pat"

Kwanza Interpretation yake ya sheria na katiba inanitia mashaka sembuse uwezo wake wa kutambua nini maana ya haki za binadam na Freedom of press? Hii ni hatari sana kuwa na mtu wa aina hii kama kiongozi wa nchi hasa nchi kama Tanzania ambayo nchi nyingi za kusini mwa Afrika zina itegemea!

Clip hizo mbili hapo chini zina mwonyesha RC wetu wa jiji letu la Dar es salaam Paul Makonda katika harakati zake za kwenda kuwaonyesha wasanii wetu mbali mbali na wasio wasanii na waandishi wa habari maendelezo ya mradi wetu mkubwa Tanzania wa Std Gauge. Lini ilisha wahi kutokea hivyo katika historia ya Tanzania?
Hii inatokea baada ya Rais wetu mpendwa Mh. John Joseph Pombe Magufuli kutambua umuhimu wa kuwatumia vijana wetu wa Tanzanin katika positions mbali mbali ili kutumua nguvu zao na maarifa yao kulijenga Taifa lao la sasa na la baadae kwa manufaa ya watanzania wote ambao ni tanzania. Kumpongeza sana Rais wetu kwa jambo hili.

Kwa kumalizia nakuomba kijana hamka utoe mchango wako wa kulijenga taifa lenu usiwangojee vidamp kama akina Lissu ndiyo wakuletee mafanikio unayo yataka. Hakuna kitu kama hicho! Sahau!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mh. Ki ukweli hafai kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Kwa maoni yangu, nadhani anafaa kuwa Waziri Mkuu. Hata hivyo atatakiwa kwanza kupata Course Maalumu ya Uzalendo, Staha na Heshima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo aliekalia kiti mbona haujatupa nidhamu yake tuijue?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je unalijua jiwe jinsi lina dharau? Au umelifanya kuwa jiwe walolikataa waashi na sasa limekuwa jiwe kuu la pembeni
 
Masikio yote ni kwa Lissu ndio habari ya mjini haya maigizo yenu peleka huko ujinga mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…