Amani iwe nanyi.
Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu, ukiacha Mgombea Urais wa CCM rais Magufuli anayetetea nafasi yake ananadi vizuri ilani ya chama chake, Wagombea wa vyama vingine hata ilani ya chama hawana!!
Mfano mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lisu ameonekana mara kadhaa kwenye majukwaa ya kampeni akijaribu kuwafundisha watanzania kuhusu rais Magufuli alivyo! Yani Lisu badala ya kunadi ilani na Sera ya chama chake anatumia muda wote wa kampeni akitaja jina la Magufuli! Hivi Magufuli ndiyo ilani ya chadema?
Nikuambie tu Tundu Lisu, sisi watanzania huna cha kutufundisha kuhusu rais Magufuli.
1. Magufuli ametutumikia akiwa waziri kwa miaka 20 tangu enzi hizo kwenda Mtwara unatumia siku mbili kwenye meli, mpaka enzi hizi ambazo Mtwara unatumia masaa sita tu kufika ukiteleza kwenye lami, mjenzi wa mabarabara yote hayo ni Magufuli ,hivyo tunamjua huna cha kutufundisha.
2. Magufuli tulimchagua sisi wenyewe October 2015 tukiwa tunamjua na tumehangaika kwa miaka 5 akikomesha rushwa ufisadi,elimu bure, flyover na akirejesha nidhamu serikalini. Wewe Lissu ndiyo uje kutufundisha leo kuhusu Magufuli?
3. Tundu Lisu ulituambia tukibadili sheria za madini tutashitakiwa MIGA tukuulize je tumeshitakiwa MIGA?
Umekuwa mbunge kule Singida kwa miaka 10 je una lipi la kukumbukwa na wananchi wa jimbo lako?
Lisu umekuwa rais wa TLS je una lipi la kukumbukwa hapo?
Kwa ufupi sisi wananchi tunatakiwa tufundishwe kuhusu wewe Lisu ni mtu wa namna gani kwa sababu huna kitu cha kuonekana ulichowafanyia wananchi zaidi ya makelele na kutukana serikali.
Tundu Lisu wewe siyo mzalendo wa nchi yetu hivyo hufai kuwa rais na hutakaa uwe rais wa Tanzania na tarehe 28 October tutakupa fundisho kali la kwamba watanzania siyo wajinga wa kuchagua mtu yoyote hata mtetezi wa mabeberu.
Mimi natofautina sana na hoja yako nimesoma ilani ya CCM na nimesoma ilani ya CDM kwa kifupi ilani ya CCM ni ile ile ya kufikiria serikali italeta maendeleo katika hii nchi. Ilani yote imejaa serikali itajenga shule, itajenga hospital, itajenga barabara itajenga reli itajenga viwanja vya michezo itajenga bwawa la Umeme na kadhalika.
Lakini haisemi baada ya kuwa na ilani za kufanya vitu hivyo zaidi ya miaka 50 inakuwaje wananchi bado wanaendelea kuwa masikini wanakabiliwa na maradhi pamoja na ujinga. Kimsingi hakuna kimya katika hiyo ilani. Haisemi ni namna gani wananchi wanaweza kujipatia maendeleo yao.
Ukisoma ilani ya CDM kwa kiasi kikubwa inazungumzia mambo mapya yanayoweza kuleta mabadiliko kwa mwananchi, kwanza inazungumzia ugatuzi wa madaraka jambo ambalo litasaidia kuondoa ufisaji wa rasilimali za nchi.
Pili inaongelea sekta binafsi kwasababu hiyo ndiyo njia pekee ya kumsaidia mwananchi mmoja mmoja kwasababu sekta binafsi ndiyo inayoajiri watanzania wengi kuwa na sera ya kukuza sekta binafsi ni sawa na kuwa na sera ya kuwaendeleza wananchi moja kwa moja badala ya kuwa ombaomba kwa serikali.
Wanazungumzia kodi, kila mtu anaona biashara nyingi zinakufa sababu ya kodi kubwa ni vema kuangalia kodi itozwe kiasi gani ili kuweza kukuza biashara na hivyo kuwa na wito mkubwa zaidi wa kupata kodi kuliko utitiri wa kodi ambayo matokeo yake ni kuua biashara na kusababisha hali ya umasikini zaidi kwa watanzania walio wengi.
Tatu CDM inazungumzia uhuru wa wananchi kufanya shuguli zao na kuuza mazao yao popote wanaopona pana Soko zuri badala ya serikali kuwapangia na hivyo kulazimika kuuza mazao ya kwa hasara na hivyo kuzidi kuwa masikini.
Nne CDM inazungumzia kumjali mfanyakazi kwa kumalipa vizuri pamoja na kuwalipa wastaafu malipo Haya yanapofanyika yanasababisha kuleta nafuu ya maisha kwa wafanyakazi, wastaafu pamoja na wategemezi wao. Lakini pia wanapozungumzia wakulima kuruhusiwa kuuza mazao yao popote penye soko zuri pamoja na kupunguza utitiri wa kodi wanalenga kutatua kilio kikubwa cha watu kuwa na maisha magumu wakati nchi yetu ni tajiri sana.
Kwa ujumla sera ya CCM ni kuendeleza Uchumi dola ambao haujawahi kumnufaisha mwananchi wa kawaida na badala yake sera hiyo ilijaribiwa na awamu yankwanza ikashindwa.
Sera ya CDM ni ya ugatuzi wa madaraka pamoja kushirikisha sekta bianfsi katika miradi ya maendeleo ambayo ni nzuri inafanya miradi mingi itekelezwe kwa ufanisi bila nchi kuingia kwenye madeni makubwa na hivyo kutumia sehemu kubwa ya mapato yake kulipia deni.
Kwakweli kwa vyovyote vile ili wananchi waweze kupata maendeleo yao hatuwezi kuendelea na sera zile zile miaka nenda rudi ipo haja ya kuangalia upya nini kifanyike jambo ambalo CCM haijafanya imebakia na mazoea ambayo hayawezi kutuletea mabadiliko tunayohitaji.