Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, ameendelea kuzungumzia changamoto za mfumo wa uchaguzi nchini, akisema kuwa kura ya mtu mmoja lazima iwe sawa na kura ya mtu mwingine popote ndani ya nchi. Lissu alitoa mifano akisema, "Kama ni kuchagua mbunge, uwe na uwezo wa kuchagua mbunge wa aina moja." Aliongeza kuwa, kwa sasa, tofauti kubwa ipo katika idadi ya watu wanaowakilishwa na wabunge wa majimbo tofauti.
Alisema, "Mbunge anayetoka Zanzibar anachaguliwa na watu elfu kumi na moja, wakati mbunge kutoka Jimbo la Kawe anachaguliwa na watu laki tatu na elfu arobaini na mbili."
Lissu alisisitiza kuwa ingawa wawakilishi hao wanapewa mishahara na marupurupu sawa, lakini idadi ya watu wanayowakilisha inatofautiana sana sawa na ‘Mbingu na Nchi’ jambo linalochafua mfumo wa kidemokrasia.