Tundu Lissu: Kwenye Maridhiano Rais Samia ametatua yale mepesi lakini Mazito yanayohitaji kubadili sheria hajayagusa, tuzidi kumuombea!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wakati akihojiwa na Chief Odemba pale Star tv Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu alisema Rais Samia ameshughulikia mambo mepesi lakini Mazito yanayohitaji kubadili sheria bado hajayagusa tuzidi kumuombea

Lisu alisema mambo ambayo Rais ameshayashughulikia ni pamoja na kuwafutia kesi viongozi wakuu wa Chadema pamoja na Wanachama wa kawaida, pia Rais ameruhusu Mikutano ya hadhara

Ni jambo jema sasa Waziri wa Katiba na Sheria ameanza mchakato wa kisheria wa kuiendea Katiba Mpya

Dominica Njema!
 
Katiba Mpya ya Wananchi, Tume Huru ya Uchaguzi na itakayo tenda haki kwa wagombea na wapiga kura wao; ni moja ya mahitaji makubwa kwa Watanzania wengi kwa sasa.
 
Halafu inflation itakuwa controlled?
Kwa namna moja au nyingine. Maana wananchi watakuwa na uwezo wa kuchagua viongozi wenye uwezo, na pia akili ya kupambania matatizo yao.

Na siyo viongozi vilaza na wajuaji wanaoingia madarakani kwa msaada wa tume mbovu ya uchaguzi, na katiba inayo kipendelea chama dola miaka nenda.
 
Kenya wamefanikiwa Katika hilo?
 
Wakati akihojiwa na Chief Odemba pale Star tv Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu alisema Rais Samia ameshughulikia mambo mepesi lakini Mazito yanayohitaji kubadili sheria bado hajayagusa tuzidi kumuombea

Lisu alisema mambo ambayo Rais ameshayashughulikia ni pamoja na kuwafutia kesi viongozi wakuu wa Chadema pamoja na Wanachama wa kawaida, pia Rais ameruhusu Mikutano ya hadhara

Ni jambo jema sasa Waziri wa Katiba na Sheria ameanza mchakato wa kisheria wa kuiendea Katiba Mpya

Dominica Njema!
Hilo ni debe tupu hata akipewa hiyo katiba mpya atasema anataka kulala kitanda cha ikulu!
 
Nenda kawaulize hao Wakenya. Au kuna mahali nimekuambia ya kwamba mimi ni Mkenya?

Mzee Mgaya, acha kupenda kunywa mkangafu asubuhi kabla ya kula kitu chochote.
Kwa sasa Kenya ndio rejea nzuri ya Katiba Mpya 😄😄
 
Rejea ya Katiba ya Watanzania, ni ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba iliyovurugwa na Wanansiasa wabinafsi kutoka CCM na UKAWA kwenye lile Bunge la Katiba, lililojaa Wanasiasa wengi! Kukiko wataalam.
 
Rasimu ya Warioba imeshapitwa na wakati kisheria sasa rejea ni Katiba Pendekezwa!
 
Katiba pendekezwa ilipitishwa na watu wa mlengo mmoja. Hivyo kwa utaratibu wa kawaida kabisa, haina uhalali.

Mchakato urejeshwe kwenye Bunge lingine la Katiba, litakalo jaa wataalam wengi halafu na wanasiasa wachache tu ili kupunguza mivutano ya kuweka za vyama vya siasa.
 
Mchakato wa aina yoyote wa Katiba Mpya lazima utatawaliwa na CCM kwa sababu ndio Wenye nguvu!
 
Katiba Mpya sio maandamano.

Kila nchi ina utamaduni wa kuendesha mambo yake ikiwemo utawala demokrasia n.k
 
Naona dalili hii Katiba Mpya nayo inaweza kupatikana kwa maridhiano, wakasema tunachukua kidogo toka kwenye ile Rasimu ya Warioba, na kidogo tena toka kwenye ile Pendekezwa ya CCM.
 
Ndivyo itakavyokuwa!
 
Kama chadema wana lalamika kwamba katiba inasiginwa wanadhani ikiwa mpya ndio itafuatwa, hata ikishuka kutoka mbinguni bado yatakua yaleyale
 
Back
Top Bottom