Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu


Kama Lissu ni Kichaa kwa kusema ukweli basi Taifa hili linahitaji vichaa wengi na hata waliopo mitaani na mirembe waachiwe kwa manufaa ya taifa maana wapo sehemu zisizo sahihi.
 
kichaa ni ww unayomwabudu mtu,tangia lini nyerere amekuwa nabii au mtume asikosolewe?acha upimbi ndgu angu
 
It took
the madmen of yesterday for us to be
able to act with extreme clarity today. I want to be one of those madmen. Quote Thomas Sankara
 
Kumbe milembe nao wanaruhusiwa kwenda sikukuu haya ndo matitizo ya mtaani kutokuwa chini ya uangalizi wa dactari hahaha
 
Kweli umewakilisha.
 
Vichaa hakika ni wengi Tz, unaweza je kumsifu mtu ayemtukana Mkombozi wa nchi yako kuwa ni msanii, mwongo, mtapeli... Je! kwanini asherekee tarehe ya uhuru ambayo mtu alimwita tapeli ali iomba? kwa nini anakuwa off siku ya kifo cha mwalimu? Lissu ni kichaa na msaliti wa nchi hii.
 
Hivi wewe zetho una akili kweli?

Unamfananisha Nyerere na Bwana YESU?
Wewe mwehu kweli!
Kiboko yenu ni Tundu Lissu tu!
 
Last edited by a moderator:
Kha ha ha ha ha haaaaaaa! Wehu wako katika chama chama mafisadi a.k.a ccm!
Wameshindikana lakini dawa yenu iko jikoni kudadeki!


 
Tatizo la watanzania ni pale tunapomfanya Nyerere kama kanuni ya imani. Wakatoliki wananielewa vizuri ninaposema hili. Wakati nikianza mafundisho ya ubatizo tulikuwa na mtihani ambao pamoja na sara zingine ulitakiwa kuijua vizuri kanuni ya imani ambayo inasema nasadiki kwa kanisa katoliki la Rumi. Nasadiki kwa Mungu baba mwenyezi. Nasadiki, Nasadiki, Nasadiki.

Mawazo yako ukiyaweka katika kuamini kwamba hii ndiyo imani uliyoingia kamwe hutaruhusu kusikia upinzani dhidi ya kile ulichokiamini. Wakatoliki watupu wakiingia katika mjadala juu ya imani ya matumizi ya rozari kamwe hatutegemei upande wa pili katika rozari hiyo. Wasabato wawili watupu katika mjadala juu ya ibada ya siku ya jumamosi kamwe hatutegemei kuiona kasoro ya uhakika wa siku hiyo, hali kadharika mashehe wawili wenye imani juu ya mtume hawataweza kuja na jipya juu ya kasoro ya mtume kwa sababu tu kwamba wako ndani ya kanuni moja ya imani.

Inahitaji msuli na ubabe wa hali ya juu kusimama katikati ya watu walioiva katika kanuni ya imani ya matumizi ya rozari ukaanza kuikosoa, Tegemea ukweli alioubainisha "Henrick Ibsen" katika kitabu chake "An Enemy of the Peole". Utaitwa adui mkubwa wa watu kwa sababu umetamuka jambo ambalo watu hawataki kulisikia. Wenye msuli wa hivi mara nyingi humaliza vibaya. Huishia kupotea kabisa kwa sababu hata walio karibu nao hawako tayari kuonyesha kuungana nao kwa sababu wanajua kanuni ya imani iliyo katika jamii wanayopambana nayo. Kama ni ukweli bado utabaki kuwa ukweli lakini dhahili itaonekana wakati wewe tayari umeshapotea katika jamii. Umeshabwagwa kama msaliti.

Nyerere alikuwa binadamu hivyo kuna kasoro alizozifanya, lakini kwa vile ni kanuni ya imani kwa wengi hakuna mwenye ujasiri wa kutamuka kasoro zake. Ukiruhusu akili zako zimuone kama binadamu utaona kasoro zake nyingi tu za ubinadamu.

Kwa mfano: Nyerere kama kiongozi na mdau mkubwa wa muungano wa dunia tangu katika wazo walilokuwa pamoja na Nkrumah kuunganisha Afrika nzima, dunia ilimshangaa alipokubaliana na waasi wa Biafra waliotaka kujitenga kutoka Nigeria. Hiyo ni kasoro ambayo kama akili yako haijaruhusu kanuni ya imani utaiona na kusema kweli binadamu mwenzangu alikosea.

Nyerere aliwahi kusema katika moja ya Bith day part yake kwamba watanzania wananiombea niishi miaka mingi wakati sayansi inasema miaka kuanzia 80 ni ya shida. Nami nashukuru na kwa afya niliyonayo naamini nitafikisha na kuiona 2000. Kama akiri yako haiko katika kanuni ya imani utaiona kasoro kubwa ya ubinadamu wa kutokujua kwamba Mungu ndiye anaamua. Matokeo yake Nyerere hakuiona 2000. Kama akiri yako iko katika kanuni ya imani utapata tafsiri nzuri. Waweza kusema alikuwa akiwafariji watanzania, au lolote la kupamba kauli hiyo.

Tatizo langu kwa Lissu ni uchaguzi wa maneno ambayo unaweza ukatoa ukweli lakini bado ukaacha faraja kwa wadau wa kanuni ya imani. Anayoyasema yote ni kweli. Kuna sababu gani ya kutokuonekana Abdul Jumbe katika matukio mengi ya kitaifa wakati yuko hapa Mji mwema?

Nani aisiyejua kwamba wasira aliwahi kumwendea Nyerere akimfahamisha kwamba safari hii warioba hataupata ubunge kwa sababu watu wamechoka na mikono mitupu. Nyerere kwa kauri hiyo alizunguka majimbo yote ya mkoa wa Mara akiwaambia wasira ni mtoa rushwa mkubwa. Anachinja ng'ombe, anagawa kanga, chumvi ili kupata ubunge jimbo la Bunda. Akawaambia wasira hafai. WARIOBA anafaa. Haya niliyasikia mimi mwenyewe uwanja wa sabasaba Bunda. (kumbuka Lissu alisema kuna watu waliingia upinzani mpaka Nyerere amekufa ndio wakarejea CCM).

Kwa vile siasa inakutaka uwe mnafiki, sasa hivi wasira ndiye mpinga rushwa mkubwa. Ndiye wa kumuenzi baba wa taifa. Sijui kama rushwa alishaacha au lah.

Ndio maana mara nyingi nimekuwa nikisema katika ngazi ya uongozi wa kitaifa lazima uwe mnafiki na wakati mwingine hata mbinu chafu za kuhakikisha msimamo unaouamini kwamba ni muafaka unakubalika katika jamii. Haya yote wanayafanya wanasiasa akiwemo Nyerere na hawa tulionao leo. Hata Lissu akiingia madarakani lazima awe mnafiki na mzoefu wa mbinu chafu.

Namaliza kwa kumwambia Lissu umegusa kwenye kanuni ya Imani, tegemea mashambulizi mengi. Usiposimama imara utapotea. Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika hawatakutetea kwa sababu wanaogopa kugusa kanuni ya imani.
 
Kama Nyerere alikuwa ni kanuni yao ya IMANI, mbona walivunja AZIMIO LA ARUSHA bila ridhaa yake? Tena katika hotuba yake moja, alieleza huwa anatembea na Biblia pamoja na kitabu cha AZIMIO LA ARUSHA, na alisisitiza kuw hajawahi kuona makosa yaliyokuwepo kwenye AZIMIO la ARUSHA walilolivunja CCM wenyewe kule Zanzibar.
 
Maamuzi yeyote ya katiba yatategemea kura za BARA na za ZANZIBAR kivyake. Wanaoegemea hoja ya "umungu" wa Nyerere, wakafanye analysis na Zanzibar. Aliyotendewa Abdu Jumbe, Deurado na wengine na Nyerere yatawapa ugumu sana CCM Zanzibar. ..
 
Ahsante kwa Uzi makini mkuu.Ila wasiwssi wangu Ni kwanini tunaukataa ukweli,kwanini hotuba ya lisu ilete ugomvi na kuacha mmambo ya msingi❓,kwanini misingi ya nyerere imeachwa,Kuna matusi makubwa kama hayo❓,utakatifu WA nyerere hats Mara moja hauwezi kuosha Yale aliyofanya kwa uzandiki na unafiki mkubwa.
 
Kinachowasumbua CCM zidumu fikra....! Wanatumia u mbumbumbu wa watz wengi hasa vijijini kujipatia wanachama. Wanachama wao wengi ni wale wa kupewa chumvi na sukari, ni nadra mno kukuta msomi wa chuo kikuu anashabikia Ccm Vinginenyo ni unafiki.....!
 
Mkuu nimekusoma vyema sana.

Kifupi Nyerere alifeli karibia asilimia 70 ya kila jambo lake aliloliasisi. Alifeli mengne hata kabla hajaanza kuyatekeleza. MUSOMA RESOLUTION lilifeli hata kabla halijaanza kutekelezwa, AZIMIO LA ARUSHA lilipelekea Taifa kuwa maskini hata kufikia nchi kuwa katika kumi za mwisho kwa hali mbaya ya uchumi. Alifeli kwakuwa hakuwa na strategia za kufikia yale malengo yake ispokuwa alikuwa ni mbinafsi na aliyetaka kujijengea umaarufu binafsi wakati kulikuwa na watu waliomzidi kimaarifa na ufahamu wa sera ya ujamaa kama ABDURHAMAN BABU. Hakutaka kujifunza bali alivamia sera ya ujamaa kwakuwa tu ilikuwa yafavour malengo yake ya kidikteta.

Mjamaa gani hata umeumwa unaenda kutibiwa nchi ya makapitolisti? Hakuwa mjamaa bali aliuchagua ujamaa kwakuwa unaendana na uongozi aliyoutaka. Haya ndio Watanzania wasiopenda kuyasema wala kuyasikia ndio maana aligeuzwa Mungu mtu kumbe hana lolote.
KWELI LISSU AJIANDAE KUKUMBUNA NA CHANGAMOTO.
 
Wassira kama Kigwangala vile! Duh! hii nchi kweli imeoza....ndio maana wanachezea mitaala kama wanaandika barua za mapenzi vile! ili watanzania maskini waendelee kuwa mbumbumbu wasiojua kuchambua mambo na wanaokubali sukari kilo moja na kipande cha kanga kuimbishwa wimbo wa "kidumu chama cha majambazi" miaka nenda rudi!

We are behind Lissu at any cost, liwalo na liwe!
 
Well said, Lisu kasema kweli, ila kweli hii sasa inageuzwa negatively na kipropaganda zaidi ili haswa ionekane hoja zote za Lisu kuwa ni ubabaishaji, mi nadhani hakuna kitu ambacho Lisu hajakitolea reference na hajafanya uzushi wowote. "Mkubwa hakosei" huu msemo siupendi, maana unaruhusu watu waliowahi na walio madarakani wasikosolewe, hata sisi watu wa kawaida tume adapt culture hii. Hili halikubaliki, Nyerere alisaidia kuleta uhuru, ni jambo jema lakini halituzuii kusema alipokosea maana makosa yake sasa yanaleta migogoro.
 
mi simkubali nyerere wala nini,ya nini kumkumbatia mtu alie amua kwa makusudi kutuchagulia umaskini watanzania hasa sisi wananchi wa mikoa ya kusini. alitutelekeza kwa makusudi kabisa aling'oa reli wakati alikua anajua kabisa barabara hatuna kifupi nyerere alitunyanyasa sana kusini mpaka ikajengeka mentality mbaya sana kwa watu wa mtwara tulionekana kama sio binadamu vile full kudharaulika.aah mzee nyerere wewe mzee bana......agggrrrr lala salama mzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…