Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu



Azimio la Arusha lilivunjwa Nyerere akiwa hai, na kwa ridhaa yake maana hakulikomalia kama lile la G55 na TANGANYIKA yao!
Azimio la Arusha lilivunjwa wakati DUNIA nzima ikifanya kinachoitwa 'STRUCTURAL ADJUSTMENT' baada ya mfumo wa ujamaa DUNIANI ukionyesha kushindwa kuhimili mapigo ya VITA VYA BARIDI mnamo miaka ya 1980 ya mwishomwisho!
KWAHILI LA KUVUNJA AZIMIO LA ARUSHA NAOMBA WATANI ZANGU BORA MNYAMAZE!
NA KUHUSU 'ATI KUNA' WATU NYERERE ALIKUWA HAWATAKI VILEVILE MNAONGEA BILA USHAHIDI, HEBU TULETEENI USHAHIDI NA SAHIHI MTUONYESHE! (TUMEISHAWAONYESHA MKATABA WA MUUNGANO!)
 
Mwanadamun ni mwanadamu tu...., hata akiwa na hekima/busara kwa kiwango chochote, hapotezi ubinadamu wake!
As long as amezaliwa na mwanamke, ni lazima atafanya makosa tu, kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
Nyerere included...
 
Pole Chinga One. Ukweli ni kwamba Nyerere hakua perfect. Hata yeye alijua. Naamini hata kuondoka kwake madarakani ilisababishwa na uchumi kuwa mgumu huku International Bodies zikimlazimisha afanye mabadiliko ya sera za kiuchumi ndipo akopeshwe.

Kukwepa aibu ya kufungua mipango ya ubepari akaamua King'atuka.

Ila watanzania hawapendi kusikia.
 

Sikubaliani na wewe kwa 100% kuhusu ridhaa ya ayati Nyerere kuridhia kuvunjwa kwa AZIMIO la ARUSHA. Sote tumemsikia akilalamika kwenye hotuba zake jinsi viongozi wa CCM walivyofanya ufedhuli wa kulivunja AZIMIO LA AARUSHA ambalo alisisitiza ya kuwa halikuwa na tatizo lolote. Ile miiko ya uongozi katika AZIMIO LA ARUSHA, ndiyo zao la viongozi tulionao leo ndani ya CCM.
 
Hawa ndio maadui wakuu wa Tanganyika
1.J.K.Nyerere
2.CCM
3.Rushwa
4.Ujinga wa Watanganyika wa vijijini.
5.Ubinafsi wa viongozi wa CCM
 

Sawa mkuu mkataba mumetuletea tumeuona. He mkataba ule kuna mahali pameandikwa Nyerere ni Mungu wa CCM? Je mkataba ule kuna mahali popote pamezuia serikali tatu? Je mkataba ule ulikubaliwa Zanzibar? Ni mkataba halali? Je mkataba ule umezuia kujulikana kwa Tanganyika? Where is Tanganyika birth certificate?

Mkataba ule unaitambua Tanganyika sio Tanzania. Mkataba umeandikwa Union of Republic of Tanganyika and people's Republic of Zanzibar. Ndani ya Mkataba ule hakuna kitu kinaitwa Tanzania. Tanzania iliundwa kwa maneno sio kimaandishi?
 
Hawa ndio maadui wakuu wa Tanganyika
1.J.K.Nyerere
2.CCM
3.Rushwa
4.Ujinga wa Watanganyika wa vijijini.
5.Ubinafsi wa viongozi wa CCM
 

Asingeridhia lisingeguswa kama alivyowafanya G55!
ZAIDI YA HAPO ANGELILIRUDISHA MARA BAADA YA MKAPA KUINGIA IKULU MAANA NINAAMINI KABISA NDUGU YETU MKAPA ASINGETUANGUSHA, LAKINI MAJI YALIZIDI UNGA!
 
Maamuzi yeyote ya katiba yatategemea kura za BARA na za ZANZIBAR kivyake. Wanaoegemea hoja ya "umungu" wa Nyerere, wakafanye analysis na Zanzibar. Aliyotendewa Abdu Jumbe, Deurado na wengine na Nyerere yatawapa ugumu sana CCM Zanzibar. ..
Kura za zanzibar hazina uhusiano na CCM wala hazina uhusiano na UKAWA.
 

Mkuu fuatilia hotuba ya Nyerere kuhusu kuvunjwa kwa azimio la Arusha na kuletwa azimio la Zanzibar, kisha utueleze kama aliridhia.
 

Wanachagua vya kumuenzi
 
Ule mchakato kumtangaza mwenye heri sijui uliishia wapi?
 
umenikumbusha mbali sana. kwa sisi tuliochungulia physics kidogo tunamkumbua professor mmoja wa kiitaliano aitwaye Galilei Galileo miaka ya 1616 pale alipogusa masilahi ya kanisa katoliki. sote ni mashhdi kwa kile kilichompata.
 
yule mzee alikuwa haambiliki. ndo maana hata sera yake ilikuwa "zidumu fikra SAHIHI za mwenyekiti wa chama".
 
In politics.... There are borders that should never be crossed.
Ni upunguani kusema eti ""TUNDU LISU ASUBIRIE CHALLENGE"" Anachokisubiri huyu mvuta Bangi ni KIFO TUUUU.kinaweza Kuwa cha kisiasa,kiroho au vyote viwili
 
Anayejiona yeye ni msafi hajawahi fanya kosa na awe wa kwanza kumhukumu Mh Lissu. Alichokisema Mh Lissu kuhusu Mwl Nyerere ni kile ambacho wengi hawawezi kukisema,Mwl Nyerere ni mwanadamu km ulivyo wewe hivyo makosa ni jambo la kawaida. ikiwa Mh Lissu alitenda dhambi juu ya udhaifu wa mwl Nyerere basi anahitaji kusamehewa bure, kama wale wanaotukana live pale mjengoni then wanachekewa tu bila kuchukuliwa step yeyote..Liondoe boriti jichoni mwako ndipo utoe kibanzi jichoni kwa mwenzio.
 
Tundu Lissu MJINGA asiyetaka kuelimika, asiye na adabu, asiyetaka kukiri kosa hata lililowazi. Unamsamehe vipi mtu kama huyu anayesema TANZANIA na WATANZANIA hawapo duniani KIHALALI?

Tundu Lisu hajatuambia KITI cha TANGANYIKA kiliondokaje kule UNO. KIliondolewa na hati hii ya MUUNGANO ya "kughushi"?

Tundu Lissu anatuambia Mwalimu hakuwa Mungu wala Malaika lakini hatuambii pia kuwa Mwalimu hakuwa Shetani wala Luciferi.

Mwambieni Tundu Lissu asimame mle Bungeni akiri ujinga wake huo kama alivyousambaza kwa nguvu zote mle mjengoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…