Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Wakuu.

Hivi majuzi rais Kikwete ameingia kwenye mtego wa propaganda na kujikuta naye anaingia kwenye kundi la kumsulubu Mheshimiwa Tundu Lissu kwa madai kuwa amewatukana waasisi wa Taifa letu, Jana tena kwenye hotuba yake amerudia yaleyale! cha kushangaza na kustaajabisha ni kwamba wote wanao imba na kughani (akiwemo JK) kuwa Tundu Lissu amemtukana Baba wa Taifa hawasemi kuwa ni tusi gani baya ambalo Mheshimiwa Tundu Lissu amelitukana hata na wakiulizwa kuwa tusi hilo ni lipi hawawezi kulitaja.

Naomba kuwakumbusha pia kuwa hata Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (SUGU) Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA naye alisha wahi kuingizwa matatani baada ya kusema kuwa Mhe waziri mkuu Bw Mizengo Pinda ametoa kauli ya "KIPUMBAVU", Sugu alitoa kauli hiyo baada ya waziri mkuu kutoa ile kauli ambayo mahakama ili dhibitisha kuwa ilikuwa kauli ya kipumbavu. kauli ile pia imemuingiza Pinda matatani maana ana kesi ya kujibu. Kauli yenyewe ambayo imeitwa ya kipumbavu ni ile ya "....Wapigwe tu..." Sugu alishatakiwa kwa kuiita kuwa ilikuwa kauli ya "Kipumbavu" na baadae mahakama ikamuona hana kesi ya kujibu.

Mtakumbuka kuwa mheshimiwa Tundu Lissu alipata wasaa wa kujibu alicho kiita kihoja cha kuambiwa kuwa amemtukana Mwl Myerere alipo kuwa anachangia kwenye BM la katiba kule Dodoma. Alisema...

"Mh, Mwenyekiti naomba nijibu vioja , kuna kioja Mh,mwenyekiti kinasema TUNDU LISSU amemtukana baba wa taifa, naomba mh,nijibu kama ifuatavyo mwaka 1995 baba wa taifa alihudhuria mkutano wa Meimosi Mbeya na badae akaandika kijitabu kinaitwa " TUJISAHIHISHE" katika kijitabu chake baba wa taifa alisema asiye kubali kukosolewa hawezi kuwa kiongozi bora na baba wa taifa aliye kuwa mwenyekiti mwanzilishi wa ccm alisema CCM sio mama yangu,Mh mwenyekiti baba wa taifa alikuwa binadamu, hakuwa mungu, hakuwa malaika na hajawa mtakatifu bado, tunaposema makosa yake tunathibitisha ubinadamu wake, na baba wa taifa mwenyewe angekuwa wa kwanza kukubali alikuwa binadamu na sio mungu na kama binadamu alikuwa anakosea, na kwa wasio fahamu mwenyekiti; baba wa taifa aliwahi kuunga mkono jamuhuri ya biafra iliyokuwa inapigana vita kujitenga na Nigeria, alikosea hakuwa mungu, alikosea na tunaposema alikosea hatumdhalilishi tunathibitisha ubinadamu wake, kuna watu ambao wapo humu bungeni ambao akiwa hai walikikimbia chama chake wakaenda NCCR -MAGEUZI wakasubiri mwl amekufa wakarudi CCM, leo wanajidai wao ndo watetezi wa baba wa taifa , Mh,Mwenyekiti nimemaliza na baba wa taifa sitarudia!.."

Jana tarehe 25 April 2014 kwenye hotuba yake, JK ameendelea kupotosha tana kuwa Tundu Lissu amemtukana baba wa Taifa, Hii ilipelekea kujiuliza maswali kadhaa, Je ni kweli kwenye hoja zote na ufafanuzi alio toa Tundu Lissu kuna neno lenye ncha kali (TUSI) ambalo amemtukana baba wa Taifa?! Je kwenye hotuba nzima JK ameshikilia tu tusi ambalo halionekani na hakuna hoja nyingine za msingi ambazo zinahitaji majibu ya kina?! Na kama tusi hilo amelishikilia na kulighani kila mara, Je tusi hilo ni lipi?! Je wakati huu rais JK anapo msingizia Tundu Lissu kuwa amemtukana Mwl Nyerere (muasisi wa taifa) yeye anajijua kuwa ametukana Mwl Nyerere kuliko anavyo msingizia Tundu Lissu?!


Kama raisi wetu (JK) ana msingizia Tundu Lissu kuwa amemtukana Mwl Nyerere, je orodha hii fupi ya matendo ya serikali ya JK sio matusi ya dhahiri kwa Mwl Nyerere (muasisi) wa Taifa letu?!

1. Mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar ambayo yamempora JK mabadaraka tena akiwa bado yungali madarakani na aka kaa kimya na sasa hivi analalamika kuwa kuna vyama vinataka kuvunja muungano huku akijua kuwa ukimya wake ndio umechangia kuvunja nchi moja (Ya muungaon) tuliyo kuwa nayo na sasa tuna nchi mbili, Je haya sio matusi kwa Mwl JK aliyesema "...Rais tunaye mchagua lazima ajue kuitetea na kuilinda katiba na kama hawezi aende akalime shamba lake..." na amedhihirisha kwa kuacha madaliko ya 10 ya katiba kule ZNZ kuanzisha dola huru?

2. Rais Jk anajua kuwa ulitokea wizi wa pesa za wavuja jasho kupitia akaunti ya malipo ya nje (EPA) na imesemwa maraka kadhaa kuwa pesa hizo ndio zilisaidia kampeni za kumuingiza madarakani 2005 (Haijawahi kukanushwa) na baadae walio iba pesa hizo (baadhi) ambao ni makada wa CCM yeye mwenyewe akihutubia bunge Dodoma akawaombwa kuzirejesha fedha hizo huku akijua kuwa waliofanya wizi huo ilikuwa kinyume na sheria, Je hayo hayakuwa matusi kwa baba wa Taifa kukiuka katiba na sheria za nchi?!

3. Je wale watanzania wenzetu walio uwawa kule Arusha Jan 5, 2011 na baadae ripoti ya tume ya jaji Ramadhani Manento kukiri kuwa Polisi walihusika na mauwaji yale kwa sababu za kisiasa na baadae JK huyo huyo akiwa Dodoma akiwahutubia wajumbe wa kamati kuu akawaagiza CCM kuacha kulitumia jeshi la Polisi kudhibiti vyama pinzani na baadae akauwawa Daud Mwangosi na aliyesimamia mauwaji ya Mwangosi, JK huyohuyo akampandishwa badala ya kumuwajibisha! Je hayo hayakuwa matusi kwa Mwl Nyerere aliyepinga ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binadamu?!

4. Je aibu hii ya dawa za kulevya ambayo viongozi wa CCM na serikali yake wameamua kulibebesha taifa hili ili wao wapate fedha huku wakiwageuza vijana wenzetu kuwa punda wao wa kubebea bidhaa hizo haramu, na wengine kugeuka kuwa mazezete kwa matumizi ya madawa hayo sio Matusi kwa Mwl Nyerere (Muasisi wa Taifa hili)?!

5. Je; sio matusi kwa viongozi waandamizi wa CCM kuhusishwa na uporaji na uwindaji haramu wa raslimali za Taifa (Kama kujilimilikisha madini na uuwaji wa wanyama pori) ambapo Mwl Nyerere enzi za utawala wake alizilinda na kuzihifadhi kwa matumizi na faida ya wananchi wote wa Tanzania?! (mwalimu alilinda mpaka mabenki, leo NBC iko wapi URAFIKI iko wapi, SUKITA iko wapi, Viwanda alivyojenga na kuviacha viko wapi?)

6. Je kurithishana madaraka kwenye chama ambako Mwl Nyerere hakuthubutu kufanya hivyo kwa mwanaye yoyote sio matusi kwake?! (rejea chaguzi ndogo za hivi karibu). Ni ipi kamusi ya matusi ambayo JK ameamua kuitumia na wapambe wengine kusema kuwa Tundu Lissu ametukana?!

7. Je Mwl Nyerere alipo kuwa mwenyekiti wa CCM aliasisi na kusimamia kikosi cha kijeshi ndani ya chama ambacho kimekuwa na kawaida ya kuteka, kuuwa na kutesa wanachama wa vyama vingine na polisi wakaogopa kuchukua hatua dhidi ya kikosi hicho?! (rejea mauwaji ya Mbwana Masudi kule Igunga, Mauwaji ya Samson Mbwambo kule Arumeru nk), Je haya sio matusi kwa Mwl Nyerere aliyekuwa ana sisitiza kuheshimu utu wa mwanadamu?!

8. Je hayakuwa matusi kwa Mwl Nyerere kukiri mbele ya vyombo vya habari vya kimataifa kuwa ".... Sijui kwa nini wananchi wangu ni maskini..." Huku akijua kuwa nchi ina raslimali nyingi na yeye amekuwa busy kwenda nje kuomba misaada kuliko Mwl aliyekuwa busy kusisitiza kujitegemea na kuondoa utegemezi kupitia program kadha wa kadha?
(Mfano vijiji vya ujamaa, kilimo cha kufa na kupona nk)

9. Je si matusi kwa Mwl Nyerere kutokuheshimu maoni ya wananchi na matokeo yake kutumia ubabe kuhakikisha kuwa msimamo wa chama ndio unaleta katiba huku akijua kuwa katiba inayoundwa si katiba ya chama bali katiba ya nchi ambayo ni kuu kuliko katiba yenye itikadi au msimamo wa chama chochote?!

10. Je kumfanya Mwl kuwa aliyo yafanya hayafai kukosolewa sio kumfananisha na Mungu au Malaika?! Je hayo sio matusi ya kujipendekeza wakati Mwl Mwenyewe amesha kiri makosa yake mara kadhaa na hata kufikia hatua ya kutoa machapisho kukiri makosa yake?! (Mfano; Ukisoma "Tujisahihishe" "Uongozi wetu na hatma ya Tanzania") na, je sio kinyume na mafundisho ya Mungu kumfanya binadamu mwenzako kuwa ni mtimilifu kuliko Mungu?!

Nabaki tu kujiuliza; Kati ya Mheshimiwa Kikwete na Tundu Lissu nani kamtukana Mwl Nyerere matusi yanayo onekana dhahiri kuliko yale ya kubumba na kusingizia bila ushahidi wenye mashiko?! Nani anaweza kunieleza TUSI lililo tukanwa na Tundu Lissu?



 
Umeandika upambavu mwingi sana, tatizo nyie vijana wa Bavicha mna upeo mdogo, umejifungia Ufipa ukaona umeandika la maana.

Njaa itakumaliza wewe tafuta kazi ya maana ufanye utaendelea kuwa mpambe wa Dr.Slaa na Mbowe mpaka lini.

Sijui hata hiyo shule ya kata unayofundisha unafundisha muda.
 
Hongera kwa ccm kuwa na vijana wenye upeo kama LUSINDE na KINGUNGE.
 
Ingekuwa biblia basi tungesema umenena kifupi ni kuwa umeonesha ukweli kama wanaweza basi wajibu kwa hoja na si matusi! Kikwete aache propaganda zake
 

Majibu ya Intarahamwe ndo haya.
 
Kwa nyongeza kufuatia mleta mada ni kwamba, JK akiwa kiongozi mkuu wa nchi ambae ni mwenyekiti wa maccm ,kwa takriban miaka 9 sasa ameendelea kumtusi Mwalimu Nyerere kwa kuendeleza kulipoteza Azimio la Arusha
 

Miongoni mwa mijitu mifyatu pale Lumumba ambayo naamini kwa maneno yao machafu ingekuja kusema tusi la Tundu Lisu kwa muhasisi wa Taifa ni wewe. kama na wewe umeshindwa kulisema hilo tusi basi kweli Lissu hakutukana. Hahaha
 


Naomba kukubaliana na uchambuzi wako wa kina
 
Amesema eti 'kama sahihi ya Karume iliforgiwa basi aliFORGE ni Nyerere'.

Sasa forgery haina ihusiano wa kuongopa?
 
Tena tusi lingine alillitoa jana alipodai kuwa Nyerere alifoji saini ya karume katika hati ya muungano.
 
Hivi mlitaka JK aongee nini kuhusu Tundu Lissu, mtu aliyekuwa anamhofia tangu kipindi chote cha kampeni, mlitaka JK amsifie TL? haiwezekani...........Rais wetu anaingizwa kwenye siasa nyepesi na kusahau kuwa yeye ni Rais wa wote na sio CCM peke yao, anashndwa kusoma maandishi ukutani kuwa wenzake wanamlegeza na anaonekana kioja kwenye jamii, tena kwa hili la bunge la katiba ndio kabisa JK ameonekana wa ajabu.........Rais unahutubia Taifa unaongea mambo ya Tundu Lissu kumtukana Baba wa Taifa, kama ni tusi au sio tusi si kila mtu alisikia na kujiamulia mwenyewe jinsi ya kumchukulia TL, leo Rais unalirudia mara mbili mbili utazani hakuna mengine ya kuongea kwenye Nchi hii ya kifisadi.

Rais aache upambe kwa chama chake, Rais anatakiwa awe Rais wa Nchi, aonyeshe kukerwa na mambo yote yanayosababisha chuki na utengano, amkemee Lukuvi, amkemee Komba, amkemee Makonda awakemee wote wanahubiri na kuropoka yasiyofaa mbele ya jamii, wawe wanachama wenzake na wa vyama vingine, sio kila siku kutuletea hadithi za Tundu Lissu, kila mtu alisikia hatuhitaji kuambiwa tena.
 
Ni jukumu la kikwete kukemea tabia zisizokubalika, kama hutaki unaacha.
 

Sasa huyu kaongea nini?..kaacha kujibu mada iliyopo mezani kakimbilia kwa Slaa na Mbowe
 
Tundu Lisu Mara nyingi anakuwa Hana hoja. Cha kushangaza wengi wanapotoshwa na kumfuata. Na sababu kubwa ni WENGI WANAANGALIA NAMNA ANAVYOWASILISHA HOJA NA SI HOJA ANAYOWASILISHA. WANANASWA NA MTEGO WA KUANGALIA NAMNA ANAVYOONGEA NA SI MANENO ANAYOONGEA. Mara nyingi TULI amekuwa akiongea vitu ambavyo ni vya kawaida tu au obvious facts, lkn umati unasikiliza kwa makini kana kwamba anatema madini ambayo hayajapatA kutokea. Hivyo nashauri mkitaka kujua hoja zake msiangalie drama zake au anavyo dramatise. Wekeni uangalifu wenu kwenye kile anachoongea. Tuone kama mtamwita machachari. Umachachari wa namna yake ya kuongea ni wa watu ambayo Mara nyingi hawajiamini kuongea mbele ya umati. Sisi tunaojua psychology na philosophy of law tunawatambua watu Wa namna hiyo. Wanasheria wengi hususan mawakili huongea kwa namna hiyo.

Lingine ni kuwa TULI anashindwa kutofautisha kati ya kukosoa na kutukana. Jinsi alivyoliongelea suala la saini ya kwenye hati ya MUUNGANO siyo kukosoa ni kutukana. MTU kumwambia ameghushi saini ni kashfa au matusi.

Pia lisu ajue kuwa yeye ana mchango kwa kiasi Fulani kwa taifa. Lkn mchango wake hautafikia kamwe mchango ambao baba Wa taifa ametoa kwa taifa hili. That was a remarkable man. Lisu hataweza hata robo kufikia uwezo Wa mwalim. Lisu amejawa na mtazamo Wa kitoto kibinafsi usio na uzoefu na hehima. Kwa sababu ya kukosa uzoefu muda mwingi amekuwa akiongea very pure and fundamental principles rather than an applied and materialising principal. Kinacho mpandisha ni kwamba wale rival wake ccm wengi wao hawako makini hivyo ni rahisi kushindwa kwa hoja hata zikiwa nyepesi.
 
Miongoni mwa mijitu mifyatu pale Lumumba ambayo naamini kwa maneno yao machafu ingekuja kusema tusi la Tundu Lisu kwa muhasisi wa Taifa ni wewe. kama na wewe umeshindwa kulisema hilo tusi basi kweli Lissu hakutukana. Hahaha
Nyerere kaasisi taifa gani jamani mbona mnazidi kutudanganya . Tanganyika ilikuwepo kaasisi nini na ni baba wa taifa gani alilizaa na nani?
 
Kwa ccm uongo ndiyo ukweli na ukweli ndiyo uongo kwao

Kila siku mie nahoji matusi ya tindu lisu yako wapi maana sisi sio watoto na wote tulitizama bunge na kusikia alichosema mh lisu ila kwa vile mmezoa vya kunyonga na vya kuchinja hamviwezi kamwe

Hatuna mda mrefu washauri wa mkuu watamwambia auongee na mama nyerere atoe tamko na kulaani matusi ya lisu( sijui yepi sasa?)
 
Toka lini akili za BAVICHA zikapambanua na kuelew lipi tusi na lipi siyo tusi.

Kuna lugha zinazotumiwa hata hapa na vijana wa BAVICHA ambazo kwa watu walioelimika na kustaarabika wakizisoma wanaelewa kuwa ni matusi lakini kwa BAVICHA wanaziona ni lugha za maongezi ya kawaida katika jamii.

Tusi utalielewa ni tusi kama unafahamu ni tusi lakini kama hufamu ni tusi, utaelewaje kama ni tusi?.

Wewe huelewi lipi ni tusi na lipi siyo tusi, sasa utaelewewaje na kupambanua kama alichokisema Tundu Lissu ni tusi.

Asiyefunzwa na wazazi wake, dunia ipo kwa kazi hiyo.

He who knows not and knows not he knows not, he is a fool
 
Nyerere kaasisi taifa gani jamani mbona mnazidi kutudanganya . Tanganyika ilikuwepo kaasisi nini na ni baba wa taifa gani alilizaa na nani?

Una maana gan? Labda hatujakuelewa. Lkn kwa kuanzia soma historia ya kuanzisha sheria ya NYARUBANJA ENFRANCHISEMENT ACT NA CHIEFDOMS ENFRANCHISEMENT ACT YA 1963.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…