Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tusubiri, ukweli ukidhihiri uongo hujitenga. Kumbuka juzi, Sitta ingawa yupo busy bungeni lakini kaitwa na Pengo na kaenda mbio-mbio, jiuliize kunani?

Sita hakuitwa na Pengo.
Yeye mwenyewe ndio alimtafuta.
Na sio Pengo tu alenda pia kuonana na Mufti.
Unafaidika nini hasa na chuki zako za kidini Lakini ?
 

Wewe sasa ushahamia kwenye udini, sisi huko hatupo tunajadili muungano sie.
 
Pengo msimamo wake binafsi ni serikali mbili na kashamwambia Sitta...bado Lissu na yeye kupewa maagizo
 

Hapa sasa mutaanza kuamini na kujua nini MZEE MUHAMED SAID anacho kiandika na kukisema kuhusu JKN
 
hivi watu wanajua maana ya kutukan kweli?walio hoji uhalali wa muungano enzi za ticha wote walipotezwa.
 
Unaweza kuwa sawa kutokana na umri wako hiyo hotuba ukaipa hiyo hadhi.

Kulikoni leo umeshindwa kumtetea Nyerere kisa aliyesema hayo maneno ni mtu unampenda Tundu Lissu.

Punguza unafiki siku ingine watu wakieleza mapungufu ya Nyerere usitokwe na povu.
 

sasa kama mtu hadi vyombo vya habari alizuia mi namuona ka dicteta kwan alichotaka yeye ndo kifanyike kazuia maendeleo kwa muda mrefu
 
Sita hakuitwa na Pengo.
Yeye mwenyewe ndio alimtafuta.
Na sio Pengo tu alenda pia kuonana na Mufti.
Unafaidika nini hasa na chuki zako za kidini Lakini ?

Mkuu huyu FaizaFoxy ni mdini balaa! Yaani kamwona Pengo tu; Mufti kwake sio issue. Sometimes huyu ni wa kupuuza tu.
 
Last edited by a moderator:
Pengo msimamo wake binafsi ni serikali mbili na kashamwambia Sitta...bado Lissu na yeye kupewa maagizo

Wewe ni wa kupuuzwa na kuonewa huruma kabisa.
Uendako lazima utaokota makopo tu.
 
sasa kama mtu hadi vyombo vya habari alizuia mi namuona ka dicteta kwan alichotaka yeye ndo kifanyike kazuia maendeleo kwa muda mrefu

Kwa kipindi chake kulikuwa na mantiki. Bila udhibiti ingekuwa vigumu kujenga misingi ya umoja wa kitaifa ukizingatia wakati ule hangover ya ukoloni na usultani ulikuwa bado dhahiri.
 
Mkuu huyu FaizaFoxy ni mdini balaa! Yaani kamwona Pengo tu; Mufti kwake sio issue. Sometimes huyu ni wa kupuuza tu.

Kabisa Mkuu.
Mimi sijui hata anafaidika nini na kete yake ya udini.
 
Last edited by a moderator:
na pale alipomnukuu nyerere aliyoyasema gazeti la observer? Na baadae nyerere akawatia ndani waliohoji muungano? Huo si uongo wa nyerere?

mkuu uwe mkweli nachelea kukuita mtumwa wa mawazo yako mwenyewe! Wapi lisu alisema" nyerere aliishi kwa uwongo na udanganyifu" nukuu ya gazeti la observer ndo imekamilisha uongo wako? Kumbuka hata lisu anamheshimu na kuthamini mchango wa baba wa taifa.lete ushahidi onesha wapi lisu kasema hayo.vinginevyo ww ndo unamtusi mzee wa watu muacheni apumzike huko aliko kwa amani usimtumie baba wa taifa kummaliza na kumgombanisha lisu na watanzania. Kama huna cha kuandika kaangalie mambo mengine. Najua utakereka ila jaribu kuwa mkweli na unisamehe kama nimekukosea.leo ni siku ya kuabudu acha uongo
 
Lissu hajamtukana Nyerere amesema ukweli !

Mimi ni mtanzania na ninamuheshimu Nyerere na ninaamini alikuwa kiongozi mzuri na so far sioni kiongozi yeyote aliyekuja baada yake unayeweza kusema anafikia viwango vya Nyerere !

Lissu ameonyesha kwa USHAHIDI kwamba Nyerere alichokisema 1968 alikuwa anasema uongo. Nyerere alisema 1968 kwamba wanzanzibari wakitaka kujiondoa yeye hatawazuia, lakini baadaye (1984) imeonyesha kwamba alichokisema 1968 ilikuwa ni ulaghai/uongo ! Sasa kosa la Lissu ni kitu gani ? Kama Nyerere alisema uongo na Lissu amelionyesha hilo kwa ushahidi, kosa lake nini ?

Huu upuuzi wetu waTz wa kuacha kuambiana ukweli kwa kuogopana ndio unaoangamiza taifa letu !

Lissu omba radhi. Kumtukana Nyerere ni kuwatukana watanzania
 
Tatizo unataka kuchukua vyote kwa maana kuwa unataka kukubaliana na hoja ya upande wa Mh. Lisssu. Vile vile unakubaliana na kile ambacho alikuwa anakijengea hoja ya kukiua katika fikra na mitazamo ya watu. Haiwezekani!.

Mh. Lissu anasema kimantiki kuwa, Mwl. Nyerere alitutapeli sisi Watanganyika na Wazanzibari kuhusiana na Muungano kwa maana kuwa, hata huu unaoitwa Muungano siyo muungano kwa sababu hauna hata hati maalum kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa. Hiyo hati hata Tanzania haipo na wale waliohoji, walifukuzwa na Mwl. Nyerere katika uongozi wakati alishasema huko nyuma kuwa hawezi kumpiga mabomu mtu yeyote anayehoji muungano kwa mapenzi yakena nchi.
 

Sahihi kudanganya? sahihi kuwatia kizuizini wanaohoji? sahihi kuwaondoa nchini wanaokukosoa?

Tuweni wakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…